Vikao vya NEC na Baraza Kuu CDM kujadili hali tete ya nchi!

Mimi nadhani tatizo siyo kuvunja Baraza bali hao Mawaziri wapya atawapata wapi miongoni mwa hawa wabunge wa CCM? Mwigulu na Lusinde?....
 
WARNING na TAHADHARI KUBWA.
Chadema kuweni na mkakati na msiingie katika mkumbo wa kuwa opprtunistics.
Ujumbe umeshawafikia wananchi,tulieni kidogo na muone na kupima impact yake kabla ya kuanza makabilainao makali na makubwa zaidi.
Kumbukeni kuwa mmekubalika mno mijini lakini vijijini ambapo watu wengi ni maskini hamjaweza kupenya na manelewa fika ya kuwa mtaji wa wapinzani wenu ni pamoja na umaskini wa wananchi.Sio jamii zote zina ujasiri kama wa watu wa Meru mashariki.
Naamini ukiitishawa uchaguzi halali kabisa sasa hivi bado CCM itaibuka kidedea.
Kaeni mjadili lakini msitoe tamko kali wal ultimum kwani hiyo ispofanikiwa mtakuwa mmepoteza jambo ambalo wapenzi wenu hatutalifurahia.
He who fights and run away lives to fight another day.
 
Walishauriwa, lakini hawakusikia ushauri,hata walipochunguzwa bado walikalia ripoti za uchunguzi na kuziita ni upepo mbaya. Hatukuwachagua lakini walituibia kura, hata tuliposalimu amri kwa kigezo cha amani na uongozi bora bado walikataa kujirudi na kufanya yale waliyowaahidi wana wa nchi hii. Walifanya nyuso zao na mioyo yao kuwa migumu kuliko chuma katika kukidhi matakwa ya UMMA. Ndipo wakasema, Hawa ni maskini tu na huu ni upepo tu, hawa wapumbavu tu na huu ni wivu wao dhidi ya madaraka yetu, hawajui walitakalo, hawajui njia sahihi, na wala hawajui kwamba sisi tunastahili vilivyo bora zaidi ili tuweze kusimamia vyema rasilimali zao. Kwa hiyo wakajiamulia kutapanya kila kilichopo mbele yao kwa maslahi ya matumbo yao na familia zao

Ndipo viongozi kutoka kile chama kikuu cha upinzani wakasema, tutakwenda kwa kiongozi mkuu wa nchi na kuzungumza nae, hakika huyo anaijua ile kweli UMMA uitakayo. Lakini bila kujua ama kwa kujua, kuwa yule ndiye mzizi mkuu wa matatizo, bado waliamua kumshirikisha ili kuhalalisha uamuzi wao wa Maandamano bila ukomo. Kwa namna moja nao pia walikuwa wameivunja kusudio na kuisaliti ile ari ya UMMA na vyote viishivyo juu yake, kwani vimeshachoka kunajisiwa, na wanaona mazungumzo ni namna nyingine ya kupoteza muda, kwani wawakilishi wao walishazungumza sana katika lile jumba kuu la kutungia sheria na kufikia maazimio ambayo hayakutekelezwa.

Hakika nawaambia, jukumu hili tukishindwa kulitimiza sisi, basi wanyama wa porini watalitimiza, simba kutoka mwituni atawashambulia, mbwa mwitu kutoka jangwani atawaangamiza, chui atawavizia na kuwararua vipande vipande yeyote atakayethubutu kuwahamisha katika makazi yao ya asili, kwa maana maasi yao ni makubwa na kukengeuka kwao kumekuwa ni kwingi hata kuwaudhi wanyama wa porini pia. Mwenendo wao na matendo yao wenyewe yameleta chuki dhidi yao. Sasa tazama namna ambavyo adhabu yao itakavyowachoma, kwani wamelazimisha kunywa kikombe cha Ghadhabu ya Umma
 
CDM kwa kujiridhisha we! Sie tulio na serikali tupo tuli kama maji mtungini,leo tupo uwanja wa taifa sherehe za muungano. Nyie jadilieni tamko la polisi kuhusu Dr. Slaa na tuhuma za uchochezi Mwanza
 
Rais Jakaya Kikwete ndie anayalea haya. Hivi kweli anathubutu kusema alikuwa hajui nini kinajiri bungeni...kama alikuwa hujui nn kinajiri hizo hbr alizipata wapi, asitufanye cc mazezeta. Hatuwezi kuburuzwa na wachache. Go go go Chadema. Mslilifumbie macho suala hili. Kwasasa ninyi ndo wasemaji wa wananchi.
 
Siasa kweli mchezo mchafu. Jamani si CDM wakiongozwa na Zitto wako kwenye mchakato wa kisiasa na kikatiba wa kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri MKuu sasa tena Baraza kuu linataka nini? Mchakato wa Zitto haujafika tamati leo mnaibuka na lingine? Au hoja ya Zitto inaonekana kumpa umaarufu Zitto badala ya CDM?
 
Mkuu unafiki wako na chuki yako kwa CDM imevuka mipaka sasa.
 
CHADEMA mbona ilishapanga hili kabla hata ya mkutano huu wa bunge, angalia hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/230520-chadema-jk-vunja-baraza-la-mawaziri.html

chama kilisema kuwa "kutokana na hali ya uchumi na siasa kuwa tete CC imeamua kuwa Baraza Kuu la Chadema litakalokaa Aprili mwaka huu lijadili hali hiyo na kutoa mapendekezo kwa Serikali jinsi ya kurekebisha mambo kama Rais hatalivunja baraza hilo ambalo limekuwa mzigo kwa nchi"

Serayamajimbo
 
Mkuu unafiki wako na chuki yako kwa CDM imevuka mipaka sasa.
Mkuu Molemo hapo unafiki na chuki viko wapi? Mchakato wa kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu umefikia wapi si bado unaendelea na uko sponsored na Zitto Zuberi Kabwe naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Kwa nini tusisubiri tuone outcome ya mchakato japo tu jibu toka kwa Spika?
 
Last edited by a moderator:

Kimbunga,

Inaonyesha CHADEMA walishapanga huu mchezo kabla, watakuwa wamewatuma wabunge wake kufanya vile bungeni. Kwenye taarifa yao kwa vyombo va habari baada ya kamati kuu yao iliyokaa Arumeru walisema "Maamuzi ya Kamati Kuu katika mikutano iliyopita ya kutoa rai kwa Rais Kikwete kuziba ombwe la uongozi lililopo na kufanya mabadiliko ya msingi katika serikali yanapaswa kutekelezwa kwa haraka katika kipindi hiki ambapo vyombo vya serikali likiwemo Baraza la Mawaziri vinadhihirisha kutokuwa na uwezo, umakini na uwajibikaji wa pamoja

Kamati Kuu imeielekeza Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na Chadema kuisimamia kwa karibu serikali kupitia Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 10, mwaka huu na kuwasilisha taarifa kwenye mkutano ujao wa Baraza Kuu la chama kwa ajili ya hatua zaidi iwapo mabadiliko ya msingi hayatafanyika kwa njia za kawaida za kibunge na kiserikali.

Gazeti la Nipashe liliandika haya wakati huo.

PM
 
Back
Top Bottom