Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 213
- 490
Tunaendelea kuviona Vilabu vingi vya mpira hapa Tanzania vimekosa kuwa na jicho la ziada katika Jezi mpya katika msimu husika kuzitoa mapema hata kabla msimu mpya kuanza
Eneo la Jezi ni moja ya sehemu ya kupata mapato ambayo yatachangia kwa kiasi kizuri kuendesha klabu katika matumizi yao ya msimu mzima.
Nitoe mfano katika dirisha kubwa la usajili mwaka huu 2024 tumeshuhudia Vilabu vingi vikitambulisha wachezaji wao wapya na jezi za msimu uliopita hakika wamefeli katika eneo hili
Mfano mzuri kwenye hivi vilabu vya Yanga na Simba kama Jicho la mpira wa Tanzania nao wamefeli kwa kiasi kikubwa sana.
Yanga wamemtambulisha Chama na Jezi ya msimu uliopita hakika wangekuwa na jezi mpya wangeuza sana jezi mpya hasa jezi yenye jina la Chama maana ni usajili ambao umekuwa na mapokeo makubwa kwa msahabiki wao lakini hadi sasa hakuna jezi mpya wamefeli sanaa tu!
mfano mwingine msimu kama mmoja uliopita tuliishuhudia Simba wamechelewa kuzindua jezi zao mpya za msimu hadi wanafika kilele cha Simba day wenye jezi mpya ni mashabiki wachache sana na mbaya zaidi walikuwa na mdhamini mpya ambaye ni M bet na jezi walizovaa mashabiki wengi zilikuwa za mdhamini aliye maliza muda wake ambaye alikuwa ni Sportpesa .
Ushauri wangu wanapaswa kuwa na mpango mkakati kuzalisha jezi mpya baada tu ya msimu kumalizika na kabla ya kuanza kutambulisha wachezaji wapya hizo timu ziwe na jezi mpya za msimu husika.