Vikundi vya Dini Senegali vyasema Rihanna asikanyage nchini humo

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
_99861518_rihanna.jpg


Mwanamuziki wa kimataifa Rihanna anategemewa kuhudhuria mkutano mkubwa nchini Senegal,lakini vikundi vya dini nchini humo wamekataa kumpokea, chombo ch habari cha Jeune Afrique kimeripoti.

"Tumeukataa ufreemason na mapenzi ya jinsia moja" , shirika la vikundi 30 vya kidini wamesema, wakimshutumu mwaimbaji huyo kwa kutumia ishara za mazo na kuwa mjumbe wa chimbuko la Illuminati , lilanoaminika kuwa ni kundi maalum la watu ambao hudhibit masuala na uongozi wa dunia na inasadikika kuwa hufanya shughuli zao kisiri kudhibiti kila kitu na kuunda Utawala Mpya wa Dunia.
hutuma hizo zimefutiliwa mbali na wasanii waliowahi kufanya nao kazi huko nyuma,

Rihanna atatembelea nchi hiyo ya Afrika Magharibi akiwa katika nyadhifa yake ya balozi wa shirika la elimu 'Global Partnership Foundation'

Shirika hilo linamaadhui wa kuchangisha fedha za kuwafundishia mamilioni ya watoto na vijana katika nchi zinazoendelea.

Chombo cha habari cha Jeune Afrique kimemnukuu Waziri wa Mambo ya Ndani akisema kuwa atahakikishia usalama washirika wote wa mkutano huo.


Chanzo: BBC Swahili
 
Waarabu weusi wanamambo sana, huko Middle East kwa wenye dini yao Rihanna anakwenda kama kawa, sema hawa wa Shithole country ndio maana wanaonekana mazuzu
 
Back
Top Bottom