Vikao vya CCM vimeufunika uchaguzi mkuu wa Chadema, Mbowe na Mwambe wasahaulika katika mijadala

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,589
141,391
Kiukweli uchaguzi mkuu wa Chadema kwa sasa unakwenda kimya kimya na hii ni kutokana na vikao vya kihistoria vya CCM vinavyofanyika jijini Mwanza.

Habari kuu katika media zote imekuwa ni vikao vya CCM, na hata uchaguzi wa Bavicha na Bawacha umejulikana zaidi kwa wana Ufipa wenyewe. Na hii ni fursa nzuri kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake kurejea madarakani bila kelele za hapa na pale za media.

Nawatakia sabato njema.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mkuu hata sasa vyama vya upinzani viko ndani ya CCM ndio maana Mbowe alienda kuomba maridhiano!
 
Ningeshangaa vikao vya Upinzani kufunika vya CCM, ila nachofurahi ni kwamba Pamoja na kwamba CDM haijafunika, ila imetikisa
 
Kweli kabisa bwashee.......vyama vya upinzani vilianzishwa na makada wa CCM!
Vitu vingine mnaandikaga mkiwa mmekalia vitu vyrnye ncha butu, vyama Vingi vimekuja 1992, kabla kila MTU alilazimishwa kuwa ccm si kwa kupenda.

Siyo ajabu wapenda mageuzi kutoka ccm kwenda opposition
 
Usanii mtupu na viongozi wa vyama vya upinzani wanajua fika hawawezi kukamata dola:- (Tume ya Uchaguzi kuendelea kuwa chini ya Rais na kutokuwepo sheria ya kupinga matokeo ya urais mahakamani).

Kwa kufahamu huko bado wanahimiza wafuasi wao washiriki kwenye uchaguzi mkuu. Ili hali kamwe tume ya uchaguzi haiwezi kumtangaza mpinzani Mshindi.

Nilikuwa nategemea tangu mfumo wa vyama vingi kuingia kuanzia mwanzo wangekuwa wanagomea kushiriki uchaguzi wa urais mpaka pale TUME YA UCHAGUZI ITAKAPOKUWA HURU.

Huku ni kupotezeana muda tuu vyama vya upinzani ni mawakala wa CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu wao hawana mpango na tume huru ya uchaguzi maadamu wanalipwa ruzuku yatosha!

Ila zamu hii kwa Rais Magufuli wamegonga ukuta........hakuna vya bure ukitaka siasa ingia chama dola.
 
Vitu vingine mnaandikaga mkiwa mmekalia vitu vyrnye ncha butu, vyama Vingi vimekuja 1992, kabla kila MTU alilazimishwa kuwa ccm si kwa kupenda.

Siyo ajabu wapenda mageuzi kutoka ccm kwenda opposition
Mbwiga kila mtu alilazimishwa na nani?!

Kuna watu hawajawahi kuwa Tanu wala CCM!
 
Kwa taarifa yako mambo matatu pekee ambayo watu wanajua kuhusu vikao vya CCM Mwanza ni;
1. Ndege kuachiwa (bila kujua deni limelipwa au tumesamehewa)
2. Pinda kufurahi Magufuli kama ataongeza muda ili amlindie maslahi yake pamoja na kesi ya zile bilioni za kutafuta Urais 2015 alizo takatisha na marehemu Masaburi.
3. Membe kushtakiwa ndani ya vikao.

~ Hayo pekee ambayo watu wanajua kusanyiko la Mwanza lilifanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom