Vikao vya NEC na Baraza Kuu CDM kujadili hali tete ya nchi!

nimeona kwenye mapitio ya magazeti jambo leo linadai BWM litavunjwa kesho. kama ni kweli mkutano wa Jmosi utapitwa na wakati.

Hata kama litavunjwa kesho bado ni matokeo ya shinikizo la umma.
Ni mafanikio.
 
nimeona kwenye mapitio ya magazeti jambo leo linadai BWM litavunjwa kesho. kama ni kweli mkutano wa Jmosi utapitwa na wakati.

Mpeni muda mpaka siku ya jumatano,kikao kifanyikea maazimio yawekwe under carpet then subirini kama kweli kauli ya rais inayosemwa itatekelezwa ya kuvunja baraza lake la mafisadi.(mawaziri)
 
unashindwa nini kusema unatamani Jk awe mumeo kwa jinsi unampenda? Wanaoipenda nchi hii ni wale wanaoipigania, na wanaonyesha kwa vitendo

mme kama huyo hata bure simtaki maana utazaa vichwa nazi tu
 
Raisi alitumia busara na hekima kuiacha issue ya kuwafukuza mawaziri wake.Akiwa kama Raisi wa nchi kama angemruhusu Pinda awatimue wale mawaziri kwa sababu ya kutii shinikizo la wabunge basi ndio kabisaa angeloba stepu.Kwamba kama Raisi wa nchi angeonyesha udhaifu wa hali ya juu.Pia ingekuwa ni Political gain ya Chadema na mahasimu wake ndani ya chama.Pia kujishushia hadhi sana tuu kimataifa.Pia alijua akitoa ruhusa wale mawaziri nane watimuliwe ndio kwanza angejiweka kwenye wakati mgumu zaidi maana ungekuwa ndio mchezo wa wabunge.kwamba angebidi aje kufikia hatua ya kuvunja baraza la mawaziri kila wakati au mpaka kufikia sehemu wabunge watataka kumpigia kura ya kutomwamini yeye Raisi. Naamini kabisa kinachofuatia ni yeye kulivunja baraza la mawaziri soon.anajua effects zitakazo tokea kama hatavunja baraza.hivyo kisiasa nampa hongera kwa kungamua mtego uliokuwepo mbele yake.kwa wanaotambua siasa wanajua tuu issue haikuwa kuwafukuza tu wale mawaziri
 
Hamna kitu hapo, jamaa wanataka kula posho za kikao tu, kwani nchi hii ipo katika hali nzuri sana.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CDM kimeitisha kikao cha dharura cha Baraza kuu la Taifa kutoa maamuzi mazito kuhusiana na kitendo cha serikali kushindwa kuwawajibisha na kuwachukulia hatua za kisheria mawaziri wazembe na waliofisidi wizara zao.
Kikao hicho kitafanyika jumamosi wiki hii na kinatarajiwa kutoa maamuzi mazito sana yatakayotikisa nchi na watawala.

Source:Mwananchi na John Mnyika.

Mkutano wa Jumamosi siyo wa dharula. Umepengwa tangu January mwaka huu.

Quality
 
Kimbunga,

Inaonyesha CHADEMA walishapanga huu mchezo kabla, watakuwa wamewatuma wabunge wake kufanya vile bungeni. Kwenye taarifa yao kwa vyombo va habari baada ya kamati kuu yao iliyokaa Arumeru walisema "Maamuzi ya Kamati Kuu katika mikutano iliyopita ya kutoa rai kwa Rais Kikwete kuziba ombwe la uongozi lililopo na kufanya mabadiliko ya msingi katika serikali yanapaswa kutekelezwa kwa haraka katika kipindi hiki ambapo vyombo vya serikali likiwemo Baraza la Mawaziri vinadhihirisha kutokuwa na uwezo, umakini na uwajibikaji wa pamoja

Kamati Kuu imeielekeza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chadema kuisimamia kwa karibu serikali kupitia Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 10, mwaka huu na kuwasilisha taarifa kwenye mkutano ujao wa Baraza Kuu la chama kwa ajili ya hatua zaidi iwapo mabadiliko ya msingi hayatafanyika kwa njia za kawaida za kibunge na kiserikali.

Gazeti la Nipashe liliandika haya wakati huo.

PM

Mkuu Paparazi Muwazi sawa nimekuelewa kwamba hicho kikako si cha dharura ila kilipangwa siku nyingi.

Pamoja na hayo sasa taarifa gani itawasilishwa kwenye kikao hicho ili hali mchakato wa kutokuwa na imani na Waziri Mkuu bado haujatolewa maamuzi (rejea blue hapo)? Kwa nini wasisubiri mchakato huo ufike mahala ndio wakutane na kutoa tamko?

Najua Zitto amewasilisha taarifa ya kupeleka hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu (Msimamizi was shughuli za serikali) na pia amewasilisha ombi kwamba kuwe na kikao cha dharura cha Bunge kushughulikia suala hilo; sina hakika kama Spika ameishayatolea maamuzi hayo maombi leo CDM wanakuja tena na kikao cha kutaka kutoa tamko.
 
Last edited by a moderator:
Wewe punguani kabisa.Hivi unajua maana ya kulea.Chama cha Magamba hakijakulea.Uliona wapi mlezi akaua,akafukarisha tena kwa makusudi,akaibia,akalaghai,akalawiti na kila aina nyingine ya ushenzi kwa anayemlea?
CCm kimetulea mpaka sasa, heshimuni
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom