Vikao vya CC na NEC Dodoma: Sintofahamu Yaendelea!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,427
113,421
Hali sintofahamu, imeendelea kuvigubika vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, ambavyo vimekuwa vikiahirishwa, na kuahirishwa na sasa kuahirishwa tena na tena!.

Vikao hivyo ambavyo CC kwa mara ya kwanza ilikuwa ifanyike Ikulu Dar es Salaam, mwezi Januari, kiliahirishwa kufutia mgomo wa wajumbe kutoka Zanzibar na badala yake, wakaitisha cha kwao kubariki maridhiano na kuyapeleka moja kwa moja Baraza la Wawakilishi ambako waliyapitisha huku CCM Bara wakipigwa na Butwaa!.

Ikasemekana vingefanyika wiki ya kwanza ya kikao cha Bunge, lakini vikaahirishwa kwamba sasa vingefanyika viki ya pili ya Bunge kabla ya kuahirishwa kuwa vingefanyika wiki ya tatu ya Bunge iliyoanza jana.

Kuna taarifa kuwa vikao hivyo vimeahirishwa tena hivyo Kikao cha Bunge, kinamalizika rasmi Ijumaa hii, kama kawaida kwa buzuki la nguvu, bila uhakika vikao hivyo vitafanyika lini haswa.

Hata hivyo wajumbe wa NEC, wameshapewa taarifa rasmi kuwa wao wasisambaratike baada ya kuahirishwa kwa Bunge, kwa maelezo kuwa waendelee kuwepo mjini Dodoma kwa semina maalum ya NEC.

Hii hali ya sintofahamu, kwa upande wa vikao hivi, inaelezewa kama "kimya kingi" hivyo sasa unasubiriwa huo "mshindo mkuu", haswa kwa kuzingatiwa ni vikao hivi, ndivyo vitapokea taarifa ya Kamati ya Mzee Ruksa kuhusiana na mustakabali wa mafisadi walioko ndani ya CCM kama chama kitaamua kusuka kwa kuwakumbatia, ama kunyoa na kujisafisha kwa kunawa matanga!.

Mwana CC na NEC mmoja almaarufu kwa jina la 'king maker' ametika Dodoma asubuhi ya leo kuelekea Kwa Mzee Mandela, akiahidi kurejea wiki ijayo, hali inayoelezewa vikao kuendelea kusogezwa mbele, kutoa nafasi kwa wajumbe muhimu kumaliza issues zao! Ama kweli kumbe king maker sio tuu ni mtawala wa nchi kisiri siri, bali hata kudetermine vikao vya chama!.
 
nimesema na narudia tena
Kikwete anahitaji kumuomba Mungu sana....
maana sasa kila kitu kina fall apart under his watch....
 
Sintofahamu juu ya vikao hivi bado inaendelea, JK yuko Dodoma, pia nimemuona Msekwa. Bunge linaahirishwa kesho, mawili, kwanza kuna cabinet meeting mchana, Jumamosi au Jumapili CC ili Jumatatu NEC.
 
Is he that genious? well good for him

au mna -exagrate his powers kwa agenda zenu just curious?
 
Tumain, Sijakupata vizuri, haswa eneo hili la exageret powers za nani?.

Pasco,

Kama vikao vya CCM vinaahirishwa kwa sababu ya kumsubiri RA basi ni hatari. Kwa nini sasa asikae Ikulu tukajua moja? Ila kwa jinsi haya mambo ya Richmond na mengine yanayomhusu yanavyoendeshwa, it reveals beyond reasonable doubt that he is on the driving wheel. Tatizo ni kwamba ana-drive kutupeleka wapi?:confused::confused:
 
Nimesikia vikao vinaanza kesho na Jumapili, kwa hili la vikao vya CC na NEC, JF has our inside hivyo lets hope thead itapaishwa leo au kesho, huko tutajua zaidi.
 
Nimesikia vikao vinaanza kesho na Jumapili, kwa hili la vikao vya CC na NEC, JF has our inside hivyo lets hope thead itapaishwa leo au kesho, huko tutajua zaidi.

Ofcourse baada ya kutegua kitendawili cha Richmond, Vikao vinaweza kufanyika hata kila wiki huku bara. Sijue pale kisiwani hali ikoje kwa sasa!!!!!!!!
 
Nimesikia vikao vinaanza kesho na Jumapili, kwa hili la vikao vya CC na NEC, JF has our inside hivyo lets hope thead itapaishwa leo au kesho, huko tutajua zaidi.

Sasa hivi ni kama kumsukuma mlevi tu!!!!!!!! Ooh myh dear!
 
Sintofahamu juu ya vikao hivi bado inaendelea, JK yuko Dodoma, pia nimemuona Msekwa. Bunge linaahirishwa kesho, mawili, kwanza kuna cabinet meeting mchana, Jumamosi au Jumapili CC ili Jumatatu NEC.

Pasco kule hakuna chochote wanaenda kunywa chai tu kazi ilikuwa bungeni sasa kule watadhibitiwa kama panya katikati ya paka nikumbushe Jumanne ijayo
 
Je tutegemee nini kutoka CC na NEC?

1.
2.

1. Makofi na vigelegele
2. Maandalizi na mbinu chafu za ushindi wa kishindo 2010
3. Kukusanya hela popote na kwa njia yoyote ili kufanikisha #2 hapo juu
4. Ujio wa CCJ na ushauri wa kwa wana CCM kukichukichukia kama ukoma
5. ............................
6. ............................
 
Masuala ya ufisadi ndiyo yanayoviyumbisha vikao hivi vya juu vya CCM, tukiacha labda yale ya naridhiano Zanzibar.

Chukuwa suala hili la radar ambalo haiyumkiniki kwa Chenge kuendelea kuwamo katika vikao hivyo, hasa pia kama ni mwenyekiti wa Maadili.

Habari nilizopata ni kwamba kuna wajumbe wa NEC na CC wanataka Chenge ang'oke mwenyewe kutoka katika vikao hivyo, ama sivyo ang'olewe kwa nguvu ili kukiokoa chama na kukipa heshima iliyopotea.

Yeye mwenyewe hataki, anafanya jeuri kubwa kwa sababu hakuna atakayethubutu kumfukuza kwani anazifahamu siri za ufisadi za wakubwa, na ameshaweka bayana, kupitia kwa wapambe wake, wakiwemo akina RA, EL na hata Mkapa, kipi atakachokifanya akizidi kusukumwa ukutani. Siri nyingi anazo huyu – hasa zile za mikataba ya kifisadi – kwani alikuwa AG kwa miaka zaidi ya 12.

Halafu Mkuu wa Kaya ni dhaifu mno kutumia uwezo wake na umahiri wake kuhakikisha chama kinajisafisha na Chenge, kwani naye ana mazito yake kibao – la radar hilo hilo na Richmond. Katika vikao hivyo hubaki akicheka cheka tu bila kutilia mkazo maamuzi yoyote, na yote hii inatokana na woga alio nao.

Inasikitisha kweli kweli.
 
nimesema na narudia tena
Kikwete anahitaji kumuomba Mungu sana....
maana sasa kila kitu kina fall apart under his watch....

Mungu anasaidia waja wake pale wanapoanza kujisaidia wenyewe.....vinginevyo itabidi mungu awe ni wa miujiza kila mara....
watu wamekaa hawajishughulishi....mungu yupo anatuona, atatusaidia....mafuriko yanakuja...watu wamekomaa kukaa mabondeni...kisa, mungu yupo atatusaidia...mungu hawezi kuwa bize kusaidia wapumbavu wasiotaka kutimiza wajibu wao kwanza...
 
Uko sawa kabisa sisi tunajisaidia...kwa maana ileeeee ya kuny*......or else, hatuna la maana tunafanya. Chenge , RA, EL, Mkapa wanastahili kurushiwa mawe barabarani ikiwa mamlaka husika zinawaogopa. Na sis nao kimyaaa! ndi kwaaanza tunawaita waheshimiwa!
 
Timu ya wajumbe kutoka Zanzibar imeingia, wameletwa kwa ndege ya rais, ningesema ni lift, lakini mwenyewe kaja jana ndege ikawafuata leo. Huu sasa ni ushahidi tosha kuwa now CC na NEC ni for sure. Mkulu anafanya cabinet meeting mchana huu, ili kuokoa muda naomba msishangae kama CC itakutana usiku huu huu ili kesho NEC wakae.

Cha muhimu ni ajenda ambazo CC ndio watazipanga. Hiki ni moja ya vikao muhimu sana vya NEC kwa ajili ya kupokea taarifa ya Kamati ya Mwiny, hata hivyo nadhani vikao hivi navyo vitafunika tuu kombe kwa sababu tayari Spika Six keshakuwa mtoto mzuri!
 
Heshima mbele Mkuu Pasco,

Kwanza nikushukuru kwa kuendelea kuletea habari za hapo mjengoni na habari za NEC na CC huko Dodoma.hayo maadishi ya rangi nyekundu kwa kweli kila nikiyasoma roho inaniuma kweli sijui lini Tanzania itapata wanasiasa wenye nia njema na taifa letu.
 
Back
Top Bottom