Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,216
- 113,519
Kwa karibu miaka 10 sasa baadhi yetu tumekuwa tukipinga na kukemea vikali sana vikao vya CCM kufanyikia ikulu ya Dar es salaam.
Haya mambo yalishika kasi sana enzi za Jakaya Kikwete [ambaye siku hizi ni kipenzi cha makamanda].
Magufuli naye sasa anauendeleza huo utaratibu wa hovyo.
Hii inakera sana. Siipendi kabisa mimi.
Ndiyo, inawezekana si kinyume na sheria kufanyia hivyo vikao vyao hapo ikulu.
Lakini, hata kama kwa sasa si kinyume na sheria, kufanyia vikao vya kichama kwenye mali ya serikali ya Watanzania si sawa hata kidogo. Inaleta picha mbaya ya matumizi ya mali ya umma kwa shughuli binafsi za kichama.
Muda umefika sasa wa kulifanya jambo hilo liwe ni kinyume na sheria. Ningependa kuona wabunge wote wenye nia njema, bila kujali vyama na itikadi zao, kulivalia njuga suala hili na kulitungia sheria dhidi yake ili likome.
Mambo ya vyama yawe yanafanyika huko Lumumba, Ufipa, Buguruni, na kwingineko huko. Lakini siyo ikulu.
Naamini jambo kama hili linaweza kupata idadi ya kutosha ya wabunge na kuweza kulikomesha kabisa.
Wabunge kazi kwenu sasa...hebu fanyeni kazi kwa manufaa ya Watanzania wote...walau hata kwa mara moja tu.
Soma pia > Ni halali CCM kufanyia vikao Ikulu?