Vikongwe wanane wafanyiwa ukatili, wawili wafariki

Jun 17, 2011
20
5
Baada ya mauaji ya kutisha kwa watu wenye ulemavu wa ngozi(Albino) yaliyoshika kazi zaidi katika kanda ya ziwa mwishoni mwa mwaka 2008sasa vitendo vya kikatili kama hivyo vimeamia kwa vikongwe Mkoani Kagera.

Takribani vikongwe wanane wanawake wamefanyiwa ukatili wa kinyama na wawili katiyao wamepoteza maisha kwa nyakati tofautitofauti vijiji tofautofauti vya vijijivya kata hiyo.

Vikongwe waliofanyiwa ukatili ni pamoja na Eufrazia Iluganyuma, Anamaria Develian,MarthaKilumushwoi, Salapia Thomas, Aulelia Mlabi, Adrofina Anacret na Mafurazia Felix na mwingine aliyejulikana kwa jina moja Paulina mkazi wa kijiji cha Itongo yeye alipotezamaisha baada ya kukutwa amekufa ndani ya nyumba yake huku akiwa amekatwa sehemuza siri.

Vitendo hivyo vya kikatili ni pamoja na ubakaji,kunyofolewasehemu za siri vyote hivyo vikihusishwa na imani za kishirikina vinavyofanywa na vijana wenye umri mdogo kwa wabibi wenye umri wa kuanzia miaka 70 na kuendelea.

Jamii imegubikwa na hofu ya mtandao unaoshukiwa kuhusika. Inasemekana mtandao huo una nguvusana na kuwa tishio kwa jamii nzima.


Ndugu jamaa lakini pia na waathrika wenyewe wa vitendo vyakikatili wanashikwa na kigugumizi kuelezea yanayowapata wakiofu wakisema wanawezakufanyiwa vibaya zaidi ya hayo wanayofanyiwa kutokana na rekodi za washukiwa kuhusishwa katika kesi za mauaji na utekaji lakini baada ya muda kuonekana katika jamii huku wakiendelea na matendo yao ya kikatili.
 
Back
Top Bottom