Vikombe vya tiba vinavyozuka huku na kule vinakuja kushusha imani ya watu kwa Mungu wa kweli!

binti ashura

Senior Member
Jan 14, 2011
118
19
Ndugu zangu katika jf mimi ninapenda kuwajurisha ya kwamba hizi ni nyakati za mwisho, tumezoea kusikia kuwa hizi ni nyakati za mwisho lakini hazikulinganishwa na hizi za sasa. mimi napenda kuwajurisha kuwa kuna njia moja tu ya kujihakikishia usalama wa hatima ya maisha yetu na usalama wetuni kujikabidhi kwa bwana yesu. tujisalimishe kwa yesu huko ndiko tutakapokuwa salama! vinginevyo ibirisi atayafanya maisha yetu kama viumbe wa kuchezea kama panya wa majaribio ya kisayansi. kwa wale wavuvi wanajua namna ya kuvua samaki kwa kutumia ndoana, hivyo ndivyo shetani avuavyo watu. anaweka chambo kidogo unaona kama unafaidi lakinindiyo unakamatwa mpaka mwisho hivyo.
yesu ni njia ya kwendea mbinguni ukimwamini ujue umechagua fungu lililojema!. wapendwa nawatakia kila kheri kwa mwenyezi Mungu.
 
Baambie baelewe papa, mutu ukiwa na Imani thabiti hautatetereka. Dawa ni moja tu kumrudia Mungu kumwamini na kutii amri zake 'kwa imani yote yanawezekana'. Mwenye sikio na asikie
 
Hizo Nyakati za mwisho ni kwa bongo tu! maana nchi nyingine hakuna hayo ya vikombe. Watanzania tumekata tamaa ya maisha kwani ni magumu na magonjwa yanatuzidi ndio maana akitokea mwingira tunakimbilia, akitokea lusekero tumejaa, akitokea babu ndio kabisaa. Maisha yakiboreka haya mambo nayo yatapungua.
 
Mimi nadhani kuna wanaosaidia kuimarisha imani. Babu anasema, unapokunywa dawa na kupona mtizame Mungu si mwanadamu! (maana yeke mwamini Mungu si binadamu). Babu anasema mimi si mganga wala sitibu, kinachotibu ni neno la Mungu lililowekwa kwenye mti huo (maana yake amini kuwa neno la Mungu ndilo uzima).
Je hapo si anawaimarisha watu katika kumwamini Mungu?
Angalieni na kusikiliza video zinazomhusu; msimhukumu kwa kitu ambacho hajafanya wala kusema.
 
Hizo Nyakati za mwisho ni kwa bongo tu! maana nchi nyingine hakuna hayo ya vikombe. ......, akitokea babu ndio kabisaa. Maisha yakiboreka haya mambo nayo yatapungua.
Nchi nyingine hawana kikombe cha babu lakini wanakifuata Loliondo kwa babu.
Huko maisha yalikoboreka kikombe hakipo lakini wanakifuta kwa babu;
Au unafikiri wanaokunywa kikombe cha bau ni waTZ tu? Video ya The loliondo wonder part 2 imeonyesha watu wanaoongea kifaransa wakinywa kikombe!
 
Kwa
sababu, ukimkiri Yesu
kwa kinywa chako ya kuwa ni
Bwana, na kuamini moyoni
mwako ya kuwa Mungu
...alimfufua katika wafu,
utaokoka. Kwa kuwa, kila
atakayeliitia Jina la Bwana
ataokoka. Warumi 10:9,
13.
 
Back
Top Bottom