Vikwazo vya Kikatiba katika kuleta Maendeleo na Demokrasia

kuomba wakoloni waliooondoka nchi zetu zamani kuwa wanakuja kutusaidia kuangalia uchaguzi na wao ndio wauamue

Ila duuu nao wanajua kuchagua viongozi wa nchi zetu kwa upendeleo fulani wakimpenda kiongozi wanaurahi akikaa wakikuchukia wanafurahi akiondoka

Kwa kenya Kibaki anangang'ania uongozi anaogopa kupelekwa kortini kwa wizi na uongozi mbaya

Tanzania mmmmhhhhhh, Kikwete nae sijui anafanya nini

Hivi bado anasafiri kila wakati kwenda holiday ulaya?
 
Namsubiri Greenland!!!!!
 
Waheshimiwa,

Mimi naamini hatuwezi kuondoa wizi wa kura, lakini jitihada zinaweza kufanyika, angalau kuupunguza wizi huo.

Kilio changu cha kwanza kabisa ni KATIBA. Inanisikitisha kusema kuwa mimi nilikuwa mwanachama wa TANU, sijakuwa na wala sitakuwa mwanachama wa CCM. Nilipokuwa mwanachama wa TANU, niliamini kuwa chama cha TANU kilikuwa chama cha Wakulima na Wafanyakazi na sasa naamini kuwa CCM ni chama cha Matajiri na Wajanja.

TANU, ilifanya kazi nzuri sana ya kuweka na kuitekeleza mikakati ya kumuondoa Mkoloni, kwa madhumuni ya kumpatia mkulima na mfanyakazi (wananchi) uhuru wa kujitawala wenyewe.

Lakini, baada ya kushika madaraka TANU badala ya kuwapa wananchi HATAMU za nchi, zikachukuliwa na TANU yenyewe. Tanu si wananchi, TANU ni kikundi cha wananchi kilichoshirikiana na wananchi wengine katika harakati za kupata uhuru. Sasa badala ya wananchi kujitawala, TANU ikaziba nafasi iliyoachwa wazi na Wakoloni. TANU ikaanza kutawala.

Kwa kuwa KATIBA ya kwanza iliyotengenezwa Lancaster House, London, haikuwapa TANU nafasi ya kutawala, kitu cha kwanza TANU ilichofanya ni kuibadili kuwa KATIBA ya Jamhuri ya TANGANYIKA. Hapo ndipo TANU ilipopata nafasi ya kuweka vyama vyote vya wafanyakazi chini ya mwavuli wa TANU, Kisha ikavipiga marufuku vyama vyote vingine vya kisiasa. Ikaunda tena KATIBA na kuchukua HATAMU. Hapo sasa hata migomo ikawa haramu. Hapo ndipo ukawa UTAMU wote TANU.

Kwa bahati mbaya au nzuri ukapatikana huu muungano, ikabidi sasa iingie AFRO-SHIRAZ. Hii AFRO-SHIRAZ na Mzee Karume Snr.,
kidogo walikuwa wanaleta leta kinaa.Ikabidi itafutiwe mbinu ya kudhibitiwa. Hapo ndipo ikazinduliwa hii CCM. Nafikiri ingekuwa bora kama ile nyundo na lile jembe katika nembo ya bebendera ya CCM ingeondolewa ikawekwa nembo ya TWIN TOWERS.

Kisa hiki nilichokihadithia kwa muhtasari tu ndicho kinachonifanya niweke kilio changu katika KATIBA hii tuliyonayo hivi leo. KATIBA hii ndiyo inayotoa mianya ya wizi wa kura.

KATIBA haina "checks and balances" baina ya Executive Branch, Judiciary na Legislature.

Kila kitu kiko chini ya CCM na Viongozi wake and especially Rais. Na Rais ni Mwenyekiti wa CCM. Hupati nafasi ya kumkamata mwizi wa kura wala kuthibitisha wizi wenyewe.

Tangu mawakala vituoni, wahesabu kura, watunza daftari za wapiga kura, sijui mashekha, returning officers, polisi, na wengine wote mpaka National Electral Commission. Wote wako pale kwa ajili ya CCM na serikali yake. Iwe kwa ridhaa yao au kwa kuogopa kumwaga unga au kwaa kujikomba komba. Wizi wa kura utaondokaje?

KATIBA, KATIBA, KATIBA hapo ndio penye KICHAKA. Si unaona? Ukiitaja tu wenye nchi yao wanakwambia, KATU, hilo halitafanyika. Kwa nini? UTAJAZA MWENYEWE.
 
Imeanza Kenya, sasa Irani, vijana wanakataa kuburuzwa na wazee wanasema haiwezekani. Tanzania tunasema tuna amani wacha liende, umasikini unakomaa wachahce wanakula nchi.

Je demokrasia gani tunayo Tanzania ya kuiba kura na kununua shahada? na hili linaonekana ni jema hakuna anayeshitakiwa wala kuonekana mhalifu. Makampuni yanayoiba fedha za walipa kodi yanalindwa kwa kisingizio ni makampuni ya jeshi ila yana ubia na wafanyabiashara wa nje, wananchi wakiuliza wanaambiwa wakae kimya.

Ni demokrasia gani na nchi gani tunaijenga, je siku matumizi ya usalama wa taifa au polisi yakishindikana itakuwaje? kwani kuna siku usalama wa taifa na polisi watakuwa ni watoto wa walioteswa na watakataa kuendelea kuwafanyizia ndugu zao ubaya! patakalika.

Viongozi mlioko madarakani mnaotetea udhalimu someni ishara za nyakati, Ayatolla haikutegemea kupingwa kwenye kauli zake na wananchi wake leo mnaona yanayotokea Irani. Kenya hawakutegemea kutoana macho, wala Zimbwabwe haikuzaliwa vile. Ila Tanzania inaweza kuja kuwa mbaya sana, kwani itakuwa ni kitu isiyotegemewa mpya kwa kila mmoja itakuwa mbaya sana.

Uchungu wananchi walionao uliojificha kwenye mioyo yao unahitaji msukomo mdogo sana kuuwasha, na huo msukumu ninyi viongozi wenyewe ndio mtauleta halafu mtaanza kutafuta wachawi hapo ndio moto utakapopamba moto.

komesheni wizi wa kura, CCM acheni kununua shahada za wapiga kura huu ni wizi mkubwa wa demokrasia. Waambieni wezi walioiba warudishe fedha zetu na muwafikishe mbele ya sheria bila kujali sura zao na ukaribu wenu nao.Kumbukeni mtoto aliyezaliwa mwaka 1990 ana miaka karibu ishirini hajui chama kimoja ni nini.

CCM kumbukeni kundi la matajiri mnalolijenga kwa wizi wa fedha za kodi zetu ni dogo mno kuweza kuwalinda milele, ni dogo kuliko lile la wa Irani lenye utajiri mkubwa wa mafuta. Mnatusulubisha msalabani halafu hamtuui kabisa mnatuacha na majeraha makubwa mwilini na moyoni halafu mnafikiri tunasahau mazila. Mnatunyima huduma bora za afya, mnatupa elimu mbovu na miundo mbinu mibovu halafu mnatuhubiria Amani, Amani ili muweze kula fedha zetu kwa raha na kutuona watumwa.
Kumbukeni hasira ya mwenye njaa ni mbaya sana, kwani mwenye njaa huwa hana cha kupoteza alisha kufa anangoja kuzikwa.

Siombei Tanzania yangu ifike huko bali naomba enyi viongozi vipofu wabadhirifu mlione hilo. Mlione hilo kwa ajili ya uzee wenu kuwa mzuri, watoto na wajukuu wenu kuwa na amani la sivyo mtalia mkiwa hamwezi kukimbia kwani hamtoamini yanayotokea.
YANAYOTOKEA IRANI, KENYA, ZIMBWABWE NA Kwingeneko kwa kukosa haki ya demokrasia ya kweli yatatokea Tanzania kwa upofu wa viongozi wetu.
 
baada ya faulo zote hizi sasa nadhani Chadema na CUF na vyam vingine vimsikie Mwanakijiji nami naongezea leo .Vyama hivi havishindwi kwamba havipendwi bali vinashindwa na mtu mmoja .Yule jamaa wa Tume mwenye nguvu sana kwamba akitangaza yeye mengine ni mahakamani lakini yeye kamaliza .Uteuzi wa watu hawa unafanywa na CCM na waafrika na hasa watanzania bado hawajiamini wakiwa madarakani.Wamesoma lakini kila kazi na madaraka wakiwa nayo inakuwa feva tu na si matokeo ya kisomo chao .

Chadema na wengine okeni hii nchi kutokana na janga baya mbeleni.Kuna hatari ya watu kuja kuuana kwa njia hii kisa Tume inaamua na hakuna wa kupinga labda mwende mahakamani ambako nako ma Judge wanasikia wakubwa wa CCM wanasemaje na hasa Mwenyemiti wa CCM ambaye ndiye Rais anayewpa ulaji huo .

Kuna haja kubwa wa kupinga Tume hii kuwepo na baadhi ya vipengele vya vya katiba kandamizi .Hili liwe jambo kuu kwa muda huu japokuwa najua kuna vyama kama TLP hawawezi kukubali wito huu.Chadema sasa ni Chama kikubwa mnakubalika kila kona ya Nchi uharamia mnao fanyiwa kila mmoja anauona kateni kutumika na CCM kuwatumia nyie kuonyesha Dunia kwamba kuna demokrasi Tanzania .Daini Tume ya Uchaguzi ya wote na si ya CCM na vinginevyo kataeni kushiriki Serikali za Mitaa mwakani.

Tumekuwa na urafiki wa karibu sana na Iran na sasa ndiyo kweli tuna practice yale ya Iran .
 
Lunyungu,

Tanzania ni nchi ya "demokrasia" na "amani" na "utulivu". Chaguzi hizi ndizo zinamwezesha mkuu wa nchi (Vasco Da Gama) asafiri kwenda nchi za nje kwa mabilioni ya pesa za walalahoi wakitanzania.

Hata kama Chadema wakigomea uchaguzi, kitu ambacho inabidi kifanyike, bado serikali itatumia pesa zake (kama za EPA) kushawishi vyama vidogo vidogo kama kile kipya kitakachoundwa kesho - TASAMUNDA - kushiriki huo uchaguzi.

Serikali ya kifisadi itatumia kila aina ya ufisadi kukaa madarakani kifisadi ili kuzidi kufanya ufisadi.
 
baada ya faulo zote hizi sasa nadhani Chadema na CUF na vyam vingine vimsikie Mwanakijiji nami naongezea leo .Vyama hivi havishindwi kwamba havipendwi bali vinashindwa na mtu mmoja .Yule jamaa wa Tume mwenye nguvu sana kwamba akitangaza yeye mengine ni mahakamani lakini yeye kamaliza .Uteuzi wa watu hawa unafanywa na CCM na waafrika na hasa watanzania bado hawajiamini wakiwa madarakani.Wamesoma lakini kila kazi na madaraka wakiwa nayo inakuwa feva tu na si matokeo ya kisomo chao .

Chadema na wengine okeni hii nchi kutokana na janga baya mbeleni.Kuna hatari ya watu kuja kuuana kwa njia hii kisa Tume inaamua na hakuna wa kupinga labda mwende mahakamani ambako nako ma Judge wanasikia wakubwa wa CCM wanasemaje na hasa Mwenyemiti wa CCM ambaye ndiye Rais anayewpa ulaji huo .

Kuna haja kubwa wa kupinga Tume hii kuwepo na baadhi ya vipengele vya vya katiba kandamizi .Hili liwe jambo kuu kwa muda huu japokuwa najua kuna vyama kama TLP hawawezi kukubali wito huu.Chadema sasa ni Chama kikubwa mnakubalika kila kona ya Nchi uharamia mnao fanyiwa kila mmoja anauona kateni kutumika na CCM kuwatumia nyie kuonyesha Dunia kwamba kuna demokrasi Tanzania .Daini Tume ya Uchaguzi ya wote na si ya CCM na vinginevyo kataeni kushiriki Serikali za Mitaa mwakani.

Tumekuwa na urafiki wa karibu sana na Iran na sasa ndiyo kweli tuna practice yale ya Iran .

Mkuu Lunyungu,
Inaeleweka kabisa mtu anapokutana na jambo la kumsikitisha basi kupata uchungu na kihoro ni jambo la kawaida. Mimi nadhani kama CHADEMA wangesikiliza na KUYAFANYIA kazi maoni ya watu mbalimbali kama ya Mkjj basi ni wazi kuwa leo usingekuwa na kihoro hiki.
Pili, huo wito unao waagiza / kuviagiza vyama vikae pamoja nadhani ni wazo zuri kwani keo hii CHADEMA inaonekana kukubali kupata fundisho la kwenda kwenye uchaguzi huku ikikacha kushirikana na vyama vingine vya upinzani. Ni vema CHADEMA itumie nafasi yake iliyonayo kujenga umoja wa kweli na vyama vingine kama kweli wanataka kuleta mabadiliko ya kweli.
 
Kuna nyakati Chadema , NCCR , CUF walipata wakati mgumu sana lakini hadi sasa wanao wafuasi .Niwakati sasa wa wana siasa wetu kufanya maamuzi magumu kama yale ambayo hufanywa na CCM kama kuchukua ushindi kwa nguvu .Nina waunga mkono kususia Uchaguzi na kutembea kwa kila Balozi na kumweleza kiundani kinacho endelea ili kabla ya mwakani katiba iwe na marekisbho ya Uchaguzi na pia kuwe na Tume huru ya Uchaguzi.Kama kweli nia yetu ni kufanya mabadiliko naku balance Bunge na kuiendeleza Tanzania sasa Lipumba , Mbowe , Mrema kaeni meza moja mtafute dawa ya hili .Kuna watao shiriki kisa wanakula EPA sawa lakini wana nguvu gani ama itakuwa tu kwamba wameshiriki ? ma giants go in action sasa okoa roho za watanzania wanao kata tamaa ya kupiga kura kisa kuibiwa kura warudi kwa moyo mkunjufu na kushiriki zoezi hili .
 
Labda kama kutazaliwa vyama vipya, lakini kwa hivi vilivyopo, vitashiriki, vitalalamikia faulo, na uchaguzi utakuwa umepita, hakuna jipya...2010 hivyo hivyo!

mabadiliko yanayotakiwa ni zaidi ya kugomea hizo chaguzi..hiyo ni njia moja lakini nadhani tuna kazi kubwa zaidi!
 
Naunga hoja!

Kwa tume hii ya Jaji Makame chini ya kuwajibika moja kwa moja kwa Rais aliyemteua ni ndoto kwa wapinzani kushinda maana kama tulivyoona Biharamulo ni uamuzi wa Jaji Makame na Rajabu Kiravu tu ndiyo wa mwisho nani awe mbunge na wala sio nani kapata kura nyingi!Makame na wenzake kwa utashi wao wana nguvu hata za kusema "wewe umeshinda lkn sikutangazi kuwa mbunge",wana nguvu kubwa mno!

Kama tu tunavyosema msemo wetu kule nyumbani Kyela "Kuitola CCM tukabhagila mwee,kuisosya kajamba amele rugiri"(Kuitoa CCM kwa tume hii hatuwezi labda kobe waanze kuzaliwa wakiwa na nundu)
 
Its true...!!!
Hakuna maana ya kushiriki kwenye uchaguzi huku tume ikiwa ni ya kifisadi..!!
CCM ni wezi wakubwa....!!!maendeleo hatuyaoni watanzania,Mafisadi ndani yaCCM wananufaika wao na familia zao...!!
Kwa upande mwingine watanzania tumezidi upumbavu,we chama kimekaa madalakani miaka 48 maendeleo hakuna then mtu anapoteza muda kupangi mstari,wino wa peni kuipa kura CCM hii ni hatari..!!
Naungana mkono na ndugu yangu Mwigamba kuwa siku nikiipigia kura CCM mungu aniangamize na kibanda changu cha kura.....!!!
Hivi wananchi hawajiulizi kuwa miaka 48 ya uhuru bado tupo palepale,hawa CCM wanaitaji miaka mingapi zaidi ilia kuleta maendeleo hapa nchini....?
Wananchi tuamke.....!!!
Kama wananchi tutaendelea hivi naomba CCM watukamue zaidi UKALI WA MAISHA UZIDI,VITU VIWE BEI JUU,NAULI JUU,KODI YA MAENDELEO irudi mpaka watanzania tushike ADABU....!!!
Anyway....!!!kwa sasa tuishie hapa.....!!!
 
Kule znz kwanza walianza kupigwa mapanga watu weupe,watu weusi wakaelewa wanaopigwa ni weupe tu,wao ndo wenye nchi,eh! wakaanza kupigwa watu weusi,tanganyika wakaelewa wanaopigwa ni waznz tu kwani ndo wenye vurugu,oh! mara wakaanza kupigwa tunduru,eh! mara mbeya wahaya,mara wasukuma kule busanda,

Duh! kazi kweli kweli,kumbe mwanzo watu walikuwa hawajui kuwa utapigwa ikiwa utaikataa ccm tu,lkn sio kwa rangi,kabila,dini wala cheo chochote,muhimu ikiwa wewe umeikataa ccm basi mapanga yatakukuta tu..

Hiyo ndio ccm na wameapa na hata kuthubutu kuongea hadharani kuwa serikali haitoki kwa kipande cha karatasi,duh! sasa sijui niseme Chadema wamepoteza mwelekeo au vipi,maana Cuf wakisema wameibiwa waliambiwa wamepoteza mwelekeo, kwa nini chadema wasiwaachie TLP kule Biharamulo kwa kuwa TLP ndio inakubalika kule,Y? wakakusanya nguvu pamoja kuiondoa ccm. doooooh! hii ndio Tz, Chadema waliwaambia Cuf upepo umebadilika,kweli upepo umebadilika kwa hali hii?

Ikiwa hatujakaa pamoja waTz wote,tukaunganisha nguvu zetu unafkiri tutaishinda ccm,abadan.. tutabaki kulalamika siku zote tumeibiwa.. lazima tuwe kitu kimoja na tena basi sio turidhike na kura tunazopiga bali tuhakikishe kila kura yake anailinda kwa njia yoyote...
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI DHAIFU
progress.gif
 
Hadi lini tukubali chaguzi zinazosimamiwa na makada wa CCM?

Chini ya Sheria ya Uchaguzi wakurugenzi wa halmashauri – za Wilaya na zile za Miji – ndiyo huwa wasimamizi wa chaguzi (yaani Returning Officers) katika majimbo yaliyo katika sehemu zao.

Inavyoeleweka ni kwamba wakurugenzi wa halmashauri ni watumishi wa serikali, chini ya Wizara ya Serikali za Mitaa (TAMISSEM) hivyo huteuliwa na serikali ya chama cha tawala.

Katika wakurugenzi hawa ambao idadi yao ni zaidi 150 hapa nchini, sidhani kama kuna yeyote yule ambaye ni mwanachama/mfuasi wa vyama vingine vya siasa na serikali ya CCM huwa makini sana katika uteuzi wao – na bila shaka huwa inazingatia sana masuala ya chaguzi. Yumkini hawa ni ‘makada’ wa CCM wanaofanya kazi za u-returning officer kwa niaba ya chama chao, chini ya uelekezi wa mabosi wao, ma-DC.

Umuhimu wa watu hawa katika chaguzi ni kwamba wakishamtangaza mshindi, huwa ni basi, hata aliyeshindwa akikataa kutia saini hati ya matokeo. Sana sana baadaye aende mahakamani kufungua kesi kupinga matokeo.

Kumetokea matukio kama 3 yanayothibitisha ninayosema:

1. Wakati wa uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Temeke mwaka 1996 ambapo Mrema alitangaza kugombea, kulitokea jitihada za kimakusudi za kutaka kumhamisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke, Bi Elizabeth Nyambibo kwenda halmashauri nyingine. Hii ilikuwa ni wakati Mzee Kingunge akiongioza wizara ya TAMISSEMI. Uhamisho ulilalamikiwa sana na vyama vya siasa ikiwemo NCCR-Mageuzi wakati huo ni moto kwa CCM – lakini hatimaye uhamisho haukufanyika. CCM walikuwa na wasiwasi na Nyambibo kama Returning Officer wa uchaguzi mdogo wa Temeke. Hata hivyo Mrema alishinda.

2. Katika uchaguzi Mkuu wa 2005 Mkurugenzi wa manispaa ya Tanga Elizabeth Munuo alitimuliwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Returning Officer wa jimbo hilo baada ya kugundulika kuwa alikuwa amemdhamini (kimaandishi) mgombea wa CCM – Bakari Mwapachu. Ukereketwa wa huyo mama uligundulika tu kwa sababu alikwa ameuweka kimaandishi. Swali: Kuna wakurugenzi wa halmashauri (ma-returning officer) wangapi kati ya zaidi ya 150 tulio nao ambao kimya kimya ni wakereketwa wa CCM?

3. Katika uchaguzi huo huo wa mwaka 2005 katika jimbo la Bukoba mjini, Returning Officer Faustin Fisso aliamua kumtangaza mgombea wa CCM, Hamisi Kagasheki kuwa mshindi baada ya “kumshinda” yule wa CUF, Wilfred Lwakatare kwa idadi ya kura chache mno. Lwakatare alikuwa amempigia simu Fisso kumuomba asubiri asitangaze matokeo kwanza hadi wafanye majumuisho upya. Ingawa Fisso alimkubalia, lakini wakati anafika kituoni, alikuta Fisso kisha mtangaza Kagasheki kuwa diyo “mshindi.” Wengi walisema endapo ingekuwa kinyume chake, yaani mgombea wa CCM ndiye angekuwa amewomba Fisso asubiri baada ya kuona uchache wa ushindi wa wa mpinzani wake bila shaka angekubali mara moja kusubiri.

Nimeiweka thread hii ijadiliwe na wana-JF kutokana na yaliyojiri katika uchaguzi wa Biharamulo na jinsi matokeo yalivyotangazwa kumpa mgombea wa CCM ushindi. Msimamizi wa Uchaguzi – Zuberi Mbyana alikataa wito wa upande wa mgombea wa Chadema kufanya majumuisho upya hususan katika vituo 9 kutoka kata tofauti, vituo ambavyo vilionyesha utata katika majumuisho yake. Wengi wanasema iwapo matokeo yangekuwa ni kinyume cha yalivyokuwa, Zuberi Mbyana, ambaye anaelezwa kuwa mkereketwa mkubwa wa CCM, angekubali kufanyika kwa majumuisho mapaya kama yalivyoombwa.
 
Nakubaliana na wewe – tuko katika shit katika masuala ya uchaguzi. Hawa wakurugenzi wa halmashauri ndiyo wenye ku-control utafunaji wa hela za walipa kodi katika halmashari zao. Wanajijua wako katika "asali" na vile vile muajiri wao – serikali ya CCM – inajua hivyo. Hivyo wanajua ni lazima wafuate amri na maagizo kutoka CCM ama sivyo watang'olewa kutoka nyadhifa zao. Nani atakubali atolewe mnofu kinywani?
 
Hili ni lazima lifanyike vingenevyo, ccm wataendeleza utawala wao usiomjali mtanzania.

Sasa kazi iliyobaki ni moja tu, kulia na katiba inayojali mfumo wa vyama vingi. Haki inatakiwa kuonekana ikitendeka na sio tu kusikika kuwa ipo
 
Tume ya uchaguzi ni tatizo. Lakini si kubwa kwa magnitude inayohofiwa hapa.

Tatizo la msingi ni ujinga kwanza, na njaa ya mpiga kura. CCM wanacheza na mtaji huo. Mnadhani wanaochagua CCM kwenye uchaguzi, wanaelewa wanachokitafuta?
 
It is so really nust man,Nakubaliana na wewe mzee wangu kuwa kuna haja ya vyama vya siasa kugoma kwenda kwenye uchaguzi kwa tume kama hizi na pia kuna haja ya kuunda tume huru ya uchaguzi!! tumeona tatizo sio watu kwa sasa tatizo ni Tume ya uchaguzi chini ya CCM
 
Back
Top Bottom