Vikwazo vya kiuchumi kwa mabilionea Russia ni funzo kwa Mafisadi na viongozi wa serikali mbalimbali duniani wanoiba mali na fedha na kuzificha nje

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Russia inashambuliwa kiuchumi kila kona kwa nguvu zote na matajiri wakubwa wajulikanao kama "Oligarchs" wanazuiwa mali zao katika mabenki mbalimbali duniani.

Hiyo ni kufuatia nchi mbalimbali duniani zikiongozwa na Marekani na Uingereza kuamua kuiweka vikwazo vya kiuchumi Russia baada ya nchi huyo moja ya mataifa makubwa duniani kuivamia nchi jirani ya Ukraine Alhamisi ilopita.

Pia baadhi ya mali kama meli au "Yacht" zinakamatwa zingine zikiwa zimepaki kwa ajili ya matengenezo na meli za mizigo kukamatwa na serikali ya Ufaransa katika kutekeleza masharti ya vikwazo hivyo.

Russia inadai yataka kuhakikisha Ukraine haina zilaha kali za maangamizi, haina nguvu yoyote ya kijeshi na pia haina watu wenye misimamo ya kinazi na kifashisti.

Lakini huku vikwazo hivyo vikizidi kuimarishwa kuna somo ambalo viongozi wengi duniani ambao wamezoea kuiba mali katika nchi zao na kuzificha katika nchi za Ulaya khasa Ulaya Magharibi, kwa sasa wamekuwa na tumbo joto.

Hali hiyo ni kutokana na nchi za Ulaya magharibi kuamua kuangalia fedha zinazomilikiwa na watu mbalimbali ambao wana mahusiano na uongozi wa Kremlin.

Lakini zoezi hilo la kutaka kuzuia fedha kwenye mabenki au mali (kama nyumba) haliwezi kutekelezwa leo wala kesho, bali laweza kuchukua miezi kadhaa na hata mwaka au zaidi kutokana na mapingamizi ya kisheria kutoka kwa wenye mali hizo.

Tayari wanasheria nguli wa masuala ya fedha na usalama wa mali kwa matajiri wamekuwa wakisubiria kuzuia hatua zozote zisizo na haki kisheria kuzuia mali hizo kwa kusisitiza uwepo wa sababu za kisheria kwa serikali kufanya hivyo.

Switzerland ikiwa ni moja ya nchi hizo zilizotangaza kuzuia mali (freezing assets) imewalenga baadhi ya hao mabilionea wa Russia, marafiki zao na familia zao.

Kwa mujibu wa SNB yaani benki kuu ya Uswiss,mwaka 2020 mabilionea hao wa Russia walikuwa wana kiasi cha faranga za Uswiss bilioni 10.4 au dola bilioni 11.24 katika mabenki ya Switzerland.

Viongozi wengi duniani ambao hujilimbikizia mali na kisha kuwekeza katika nchi za ughaibuni kwa sasa (inasemwa kuwa) wanapanga mipango mipya juu ya kukabiliana na matatizo kama haya.

Hiyo ni kwasababu haujulikani sheria zinazorekebishwa sasa zitaelekeza hatua za kuzuia fedha hizo kwa watu wote au wale matajiri wa Russia pekee au akina nani.

Sani Abacha aliekuwa raisi wa Nigeria alipofariki aliacha kiasi cha dola milioni 267 katika kisiwa cha Jersey, dola milioni 480 katika mabenki ya Marekani na fedha zote hizo hazikurudi Nigeria bali kugawiwa katika ya serikali za nchi hizo za mamlaka za nchi hizo yaani Marekani, Jersey na Nigeria ambayo inajulikana fedha hizo zingeishia wapi.

Mwaka 2000 Switzerland baada ya kujivuta sana kutoa kiasi halisi cha fedha ambazo Abacha aliziweka katika mabenki ya nchi hiyo walikuja kusema kulikuwa na kiasi cha dola milioni 300 tu! na ambazo pia zilihamishwa kwenda katika mabenki nchini Uingereza ambayo nayo ilichukua muda mrefu (miezi 4) kujibu barua ya maulizo kutoka kwenye serikali ya Nigeria.

Lakini baadae mwaka 2015 Uswiss walikuja kurudisha rasmi fedha kiasi cha dola milioni 380 kwa serikali ya Nigeria baada ya kuzikomboa fedha hizo kutoka katika benki moja nchini Luxembourg, baada ya kuzikusanya tangu mwaka 2006. Hiyo ilikuwa baada ya Serikali ya Nigeria kukubaliana na familia ya Abacha na kufuta mashitaka dhidi ya mtoto wake aitwae Abba Abacha.

Fedha hizo (dola milioni 380) ni mbali ya kiasi cha dola milioni 700 ambazo Switzerland ilizirudisha kwa serikali ya Nigeria, fedha ambazo Sani Abacha aliekuwa kiongozi wa kijeshi alizificha katika mabenki mbalimbali jijini Geneva.

Switzerland ilibadili sheria ya usiri wa kanuni za kibenki au "Banking Secrecy Rules" ambapo kunapokuwepo uchunguzi wa uhalifu wa kibenki au wizi wa kalamu, mabenki hupaswa kutoa taarifa za washukiwa walo na akaunti katika mabenki hayo, ilimradi mwanasheria raia wa Uswiss ndie aombe taarifa hizo kwa kuweka ombi maalum la kisheria.

Serikali za Marekani na Uingereza nazo zimekuwa na wakati mgumu wa kuchambua sheria za mabenki ili kuzuia vitendo vya utakatishaji fedha na kuweka vikwazo kwa baadhi ya matajiri wakubwa wenye mahusiano na serikali ya Russia au raisi Putin kwa kuzuia fedha zao.

Lakini nchi nyingi zinaishangaa Uingereza kwa kusuasua katika kutekeleza vikwazo kwa kuwawekea vikwazo matajiri wakubwa waishio nchini humo.

Hadi sasa ni ni matajiri wakubwa sita tu ndo walokumbwa na dhahama hizo za vikwazo akiwemo bwana Alisher Usmanov ambae meli yake ya kupumzikia iitwayo Dilbar yenye thamani ya dola milioni 600 imekamatwa na serikali ya Ufaransa ikishirikina na serikali ya Ujerumani.

Lakini hapohapo chama cha wahafidhina kimekuwa na wakti mgumu kujitetea kuhusiana na mchango wa pauni milioni 2 ambazo zimetolewa na mwanamama raia wa Russia aitwae Lubov Chernukin tangu mwaka 2012.

Isitoshe bilionea Roman Abramovich amepewa mwanya wa kuiuza timu ya mpira ya Chelsea ili kuokoa fedha zake pauni milioni 2 ambazo anaidai Chelsea na tiyari amepata wateja ambao wameweka mezani pauni bilioni 3 kutaka kuinunua timu hiyo.

Hivyo, suala hili la vikwazo vya kiuchumi wanowekewa baadhi ya watu binafsi na makampuni yao kadha wa kadha yaonyesha kuwa ni dalili ya mambo mengine kuibuliwa kuhusiana na sheria mbalimbali za uwekaji fedha katika mabenki, uhamishaji (bank transfer) na udhibiti wa utakatishaji fedha.

London ni moja ya miji ambayo inatuhumiwa kuwa ni kitovu cha utakatishaji fedha zinodaiwa kuibwa kutoka Russia na nchini zingine mbalimbali duniani ambapo fedha hizo hutumika katika manunuzi ya majumba (mansions) na vipande vya ardhi, pamoja na uendeshaji wa biashara zingine mbalimbali kubwa na ndogo.

Serikali za nchi za magharibi kwa kuweka vikwazo kwa washirika wa raisi Putin na kuangalia upya sheria mbalimbali zinohusiana na masuala ya fedha kunaweza pia kutumika kama mwanya wa kuhakikisha fedha zinoingizwa barani Ulaya na Marekani zinaangaliwa kwa jicho la tatu.

Hali hiyo bila shaka itapelekea watu wengi wenye akaunti mbalimbali katika sehemu mbalimbali duniani kuanza kuingizwa na wasiwasi na kupanga namna ya kurekebisha mabenki hayo.
 
Wakati mwingine nikizitazama nchi za ulaya especially ya magharibi nawaona wamejaa unafiki kupitiliza, akitokea yeyote kwenye kundi lao akafanya jambo baya kama uvamizi kwa nchi nyingine hawafanyi lolote kukemea mfano. uvamizi wa Marekani Iraq, Libya, etc.

Lakini akitokea asie wa kundi lao akavamia nchi nyingine, hapo ndipo unafiki wao unapoonekana wazi, wataweka vikwazo ikiwemo kuzuia mali, watafanya kila aina ya jambo ilimradi kuidanganya dunia wao ndio mababa wapenda amani duniani, kumbe ukweli ni kinyume chake.

Hata hilo wazo ulilokuja nalo mleta mada juu ya mafisadi wapate funzo napata shaka kama kweli litaweza kutokea kwa hao jamaa, kama hizo fedha za ufisadi huifadhiwa kwenye mabenki yao na wao ndio hupata faida, siamini kama wanaweza kuzuia hizo mali, labda nchi moja tu ya Uswisi, lakini sio hao wengine.
 
Nchi za magharibi ndio ' safe heaven' za mafisadi kutoka Africa, Asia, Urusi na kwingineko duniani kuficha mali zao, tena wametajirika mno na huu uhuni.....

Ina maana Urusi isingeivamia Ukraine hao mafisadi wasingeguswa?

.... isitoshe wapo wengi tu kutoka Africa (hasa viongozi) wameficha mali walizopora kwenye mataifa yao ila mbona wao hawaguswi?.

.....kwanini ni Urusi pekee? Au sababu kawakera?.....wanafiki Sana hawa mabeberu.....
 
Fisadi Andrew Chenge na yeye pesa zake pound milioni nne alizofisadi akiwa mwanasheria mkuu wa Serikali ya Tanzania alizoficha uingereza zililirudishwa Tanzania na kukabidhiwa kwa Serikali

Tanzania kuna Tajiri mmoja ana biashara zake kubwa na Urusi pesa zake nyingi ziko mabenki ya nje sijui kama atanusurika ngoja tuone
 
Inawezekana baadhi ya misaada tunayopewa nchi za kiafrika huwa ni pesa za watu wa nchi zetu wenyewe hasa waliofariki wakiwa na ela nyingi sana nje... Serikali hukosa power ya kuzifuatilia sababu wengi wao huwa hawataki ijulikane na Serikali umiliki wa pesa na mali zao nje. Africa bado safari ni ndefu.
 
Ni kweli yawezekana.

Ni pia yawezekana kupewa fedha kiduchu kuliko kiasi halisi ambacho kimezalisha faida kuwa kwa mabenki hayo.
 
thanks for your article well read. spot on.
emoji122.png
emoji122.png
emoji122.png
Mkuu, nashukuru sana kwa compliment.
 
Fisadi Andrew Chenge na yeye pesa zake pound milioni nne alizofisadi akiwa mwanasheria mkuu wa Serikali ya Tanzania alizoficha uingereza zililirudishwa Tanzania na kukabidhiwa kwa Serikali

Tanzania kuna Tajiri mmoja ana biashara zake kubwa na Urusi pesa zake nyingi ziko mabenki ya nje sijui kama atanusurika ngoja tuone
Sheria ndo zimeanza kubadilishwa lakini huenda asiathirike sana ila kwa kiasi fulani kutakuwa na mlolongo khasa kwenye kuhamisha fedha hizo.
 
Wakati mwingine nikizitazama nchi za ulaya especially ya magharibi nawaona wamejaa unafiki kupitiliza, akitokea yeyote kwenye kundi lao akafanya jambo baya kama uvamizi kwa nchi nyingine hawafanyi lolote kukemea mfano. uvamizi wa Marekani Iraq, Libya, etc.

Lakini akitokea asie wa kundi lao akavamia nchi nyingine, hapo ndipo unafiki wao unapoonekana wazi, wataweka vikwazo ikiwemo kuzuia mali, watafanya kila aina ya jambo ilimradi kuidanganya dunia wao ndio mababa wapenda amani duniani, kumbe ukweli ni kinyume chake.

Hata hilo wazo ulilokuja nalo mleta mada juu ya mafisadi wapate funzo napata shaka kama kweli litaweza kutokea kwa hao jamaa, kama hizo fedha za ufisadi huifadhiwa kwenye mabenki yao na wao ndio hupata faida, siamini kama wanaweza kuzuia hizo mali, labda nchi moja tu ya Uswisi, lakini sio hao wengine.
Inaweza kutokea maana sheria wanozitunga sasa hivi kuhusu utakatishaji fedha zitakuwa ngumu sana.

Kwa mfani watataka kuona uthibitisho wa ulipozitoa kabla ya kuziweka huko nje, kwa mfanio kisiwani Jersey ambayo imekubaliana na Marekani na nchi za magharibi kufanya "data sharing".
 
Hii ni aina mpya ya dhuluma
Kwanini usiwape option ya kutoa pesa zao ndo wafunge hizo aiaunti
 
Hii ni aina mpya ya dhuluma
Kwanini usiwape option ya kutoa pesa zao ndo wafunge hizo aiaunti
Siku si nyingi uchumi wa nchi za Magharibi na Marekani utayumba na kutakuwa na matatizo kila kona.

Ni kweli kitendo wanachofanya (kuzuia fedha na mali za watu ni uporaji).

Kuna waziri mmoja wa Uingereza amedai kuwa nyumba za "Oligarchs" zikitaifishwa zitumike kuhifadhi wakimbizi wa Ukraine.

hata wakati wa vita kuu ya kwanza na ya pili kulifanyika uvunjaji mabenki na uporaji mali (looting) na leo hii usishangae watu fulani duniani wana pesa na ndo wanoendesha dunia.
 
Wakati mwingine nikizitazama nchi za ulaya especially ya magharibi nawaona wamejaa unafiki kupitiliza, akitokea yeyote kwenye kundi lao akafanya jambo baya kama uvamizi kwa nchi nyingine hawafanyi lolote kukemea mfano. uvamizi wa Marekani Iraq, Libya, etc.

Lakini akitokea asie wa kundi lao akavamia nchi nyingine, hapo ndipo unafiki wao unapoonekana wazi, wataweka vikwazo ikiwemo kuzuia mali, watafanya kila aina ya jambo ilimradi kuidanganya dunia wao ndio mababa wapenda amani duniani, kumbe ukweli ni kinyume chake.

Hata hilo wazo ulilokuja nalo mleta mada juu ya mafisadi wapate funzo napata shaka kama kweli litaweza kutokea kwa hao jamaa, kama hizo fedha za ufisadi huifadhiwa kwenye mabenki yao na wao ndio hupata faida, siamini kama wanaweza kuzuia hizo mali, labda nchi moja tu ya Uswisi, lakini sio hao wengine.
Huu unafiki siyo kwa nchi za Magharibi tu, Israeli aliposhambulia maeneo ya Palestina, nchi za kiarabu zilikuwa na maandamano karibia kila siku wakipinga uvamizi wa Israeli. Je umewaona hawa waarabu popote wakiandamana kupinga yanayoendelea huko Ukraine? Salman anasema Russia ana haki ya kujilinda huku Uturuki akiwa yuko busy kuuza drones kwa Ukraine.
Somo la kujifunza ni kuwa, watu wa asili flan wakishindwa kusimama pamoja na kutetea haki na maslahi yao, wasitegemee maajabu kutoka kwa watu wengine. Siku ambayo Afrika itajitambua na kusimama kama bara, ikaweka mbali misukumo ya West, America, Asia, Arabia, basi tutaweza kupiga hatua.
 
Siku si nyingi uchumi wa nchi za Magharibi na Marekani utayumba na kutakuwa na matatizo kila kona.

Ni kweli kitendo wanachofanya (kuzuia fedha na mali za watu ni uporaji).

Kuna waziri mmoja wa Uingereza amedai kuwa nyumba za "Oligarchs" zikitaifishwa zitumike kuhifadhi wakimbizi wa Ukraine.

hata wakati wa vita kuu ya kwanza na ya pili kulifanyika uvunjaji mabenki na uporaji mali (looting) na leo hii usishangae watu fulani duniani wana pesa na ndo wanoendesha dunia.
ni kweli yetu macho
 
Back
Top Bottom