TANESCO
Official Account
- Jul 12, 2014
- 4,584
- 2,104
Hii sio sahihi kama ni kweli tupatie namba yako ya mita, namba ya simu na eneo tufatilie kwa kuwa bila taarifa kamili uma hauwezi kujua ukweli wa upande wa piliMimi pia ni mhanga wa TANESCO nilifungiwa mita tatu baada ya mudawakaniambia mita moja haiwezi kununua umeme, kwa bahati nzuri namba za mita nilizofungiwa nilikuwa nazo kuangalia ile iliyoko sio ile yangu, kuuliza mpangaji akasema kuna siku TANESCO walikuja kuangalia shoti baada ya hapo miezi miwili baadae mita hainunui umeme. Nikaenda pale Gongo la mboto wananiambia ninunue mita mpya , ikabidi niende makao makuu kutafuta suluhisho, kule ikachukua takriban wiki kupata ufumbuzi na nikafungiwa mita nyingine. Kummbuka mizunguko yote hiyo ilichukua miezi miwili na nusu, kufuatilia zaidi nikaambiwa wakiona kuna mita ina deni kubwa, wanang'oa na kuchukua wanakubadilishia mita ya nyumba nyingine. Kuweni makini mnaporipoti shoti kwani ile mita yangu ilifungwa nyumba ya mtaa wa jirani na akawa ananunua umeme kwa jina langu. Kisa cha pili kwenye nyumba nyingine kule Ubungo ni kuwa nililipia Survey (kumbe hailipiwi) na bado wakaniambia nitume pesa ya taxi ili muweka mita aje, nikagoma kufuatilia wakageuza mada, nyumba haikidhi kufungiwa mita, ila report ya surveyor wao iliidhinisha kufungiwa mita. TANESCO wote wanastahili kupelekwa mikoani, hata mabosi wao hawana msaada kabisa na wanawaogopa wa chini yao.