Vikwazo vya Imani na Dini kuhusu kampeni ya uzazi wa Mpango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vikwazo vya Imani na Dini kuhusu kampeni ya uzazi wa Mpango

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 2, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  VIONGOZI wa dini ya kiislamu wakiwemo mashehe na maimamu wamepinga kampeni ya Taifa dhidi ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango nchini. Hayo yalijulikana jana katika semina iliyowashirikisha viongozi hao wa dini iliyowataka watambue juu ya matumizi ya njia hizo Mkoani Kilimanjaro.

  Kampeni hiyo ya Taifa ambayo ipo kwenye michakato ya kuwakutanisha viongozi wa dini mbalimbali nchini ili wapewe elimu ya njia hizo na wao wakawafikishie wananchi na kuwapa hamasa juu ya matumizi ya njia hizo.

  Viongozi hao walipinga vikali juu ya kampeni hiyo na kusema kuwa hawatahamasisha jamii kwa kuwa njia hizo zinakwenda kinyume na maandiko ya dini hiyo.

  Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya mashehe na viongozi wengine wa dini hiyo ya kiislamu wakiwemo na walimu wanawake wamesema kuwa kutokana na maandiko ya dini ya kiislamu kampeni hiyo ambayo wamepatiwa elimu wao hawataitekeleza kwa kuwa ni kinyume na maandiko ya dini.

  Wamesema kuwa njia hizo kwanza ni kama ni kumkufuru mwenyezi mungu kwa kuwa yeye hakusema binadamu wazuie uzazi na kusema aliwataka wanadamu waje kuujaza ulimwengu na sio kuzuia kizazi.

  Wamesema kuwa kampeni hiyo wanaipinga vikali na hawatawaambia waumini wao watumie njia hizo wao watawaelimsha waumini wao kulingana na maandiko yanavyosema.

  Afisa Mipango zoezi la Mpango wa Uzazi wa Mpango Taifa, Bw. Safiel amesema kuwa, wanawakutanisha viongozi wa dini hao na wameonekana kama kutofahamu lengo la Taifa, na dhumuni la kuwakutanisha ni kutaka watambue njia hizo na waelimishe jamii juu ya njia hizo zinazoonekana wananchi walio wengi hawazitambui.

  Na kusema kuwa sio kwamba wanawazuia wananchi wasizae bali kwa kudhibiti wimbi la watoto ambao hawapati huduma stahili kutoka kwa wazazi wao na vilevile kuelimisha jamii kuzaa kulingana na uwezo walio nao.


  Chanzo:
  Nifahamishe

   
 2. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hivi unategemea nini kutoka kwa Mashehe ambao wanaongoza kwa kuoa wanawake. Kama unawake wanne, uzazi wa mpango unafaida gani?

  Inatia aibu sana kuona kuwa viongozi wa dini wapo mstari wa mbele katika kupinga na kurudisha/zorootesha maisha ya jamii.

   
 3. I

  Ibnally Member

  #3
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo lenu nyie mnaojiita watumishi wa Mungu mnang'ang'ani uzazi wa mpango kwa kuwa wengi wenu mnaongoza kuwa na vimada nje ya ndoa zenu, sasa manona kama msiposapoti uzazi wa mpango utatumia kigezo gani kumshawishi kimada wako ili asikuletee mtoto na mkeo wa ndoa nyumbani akaja juu? Au mnafikiri hatujui mambo yenu.
  lakini kama hujaelewa wanachopinga Masheikh ni njia zinaotumika kuzuia mimba hazikubaliki na sheria ya dini, lakini zaidi kampeni hizi zinachochea zinaa kwa kasi kubwa. kama hamfanyi uchunguzi vizuri, watumiaji wa njia hizi, wengi wao ni wasichana wa mashuleni na wanawake wasioolewa ambao ni vimada wenu.
   
 4. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Sidhani ya kwamba tatizo ni dini yenyewe mbali ni utamaduni pamoja na dini. Waislamu katika nchi nyingi hukubali njia nyingi za uzazi wa mpango. Wakikataa katika nchi fulani ni ya kwamba wanaamini utamaduni wao ni sawa na dini kwa sababu hawakuzoea kuangalia tofauti hizi.
  Max: swali la wake wengi wa shehe si jambo kuu. Kila mtu anapaswa kugharamia watoto wake (asipotoroka!); akipaswa kulisha watoto 10 basi ni watoto 10 kama anawazaa na mke mmoja (au kama mama amekuwa mdhaifu baada ya kuzaa mara nyingi ameaga dunia basi anaoa tena) au kama anazaa na wake wengi.

  Watoto wengi ni ishara ya umaskini; katika mazingira ya mjini na penye maendeleo idadi inazidi kupungua - hivyo ndivyo kote duniani.

  Kinachoweza kusaidia ni jitihada ya maafisa wa miradi ya uzazi wa mpango kuonyesha heshima kwa kila dini na pia kujielimisha kwanza. Nadhani Uganda na nchi mbalimbali utapata wataalamu Waislamu wanaoweza kuonyesha kwa Qurani, ahadith na fiq ya kwamba kuna njia zinazokubaliwa.

  Mimi naona ya kwamba kwenye uwanja wa elimu ya kijinsia ni vema kuongea na viongozi wa dini lakini si njia bora kuwachukua wote mahali pamoja kwa sababu kila mmoja ana mapokeo yake; wangeongea nao mmoja-mmoja na kama wote ni wagumu basi kumchukua mtaalamu wa dini yao kutoka nje kwa semina.
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 5. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  NB:
  angalia maelezo yafuatayo kutoka tovuti za Kiislamu:

  Islamic View of Birth Control - IslamonLine.net - Ask The Scholar
  "Now coming to the issue of birth control, there is nothing in Islam that prohibits it so long as it is done consensually for valid reasons such as the following: putting off pregnancy until such time when the spouses are in a better position to shoulder the responsibilities of parenting, to allow for space between pregnancies in order to provide proper nurturing and care to existing children, et cetera.

  Birth control is, however, forbidden or undesirable when it is resorted to as a permanent measure to prevent conception altogether..."


  Family Planning and Islam: A Review
  (muslim-canada.org)

  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]"A Muslim has three sources of knowledge to obtain answers to the questions pertaining to various aspects of human life. These sources are:[/SIZE][/FONT] [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1. The Holy Qur'an;[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]2. Sayings (hadith) and acts (Sunnah) of the Holy Prophet (pbuh); and[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]3. The views of the leaders of juristic schools qualified to interpret the teachings of Islam.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]1. The Holy Qur'an[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]No Qur'anic text forbids prevention of conception. There are, however, some Qur'anic verses which prohibit infanticide and these are used by some Muslims to discourage birth control.[/SIZE][/FONT]
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]But contraception does not amount to killing a human being. These verses in fact were revealed to forbid the pre-Islamic Arab practice of killing or burying alive a newborn child (particularly a girl) on account of the parents' poverty or to refrain from having a female child. Perhaps in those days, people did not know safe methods of contraception and early abortion.[/SIZE][/FONT]"
  [FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1](inaendelea kuchungulia ahadith ikionyesha ya kwamba mtume Muhamad aliruhusu "[/SIZE][/FONT][FONT=Arial,Helvetica][SIZE=-1]'azl" = azili.)[/SIZE][/FONT]
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 6. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  NB II:
  hapa naongeza jibu la shehe wa madhhab ya Shafi'i (ambayo ni mwelekeo wa waislamu wengi wa Afrika ya Mashariki kati ya madhhab 4 za Wasunni) - anaruhusu njia mbalimbali kama azili, kondomu, na kidonge.

  Modern Birth Control (qa.sunnipath.com)
  (Question ID:3949 Date Published: July 03, 2005
  Modern Birth Control Answered by Shaykh Amjad Rasheed)

  Sijui ni swali la elimu ya mashehe wa Kilimanjaro au ni athira ya Wahhabi kutoka Saudia??
  Tazama pia "Encyclopedia of Women & Islamic Cultures: Family, body, sexuality and health
  by Suad Joseph, Afsaneh Najmabadi" ukurasa 213 angalia google books http://books.google.de/books?id=bzXzWgVajnQC&pg=PA212&lpg=PA212&dq=shafii+birth+control&source=bl&ots=AprVQqslDn&sig=l9sSduxtyOkhkZwpnMBmWNYxlpA&hl=de&ei=xBNOStSDG42j_AbfucXABQ&sa=X&oi=book_result&ct=result&resnum=8
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 7. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Msimamo wa mjinga mmoja usichukuliwe kuwa ndiyo msimamo wa dini husika. Ni makosa ku-generalise mambo.
   
 8. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Hili ndilo tatizo lenu wanyenyekevu mnapo kosa hoja katika mada. Mashehe unao wapigia debe, wapo mstari wa mbele kuongoza ufuksa na mashoga. Hivi hujuwi sababu ya kuwa na MAANTI MODI kila kona imetokana na tabia chafu ya kimasheke iliyo kuwa inafanywa misikitini mwenu?

  Dini pekee hapa duniani inayo ongoza kwa kupenda ngono, ni ya Uislam, ndio maana mtume wenu Marehemu Mwamadi akawapa ruhusa ya kuoa wake WANNE, lakini bado hamjaridhika, na kuendelza biashara ya ushoga na umaumba.

  Mnavisha wake wenu majoho kama maninja, lakini bado mnaongozwa na mafadhaiko wa akili na kuamua kurukia MAANTI MODI.
   
 9. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Tazizo, je, hao wenye wake wengi na watoto kibao, wanauwezo wa kuhudumia watoto wao? Sababu kuu iliyo sababisha kuanzisha uzazi wa mpango au kuwekea umuhimu katika jambo hilo la uzazi wa mpango, ni kuwa, Familia zenye watoto wengi zimeshindwa kuonyesha na/au kutoa ushaidi wa kuhudumia watoto wao, na kusababisha watoto kupata taabu sana ya maisha.

  Haina maana wala haileti mwelekeo kuwa na watoto kumi na kushindwa kuwaudumia kimaiasha. Mwisho wake, hao watoto wanakuwa wa mitaani na kuongozwa na dunia isiyo wajali zaidi ya kuwaangamiza. Ndio maana kuna umuhimu wa kufikiria zaidi ya mara mbili kuhusu uzazi wa mpango.
   
 10. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  MaxShimba, nina mawili:
  1) je unaweza kuonyesha takwimu halisi kama Waislamu wanazaa kuliko Wakristo? Sidhani takwimu hii ipo. Sikubali kama mtu anasema "Mimi najua Waislamu wenye watoto wengi...". Kwa sababu hata hapa mwingine atasema: Na mimi najua Wakristo wenye watoto wengi. Hoja kama hizi hazina thamani. Mtu akitaka kujua anaweza kulinganisha wilaya za vijijini penye Waislamu wengi na wilaya nyingine penye Waislamu wachache na kulinganisha idadi ya wakazi kufuatana na sensa mbili. Ukifanya kazi hii tunaweza kujadiliana. Watu maskini vijijini huzaa kuliko watu wa mjini; dini inaweza kuwa sababu ya ziada lakini hili ni swali la uchunguzi kamili.

  2. nashangaa sana unajitangaza kama "bondservant of Jesus Christ" lakini ukiongea habari za Waislamu lugha yako mara nyingi inajaa hasira na chuki. Jibu lako kwa Ibnally mimi naona aibu kuitwa Mkristo kama wewe unajitangaza hivyo na kufyatulia matusi mengi.
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Umeshindwa kueleza na au onyesha kimifano, kwanini uzazi wa mpango unapingwa na waislam, na kuamua kunirukia mimi na imani yangu. Hoja hapa, ni kwanini mashehe wanapinga uzazi wa mpango.

  I am a Bondservant wa Jesus Christ, that wont change till He comes. Kama kusema ukweli kumekuwa maumivu kwa wanyenyekevu, basi itabidi, waingalie imani yao yenye shaka kwa mtazamo mwingine. I am ready to be confronted, huwa sina tatizo na hilo, lakini ninapowaconfront waislam, huwa inakuwa personal kwao/kwenu. As a man, you must be ready for anything and everything.

  Weka ushaidi au maelezo yaliyoambatanishwa na uthibisho, yanayo saidia mapingo ya mashehe kuhusu uzazi wa mpango.

  I don't think at all, wanao pigia debe uzazi wa mpango hawana hoja, kuliko mashehe walioshindwa kusema ni kwanini uzazi wa mpango usiwepo.
   
 12. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kimsimgi naona ya kwamba tunakubaliana uzazi wa mpango ni jambo zuri!

  A) Huko juu nimetaja mifano kadhaa ya mashehe na walimu Waislamu wanaokubali mbinu mbalimbali za kupanga uzazi. Nimeeleza ya kwamba kuna tofauti kati ya Waislamu kimataifa (hata dhehebu la Shafii amabo ni wengi TZ) na wale mashehe wa Kilimanjaro waliotajwa hapo juu. Ninahisi ni mchanganyiko wa dini na utamaduni. - Je uliiona??

  B) Nimetoa hoja ya kwamba maafisa wanaoandaa majadiliano na viongozi wa kidini juu ya haya i) wanafanya kazi muhimu na ii) wanapaswa kujiandaa vizuri zaidi kwa majadiliano na kila dini kulingana na mapokeo mbalimbali.

  C) Jibu lako kuhusu matusi sijaelewa. :confused: Je kuwa mwanaume inamaanisha kusimama bila hofu ukirushiwa takataka au kurusha uchafu mwenyewe kwa nguvu?? Je Yesu unavyomwona angefanya nini??
   
 13. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  Jesus is God and full of wisdom.

  [​IMG]
   
  Last edited: Jul 3, 2009
 14. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Maana yake nini?
  Hupendi kuongea tena? ("it is finished")
  Unajisikia imesulubishwa?
  Yesu msalabani eti "aliwaconfront" waliomtesa kwa maneno jinsi ulivyoyatumia ukijadili habari za Waislamu?
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tena usilete hija ziso kuwa na mantiki! Mashehe na Babu zako ni nani wenye wake wengi?
   
 16. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Mashehe
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kamuulize Babu yako, kama huna kamuulize Chifu wako, kama huna kamuulize mtemi wako, kama huna, basi huna asili!
   
 18. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160

  You don't get it eeh.

  It is hard if not impossible for muhammadans to consent the truth. I think it is their culture if not colere.

  Where are the tangible and watertight exhibits given by the so called Shehes to support their defective argument? The Shehes are against birth control! In order for them to support what they are against, it is very imperative for shehes to annex verifiables and tangible exhibits as a case law, there is none so far, than blah blah zakawaida kutoka kwa Muhammadans. It is shame and sad.

  The only thing I have learned from Muhammadans ni kulalamika tuuuu bila ya ushaidi wowote, is this what you guys inharited from Marehemu Muhammad? Kuwa inferior? What is going on people? Why should some one be a muslem kama inferiority ndio inayo ongoza cult nzima ya muhammadans?!

  Give me something, WHY DO SHEHES THINK THAT BIRTH CONTROL IS UNETHICAL? Give me some koranic merits or authentic sahih hadith inayo SAIDIA KAMPENI YAO YA KUPINGA UZAZI wa mpango.
   
 19. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Wote wanasema ni mashehe.
   
 20. Kipala

  Kipala JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2009
  Joined: Jan 10, 2009
  Messages: 3,537
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Jamani turudi kwenye swali asilia. Kama Waislamu katika nchi nyingi wanaweza kukubali njia za kupanga uzazi wakitoa sababu za maandiko na mafundisho yao (tazama juu!)

  - je kwa nini mashehe wa Kilimanjaro (pia wengine wa Tanzania??) wanaamini ya kwamba haiwezekani??
   
Loading...