The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,451
- 17,155
Marekani imetangaza vikwazo vipya kwa kampuni ya Huawei zaidi ya vile ilivyotangaza mwezi MAy mwaka huu ambavyo vilizuia makampuni makubwa ya kutengeneza chipsets kama Samsung na TSMC kuiuzia Huawei.
Jana Jumatatu Marekani imetangaza vikwazo vipya kwa Huawei ambavyo vinazuia kampuni hata za chipsets za viwango hafifu kama Mediatek kuiuzia chipsets Huawei bila kibali cha Marekani.
Marekani imesema vikwazo hivi vinaenda mbali zaidi ya vile vya mwezi May ili kuhakikisha Huawei hapati vifaa vya kutengenezea simu zake wala mitambo yake ya mawasiliano ya 5G.
Huawei imetangaza kua simu ya Mate 40 ndio itakua simu ya mwisho yenye processor za hali ya juu kwa sababu haitapata tena material kwa sababu ya vikwazo vya Marekani.
Huawei ilikua inategemea kuendelea na simu za daraja la kati na la chini, entry level and med range phones ambazo ingepata vifaa kutoka Mediatek ili kutengeneza chipsets lakini Marekani amepiga pini hadi huko.
Mediatek ndio processor ambazo zinatumika kwenye simu za infinix, tecno na baadhi ya low end na mid range phones za makampuni mengine kama A10s ya Samsung.
New sanctions deal 'lethal blow' to Huawei. China decries US bullying