Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran vyapandisha bei ya mafuta

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
2,495
Points
2,000

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
2,495 2,000

Uamuzi wa serikali ya Marekani wa kuziwekea vikwazo nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran umeibua wasiwasi kuhusu usambazaji wa kimataifa wa mafuta ghafi, huku bei ya mafuta ikiwa imepanda kwa kiasi kikubwa.

Marekani Jumatatu imezitaka nchi zinazonunua mafuta kutoka Iran zisite kufanya hivyo kuanzia Mei 1, au zitakabiliwa na vikwazo. Uamuzi huo utamaliza muda wa miezi sita ambapo nchi nane nyingi kutoka bara la Asia, ziliruhusiwa kununua mafuta hayo kutoka Iran.

Wataalamu wa sekta hiyo wamesema Jumatatu, kuwa vikwazo hivyo vinaweza kupelekea kupungua kwa hadi mapipa milioni 1.2 ya mafuta katika soko la kimataifa.

Idadi hiyo inaweza ikawa ndogo zaidi kulingana na jinsi nchi zitakavyoupokea uamuzi huo wa Marekani, na kiasi cha mafuta ambacho Iran itaenedelea kusafirisha.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka kusambaratisha mapato ya Iran yanayotokana an mauzo ya mafuta. Trump anaamini fedha hizo zinatumiwa na Iran kufadhili shughuli za uharibifu katika Mashariki ya Kati na kwengineko.

DW
 

Forum statistics

Threads 1,382,053
Members 526,258
Posts 33,818,407
Top