Vikwazo vya Kikatiba katika kuleta Maendeleo na Demokrasia

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,943
Kwa muda mrefu tumeilalamikia katiba yetu kwamba inabana demokrasia. Hata hivyo ni mara chache mno tumeweza kutaja vipengele ambavyo ni tatizo. Leo nimeamua kwa kuanzia kutajia ibara angalu mbili ambazo mimi ninaona ni sumu kwa demokrasia ya vyama vingi na vinafaa kubadilishwa.

1)Ibara ya 1 iayozungumzia misingi ya katiba. Nafikiri hakuna haja ya kutaja ujamaa kama sehemu ya misingi. mambo ya itikadi wangeachiwa vyama vya siasa kama nyenzo yao ya kuomba ridhaa. Mambo ya itikadi hayawezi kuwa mambo ya kitaifa na hivyo hakuna haja kuyatamka kwenye katiba.

2) Katika ibara ya 39 (1) kinachozungumzia sifa za kuchaguliwa kuwa Rais, nafikiri kuna haja ya kupunguza umri wa kukubalika kuwa Rais kutoka miaka 40 ya sasa hadi angalau 35. Inawezekana mwaka 1977 ilieleweka kuweka huo umri, lakini sasa umefika wakati tukakibadilisha hiki kipengele

3) Ibara ya 40(6) pamoja na mambo mengine inakataza mtu yeyote kwenda mahakamani kuhoji matokeo ya kura za urais mara Tume ya Uchaguzi ikishakutangaza matokeo husika. Hiki nafikiri ni kipengele kibovu na hatari mno kwa demokrasia na kinatoa mwanya watu kuiba kura za urais bila woga wala kificho. Ibara hii inahitaji mabadiliko ya haraka. Actually ni sisi peke yetu katika Jumuiya ya Madola wenye kipengele hiki.

Kwa leo naishia hapa. Nakaribisha maoni zadi.
 
Kitila Mkumbo,

Mimi naomba kutofautiana na wewe kidogo hasa ktk hiki kipengele cha kwanza.

UJAMAA - Hii ni dira ya kitaifa kisiasa, hii haina maana kabisa kwamba inakataza kuwepo na mtazamo mwingine nje maadam unatupeleka bado kuwa WAJAMAA. Zipo nchi za magharibi ambazo zimetumia dira hii kuhakikisha kwamba wananchi wake wote wanafaidika kwa kile kinachopatikana. Na labda niseme angalau tungekuwa kweli wajamaa ama mabepari ingejulikana wapi dira ya nchi inakokwenda lakini reality imesimama kwamba tumepoteza kabisa mwelekeo.

Huo Ujamaa umebaki itikadi ndani ya Katiba na hata hatuwezi kusema dira ya kitaifa imebadilika kwani hatuna kabisa ibara ya dira inayotumika. Sisi sio mabepari wala wajamaa.. ila nchi isiyokuwa na mwelekeo. Ubepari pia hauendeshwi hivi... kwani TZ ni nchi maskini na wala hatuelekei kuwa matajiri kitaifa. Uzalishaji wetu hauna malengo ya kuitajirisha nchi ila kuifilisi nchi na watu wake. Kwa hiyo basi hatuwezi kuwa nchi pekee duniani ambayo haina mwelekeo, na tukiondoa Itikadi kabisa ktk katiba mbona tutakuwa viumbe wasiokuwa na dini?..Labda nambie unayo mapendekezo ya dira ya kitaifa ambayo itachukua nafasi ya Ujamaa ktk katiba yetu hiyo - ibara ya kwanza.

Maoni yangu mimi, nadhani jambo la muhimu hapa ni kuhakikisha kweli Ujamaa unalipa! kodi kubwa wanazokatwa matajiri ziwe ktk malengo ya kujenga maisha ya wananchi na sio utajiri wa baadhi kwa kutumia dhulma hali wakiiacha nchi na watu wake maskini.

Nadhani, mabepari wanaamini maendeleo ni Utajiri wa nchi kwa hiyo malengo yao yote ni kuitajirisha nchi kwa kila mbinu. Nchi ni watu na watu ni nchi, hali Wajamaa wanaamini maendeleo ni Utajiri ni watu wake kwa kila kipengele ndio unawakilisha sura ya nchi.
 
Mkandara:

Nimejaribu kupitia katiba za nchi kama tano , mbili za nchi zilizoendelea (USA na UK-ambayo haijaaindikwa rasmi) na tatu zinazofanana na sisi (RSA, Uganda, na Kenya). Hakuna hata sehemu moja wanapo-mention itikadi. Misingi ya katiba yao inaeleza kuzingatia demokrasia, haki za binadamu na mambo kama hayo.

Hakuna faida kuandika mambo kwenye Katiba ambayo kwanza hatuyatekelezi, na pili hakuna msimamo wa kijamii.

Kuhusu swali lako kuhusu mwelekeo wa Taifa; hili wanazuoni na wananchi mbalimbali nchini walikwisha kuliona na wakasema tukae chini kama Taifa, tujadili ili kupata msimamo wa pamoja kama Taifa tunapotaka kwenda. lakini mara zote watawala wamekataa mjadala wa kitaifa.

Na labda niseme kuwa kwa maoni yangu itikadi haina uhusiano na mwelekeo wa kitaifa. Na wala kuwa na itikadi haimanishi kwamba ndo mmepata mwelekeo. Mfano mzuri ni sisi ambao tumeweka ujamaa kwenye katiba lakini kila mtu anapuyanga kivyake; mwanachi huku, wanasisasa kule, na serikali yao pale!
 
Kitila Mkumbo,

Hapa sasa umeleta hoja ambayo nilikuwa nataka kuisema toka mwanzo.

Umejaribu kupitia katiba za nchi nyingine!... why?

Nadhani jibu lake rahisi sana kwamba sisi hatuwezi kutunga katiba kulingana na mazingira yetu ila KUIGA nchi nyingine bila kufahamu ya kwamba hakuna katiba ya nchi mbili zinayofanana labda tu nchi hizo zili/zimetawaliwa. Nchi za Kisultani zina katiba iliyojengwa kulingana na falme zao, hata hizi zimetofautiana. nchi kama Israel hadi leo haina kabisa katiba zaidi ya kutumia baadhi ya sheria za bunge lao Knesset.

Na kuhusu hoja unapouliza - kwa nini iwepo ktk katiba hali hakuna mtu anayeifuata?.. hii kweli kabisa upo sahihi na ukiangalia kiundani utakuta sababu kubwa bado ni hiyohiyo... TUNAIGA kila kitu cha wenzetu (nchi za magharibi) ambao hawana dira ya kitaifa bila kujua ya kwamba wao hawana haja ya kusema dira yao kwani wenzetu wanafahamu wapi wametoka na wapi wanakwenda. Na tunaweza kuwauliza vilevile kwa nini wameweka ibara zinazosisitiza kutokuwepo na ubaguzi hali wao bado wabaguzi. Wao wametushinda sana kwa kutumia lugha hizi za biashara kwa malengo! kuwepo ama kutokuwepo haina maana kabisa nao wanatekeleza, isipokuwa wao hufanya kwa malengo na sisi hatuna malengo.

Binafsi sioni kosa kabisa la kuwepo ibara hiyo, isipokuwa tu ibara hiyo ifuatwe na kuwepo sheria za kuilinda ibara hiyo kama nchi za Nordic na Canada hata kama chama kitakachoshika uongozi ni cha upande wa pili. RSA, Kenya na Uganda zina matatizo yao makubwa sana ambayo katiba zao zimejengwa aidha kwa kuiga nchi zilizowatawala na kuhakikisha wanalindwa. Sisi hatuna mazingira kama yao na wala demokrasia kwao haikusimama vizuri kufikia sisi tuseme wao ni mfano bora.
 
Sijawahi kukaa Kenya ila kwa kupitia kikazi tu; nimewahi kukaa pale Nairobi na Mombasa kwa siku si zaidi ya tatu nikiwa ama mkutanoni au matembezini tu. Sina ndugu yeyoite Kenya ila nina rafiki mmoja anayefundisha Mathematics pale Nairobi University, na rafiki mwingine anyefundisha pale Egerton University. Yaliyotokea Kenya wiki hii yananiliza kama vile yametokea kijijini kwetu huko Igalula, Tabora.


Wakati sijamaliza kufuta machozi yanayonichurizika mbele ya wanangu kufuatia yaliyotokea Kenya ambako sina ndugu, napenda ndugu zangu tupige bongo kutafuta mbinu za kupambana na hili tatizo sugu lililojitokeza na linaloeleka kudumuza maendeleo ya demokrasi barani Afrika lijulikanalo kama wizi wa Kura. Ni njia zipi tuazoweza kutumia kupambano nalo.

(a) Kila mpiga kura abaki na kopi ya kura yake aambiwe aitunze hadi pale atakapotangaziwa kuwa swala la uchaguzi limekwisha salama.

(b) Kupiga kura tutumie wino ambao unabadilika rangi kadiri ya muda unavyopita. Tuwe na namna ya kusynchronize official tally na records za individual wapiga kura.

(c) Kura zote zihesabiwe kwenye kituo cha kupigia kura na sizitangazwe hadi dakika ya mwisho ya kutoa matangazo kwa taifa ndipo kila kituo kitoe tally yake.

...


...


Najua kuna njia nyingi sana tunazoweza kujijengea kupambana na uhalifu huu unaojitokeza dhidi ya demokrasia barani kwetu. Naomba tutoe michango ya mawazo yetu ya namna gani tunaweza kupambana na tatizo hili kisayansi bila kuacha ndugu zetu wauwae na nyang'au wa madaraka kama tunavyoona Kenya sasa hivi...
 
Sijawahi kukaa Kenya ila kwa kupitia kikazi tu; nimewahi kukaa pale Nairobi na Mombasa kwa siku si zaidi ya tatu nikiwa ama mkutanoni au matembezini tu. Sina ndugu yeyoite Kenya ila nina rafiki mmoja anayefundisha Mathematics pale Nairobi University, na rafiki mwingine anyefundisha pale Egerton University. Yaliyotokea Kenya wiki hii yananiliza kama vile yametokea kijijini kwetu huko Ilula, Tabora.


Wakati sijamaliza kufuta machozi yanayonichurizika mbele ya wanangu kufuatia yaliyotokea Kenya ambako sina ndugu, napenda ndugu zangu tupige bongo kutafuta mbinu za kupambana na hili tatizo sugu lililojitokeza na linaloeleka kudumuza maendeleo ya demokrasi barani Afrika lijulikanalo kama wizi wa Kura. Ni njia zipi tuazoweza kutumia kupambano nalo.

(a) Kila mpiga kura abaki na kopi ya kura yake aambiwe aitunze hadi pale atakapotangaziwa kuwa swala la uchaguzi limekwisha salama.

(b) Kupiga kura tutumie wino ambao unabadilika rangi kadiri ya muda unavyopita. Tuwe na namna ya kusynchronize official tally na records za individual wapiga kura.

(c) Kura zote zihesabiwe kwenye kituo cha kupigia kura na sizitangazwe hadi dakika ya mwisho ya kutoa matangazo kwa taifa ndipo kila kituo kitoe tally yake.

...


...


Najua kuna njia nyingi sana tunazoweza kujijengea kupambana na uhalifu huu unaojitokeza dhidi ya demokrasia barani kwetu. Naomba tutoe michango ya mawazo yetu ya namna gani tunaweza kupambana na tatizo hili kisayansi bila kuacha ndugu zetu wauwae na nyang'au wa madaraka kama tunavyoona Kenya sasa hivi...

Kichuguu,

Njia zote ulizozisema haziwezi kuondoa wizi wa kura Afrika ambao unapangwa na watawala na kubarikiwa na usalama wa taifa na tume za uchaguzi.

Watu wanaobadili matokeo hata bila aibu kutoka 20,000 kwenda 50,000, utapambana nao vipi?

Ukienda mahakamani ndio umejimaliza kwasababu katiba imetungwa ili kuwalinda, wamechagua majaji kuwalinda na hata hakuna muda wa kukata rufaa kabla matokeo hayajatangazwa na yakitangazwa hakuna chombo kinachoweza kumwondoa rais mahakamani.

Dawa pekee ni moja, ni kuwaondoa kwa nguvu. Wakenya lazima wamwondoe Kibaki kwa nguvu hata kama watu watakufa, matokeo yake kuna watu watakufa leo lakini watakuwa wameondoa hili tatizo kwa miaka na miaka maana hakuna atakayediriki tena. Kibaki akibaki madarakani, kuna kiongozi mwingine atakuja na kufanya hivyo hivyo akitegemea yataisha baada ya siku tatu.

Angalia Zanzibar, mwaka 1995, CUF waliombwa watulie na katiba na tume ya uchaguzi vitarekebishwa. Mwaka 2000, ikatokea tena na watu wakafa, wakaanzisha muafaka, mwaka 2005 watu wakafa tena. Nina uhakika watu watakufa tena 2010 huko Zanzibar.

Laiti mwaka 1995, Karume angeondolewa hata kwa mapanga, huenda CCM wangekuwa wamejifunza na kuacha huu ujinga.

Waafrika tumezidi uwoga, lazima tuwe tayari kutetea haki zetu hata kwa kutumia nguvu. Ni sawa na mtu anakuja kunyanyasa familia yako nyumbani, je utafanya nini?

Hili ni fundisho kwa CCM na wale washabiki wao kwamba siku itafika, wananchi kama wataona mmewaibia, wataenda mitaani na kuchukua nchi yao.

Watu wanashangilia kuua vibaka barabarani, vibaka ambao wakifikishwa polisi kuna angalau asilimia 50 kwamba watachukuliwa hatua. Lakini tunakaa kimya wakati vibaka wakubwa wa siasa akina Karume, wanaiba haki za wananchi wote. Hawa ni wabaya zaidi ya wale wanaodokoa pesa mifukoni.
 
Kichuguu
Kama ingekuwa ni uchaguzi unaofanyika Tanzania au Kenya, na wagombe ni kutoka makundi mawili ya Wakoloni wachache weupe na wazalendo wenghi weusi hiyo mbinu yako ingepigiwa makofi sana na wewe ungebebwa kama hero, kwa Tanzania ya sasa ambayo mafisadi ndio wanaofaidi nchi, na kwa Kenya ambako mafisadi kama kina Moi wanalindwa na Kibakis, hili jambo haliwezekani na halitakubaliwa hata kidogo kwa sababu halitoi loophole ya wizi wa kura, kwa hiyo this is just a pipe dream, it will never happene in Tanzania, labda Mungu afe.
 
Mimi napendekeza mawili. Moja, wakati wa uchaguzi, tume ya uchaguzi inatakiwa kushirikisha external commissioners. Hawa external commissioners wanatakiwa kutambuliwa na katiba ya nchi. Kwa nini nimependekeza hivyo?. Jibu ni rahisi. Ukifuatilia chaguzi nyingi barani africa, kwa kawaida kuna mixed results. Tarakimu za external observers ni tofauti na zile za tume ya uchaguzi. Hivyo basi, kama external observers wangelikuwa na sauti katika kutangaza matokeo ya uraisi, nadhani itakuwa ni vigumu sana kuchezea tarakimu.

Mbili. Tunaweza kuiga utaratibu wa nchi za magharibi ambapo matokeo ya kura hutangazwa moja kwa moja kutoka katika kila kituo kupitia katika television. Hapa kazi ya tume itakuwa ni kujumlisha tarakimu zilizotoka katika vituo na si tume kuwa wasemaji wa mwisho. Uzuri wa utaratibu huu ni kuwa kila mwananchi atapata nafasi ya kusikia/kuona moja kwa moja idadi ya kura kutoka katika kila jimbo. Utaratibu huu utapunguza ufisadi wa kura endapo serikali iliyopo madarakani itakuwa imekusudia kucheza rafu.

MSISITIZO KATIKA HOJA NAMBA 2. MAJIMBO YAWE NA NGUVU KULIKO TUME YA UCHAGUZI KATIKA KUTANGAZA MATOKEO. YAKITOKEA MATATIZO YEYOTE, MAJIMBO YAWE NA SAUTI KUJIBU HOJA.
 
Wasimamizi wote wa kuhakikisha uchaguzi unakuwa free and fair watoke nje ya nchi na pia watakaohesabu kura wote watoke nje ya nchi hasa katika Western Hemisphere. Hapa ndio tunaweza kupambana na kuondoa kabisa wizi wa kura.

Mafisadi na wezi wa kura watalikataa hili kwa kudai sisi ni huru hatuna haja ya kuita wageni waje kutuhesabia kura. Ni vigumu kweli kweli.

Jumuiya ya kimataifa nayo inaweza kuamua kuzitenga nchi ambazo uchaguzi hauko free and fair. Viongozi wa serikali hizi wasikaribishwe katika nchi za magharibi na wala wasipewe misaada au mikopo yoyote toka jumuiya na benki za kimataifa.

Lakini kuna nchi ambazo zitapenda kuwanunua mafisadi na wezi wa kura kama vibaraka vyao kwa manufaa ya nchi hizo.
 
Wasimamizi wote wa kuhakikisha uchaguzi unakuwa free and fair watoke nje ya nchi na pia watakaohesabu kura wote watoke nje ya nchi hasa katika Western Hemisphere. Hapa ndio tunaweza kupambana na kuondoa kabisa wizi wa kura.
Mafisadi na wezi wa kura watalikataa hili kwa kudai sisi ni huru hatuna haja ya kuita wageni waje kutuhesabia kura. Ni vigumu kweli kweli.

Jumuiya ya kimataifa nayo inaweza kuamua kuzitenga nchi ambazo uchaguzi hauko free and fair. Viongozi wa serikali hizi wasikaribishwe katika nchi za magharibi na wala wasipewe misaada au mikopo yoyote toka jumuiya na benki za kimataifa.

Lakini kuna nchi ambazo zitapenda kuwanunua mafisadi na wezi wa kura kama vibaraka vyao kwa manufaa ya nchi hizo.

Wazo lako ni zuri sana na nakubaliana lao kabisa. Hata hivyo, nadhani badala ya kuita nchi za magharibi labda tuunde kamati ya usimamizi wa uchaguzi katika AU ambapo wajumbe wake watakuwa wanachaguliwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika kusimamia uchaguzi na kutangaza matokeo. Wajumbe hawa wasiwe na madaraka yoyote ya kisiasa nchini kwao na wasitoke katika nchi jirani na nchi yenye uchaguzi. Uteuzi wa kamati hii ufanye kwa kuangalia conflict of interest kwa makini sana.
 
Wazo lako ni zuri sana na itakuwa vizuri hawa wajumbe wa kamati hii wawe wanalipwa vizuri na AU ili kuhakikisha hawapewi rushwa na mafisadi na wezi wa kura.
 
Wasimamizi wote wa kuhakikisha uchaguzi unakuwa free and fair watoke nje ya nchi na pia watakaohesabu kura wote watoke nje ya nchi hasa katika Western Hemisphere. Hapa ndio tunaweza kupambana na kuondoa kabisa wizi wa kura.
Mara zote ambazo kumetokea vurugu huko zenj, zilichangiwa kwa kiasi kikubwa na hao ambao wanaitwa waangalizi wa kimataifa. Mara zote wao hua ni maadaui wa chama kilichopo madarakani, na wana nguvu kubwa za kushawishi chini ya mgongo wa uangalizi wa kimataifa.

Iwapo vyama vyote hutoa wasimamizi wao kuanzia upigaji kura,uhesabu kura na utangazwaji wa matokeo ni nini hasa nafasi ya hao waangalizi wa kimataifa?
 
Tatizo hapa ni kwamba hivyo vituo vya kupigia kura ni vingi kuliko idadi ya wawakilishi wa vyama katika usimamizi wa uhesabu kura. utakuta kuna naeneo vyama vya upinzani ama vina share wasimamizi au hakuna kabisa. Posho wanazolipwa pia ni kidunchu mno kiasi kwamba ni rahisi kurubuniwa na chama tawala kuhalalisha kura za uizi.m fano kwa uchaguzi wa 2005 kuna vituo utakuta mgombea flani ana kura zero au moja. Utaona watu wanashangaa, mbona mimi nilimpigia flani lakini hana kura inamaana iliharibika au haikuhesabiwa kabisa!?

Watawala wetu na vyama vyao wako makini sana maana wanajua akitoka kurudi tena kwenye utawala sio rahisi, maana hata hao walio nje tunawaona wanademokrasia kwa vile hawajashika usukani, wakipewa nchi hawana jipya watataka nao watawale milele.

Njia muafaka ni watu kupiga kura kwa kutumia eletronic vote cards. kama serikali imeweza kuingia gharama ya kutengeneza daftari la wapiga kura basi wajenge vituo vya kudumu vya kupigia kura au Mobile Voting Centres na kuacha huu utaratibu wa kutumia mashule na vibanda boxi.

Wakati wa kupiga kura AVM (Automatic Voting Machine) itamtaka mtu atumbukukize card yake itasoma gumba lake itafanya validation then itamletea mpiga kura picha za wagombea kama Mtu anapiga mara zaidi ya moja card yake itakataliwa. mpiga kura atakapokubalika kuwa ni halali basi picha za wagombea zitajitokeza kwenye screen kisha atagusa picha ya mgombea anaemtaka kama ishara ya kumchagua, kwa wenye ulemavu wa macho akigusa picha mashine itasema jina la mgombea aliyeguswa. kura ikiwa successfully machine mtampatia mpiga kura receipt kama uthibitisho kuwa kura yake ni valid na imeenda kwa mgombea aliyemtaka. Technologia hii ikifanyiwa kazi kwa umakini hakuna mtu atakeiba kura wala kura kuharibika, hakutahitajika wasimamizi wa vyama zaidi ya mtu mmoja tu kwenye kila mashine wa kuwaelekeza wenye vichwa vizito kuelewa utumiaji wa mashine. Mashine hizo zitafanya kazi kama za ATM za Benki. Hakutahitaji wahesabu kura maana zitajihesabu zenyewe kila kura inapoingia. Hii inamaanisha kuwa wapiga kura wakiisha katika vituo vyote saa hiyo hiyo tume itakuwa na majibu ya washindi.

Tatizo ni kwamba kiongozi gani atakekubali kuweka system ya kummaliza mwenyewe? Visingizio vingi vya uwezo wa kifedha uendeshaji vitajitokeza kuzuia mradi. lakini ukweli ni kuwa ziko namna za kuondoa kabisa uizi wa kura kama Serikali ikiamua kwa nia njema
 
Mara zote wao hua ni maadaui wa chama kilichopo madarakani, na wana nguvu kubwa za kushawishi chini ya mgongo wa uangalizi wa kimataifa.

Iwapo vyama vyote hutoa wasimamizi wao kuanzia upigaji kura,uhesabu kura na utangazwaji wa matokeo ni nini hasa nafasi ya hao waangalizi wa kimataifa?

Kama una ushahidi wa kuthibitisha kwamba wasimamizi wa kimataifa ni maadui wa chama kilicho madarakani basi tafadhali uweke hapa ushahidi huo ili tuujadili.

Pamoja na kuwa vyama vyote hutoa wasimamizi wao tume ya uchaguzi inaundwa na chama tawala. Wajumbe wa tume hii wameshawahi kutumiwa Tanzania, Kenya na kwingineko katika kuiba kura. Pamoja na kwamba vyama vya upinzani hutoa wasimamizi wao, lakini chama tawala kwa kutumia vyombo vya dola hutoa vitisho vya namna moja au nyingine ili kukidhi matakwa yao ya kuiba kura. Hivi ndivyo ilivyotokea katika uchaguzi wa wiki iliyopita Kenya na uchaguzi wa Tanzania katika miaka ya 1995 na 2000 hasa kule visiwani.
 
Hapa hakuna AU, EU wala UN, kura zitaibiwa kila siku katika chaguzi za Africa, coz wakubwa wanawania kutawala na sio kuongoza, kama wanawania kuongoza tusingeona wagombea kumi na zaidi kwenye kiti cha Rais, coz kuongoza kugumu.
Kwa maoni yangu kama ingelitokea huyo Mwenyekiti wa tume inayothibitika kuiba kura kwa ajili ya mtu fulani (mfano Kenya), vijana wakamwondoa kwenye ramani ya dunia, tusingesikia tena wizi wa kura maisha. Maana kila mtu angeogopa hapo na ambae atakubali kukaa post hiyo naamini atakayeshinda basi ndiye atakaempa.
Kwa mfano Zanzibar, mara zote Uchaguzi bomu, Wenyeviti wanne wa tume ya Uchaguzi wamepita (bab Zubeir, Maalim Machungwa, Abdulrahman Jumbe na sasa Masauni), wote hawa wamevuruga Uchaguzi na woote wanapita kwa miguu mitaani hata khabari hawana, watu wanawaangalia tu yaani kama hakuna baya lolote wamefanya, na hata wakitoka hapo Tume baada ya walizopata (takrima) na fupa jengine wanapata, wanapewa nafasi Serikalini hazina kichwa wala miguu just wavute time tu.
Sasa hapo wajameni wizi utakwisha? si wanajua mtasema siku mbili then muafaka yeye anatafuna kuku, anakuja mwengine yaleyale, anachukua chake mapema.
Hapo Zenji akitiwa adabu Mwenyekiti mmoja wa Tume, itakuwa ndio mwanzo na mwisho wa MUAFAKA. Na naamini nchi nyengine za Kiafrica watakuja kujifunza Demokrasia kwetu sisi.
Nasisitiza maoni _SiDe_
 
Njia Ya Kuondoa Wizi Wa Kura Ni Moja Tu, Muda Wa Uchaguzi Ukifika Raisi Anayemaliza Muda Ake Pembeni Nchi Iongozwe Na Jaji Mkuu Kama Rais Wa Muda Hadi Hapo Uchaguzi Utapokwisha Na Rais Aliyechaguliwa Kwa Kura Kutangazwa Na Malalamiko Yote (kama Yapo) Yawe Yameshatolewa Na Kupatiwa Ufumbuzi.
 
Hawa viongozi waliopigania kile wanachoita uhuru ni problem katika demokrasia maana wao wanaamini ni wao wanaoweza kutawala. Sasa hii itaendelea kuwa problem hadi watakoishia wote. Tatizo linakuja pale ambapo inaonekana wanawarithisha watoto wao vyeo pamoja na tabia zao zote mbovu za kifisadi. Hili ndio litasababisha sisi waafrika tuendelee kukunjiani ngumu na kukimbilia misituni.

Kama walivyosema wengine, hizo strategies alizotoa Kichuguu ni nzuri sana kama hawa jamaa wangekuwa wanaiba tu kura, haya majamaa yakiona yamekwama kuiba yananyang'anya kabisa kwa nguvu kwa kutumia majeshi kama walivyofanya kule Zanzibar 1995, 2000 na 2005 na kama walivyomnyang'anya ubunge Lwakatare pale Bukoba 2005. Kwa hiyo tunaongelea watu ambao hawana ustaarabu wa kawaida unaotarajiwa kwa binadamu wa karne hii. Labda Kikwete anaweza akabadilika, lakini sidhani kwa sababu hata yeye alikuwa anachekelea ushindi wa 80% wakati akijua kabisa kuna makura mengine alibambikizwa!
 
Hakuna demokrasia kwa watu kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku, 90% hawana taaluma yeyote, 98% hawako kwenye formal sector.

niliwahi sikia mtu mmoja alienda kwenye kituo cha kura akitafuta vibarua wa kulima shamba kwa posho ya 10,000/= watu wote waliacha kupiga kura na kwenda kupalilia mihogo! mwingine alienda kwenye mkutano wa mwenzie na 20lts za gongo na kiroba cha chumvi ule mkutano ulivunjika akina mama waliwahi mgao wa chumvi na wazee wakabaki wakiburudika kinywaji!

Muulize mheshimiwa shubiri ya Geita kisa aliyejenga choo stend kakosa ubunge!

Intelahamwe, Kony, Nkunda na Raila kuingia ikulu kwa kuchoma walokole sio sawa. EAG eldoret na kibaki hakuna relation yeyote. wanaoleta vurugu kenya sidhani kama kura walipiga kwani ni watoto na vijana.

Sasa tufanyeje?
Tuondoe ujinga kwanza kwa kuhakikisha watoto wetu wanaenda shule, watz tuache biashara za hiace na lodge bubu tujenge shule na vyuo, mch.getrude katuonyesha mfano hata mungu kambariki ubunge umemfuata nyumbani.
 
kifungu cha uchaguzi wa raisi kiingie katika katiba ya nchi

na isomeke hivi:
ni uhaini kushiriki kumpa/kumuondolea mgombea wa kiti cha uraisi kura isiyo/iliyo halali yake---then baada ya hapo sheria itatafsiri hilo kosa libebe adhabu gani.

matokeo ya raisi yahojiwe mahakamani.
 
This looks like a great topic for a serious discussion. Should be a lot of interesting points of view. Thanks for starting it.
 
Back
Top Bottom