Vikao vya kujadili mradi wa bwawa vyafanyika kwa miaka kumi, tunakwenda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vikao vya kujadili mradi wa bwawa vyafanyika kwa miaka kumi, tunakwenda wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fiki, Apr 14, 2012.

 1. f

  fiki New Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo(14/4/2012) nimemsikia mkuu wa wilaya ya kibondo kwenye taarifa ya habari(STAR TV) akiwakemea wanakijiji wa kijiji kimoja wilayani humo kwa kitendo chao cha kugomea kutwaliwa kwa maeneo yao kupisha ujenzi wa bwawa la maji ,kwa hoja kuwa hawakushirikishwa. Kauli ya DC ni kuwa wanakijiji hao walishaujadili mradi huo na kuukubali.Vikafuata vikao kwenye halmashauri kwa miaka kumi,hadi kupata pesa. Sasa jamani miaka kumi unajadiliwa mradi wa kijiji.Hatuoni kuwa hata walioujadili wengine wameshaenda mbele ya haki,na waliopo,ama wameusahau au hawauhitaji tena.DC hakuona busara kuwa consult upya wanakijiji kujua kama kipaumbele chao bado kipo palepale,au kuna dharula nyingine nyeti zaidi,au angalau tu kuwakumbusha kuwa ombi lao la miaka kumi ilopita limewini.Ni sahihi kweli kuwaambia malalamiko yao hayana msingi. Haya mavikao yetu wa TZ yanatupeleka pa hovyo.Miaka kumi munajadili mradi wa kijiji kimoja tu.Nayachukia mavikao,hata kama yana posho nono,Kila kukicha vikao,wakati walalahoi wanaumia kusubiri maamuzi.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,227
  Likes Received: 1,414
  Trophy Points: 280
  Nikumbushe: mradi wa DART unamiaka mingapi?, umeme wa dharura je?, vipi machinjio ya kisasa DSm?!
   
Loading...