Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,467
- 113,567
Hali sintofahamu, imeendelea kuvigubika vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM, ambavyo vimekuwa vikiahirishwa, na kuahirishwa na sasa kuahirishwa tena na tena!.
Vikao hivyo ambavyo CC kwa mara ya kwanza ilikuwa ifanyike Ikulu Dar es Salaam, mwezi Januari, kiliahirishwa kufutia mgomo wa wajumbe kutoka Zanzibar na badala yake, wakaitisha cha kwao kubariki maridhiano na kuyapeleka moja kwa moja Baraza la Wawakilishi ambako waliyapitisha huku CCM Bara wakipigwa na Butwaa!.
Ikasemekana vingefanyika wiki ya kwanza ya kikao cha Bunge, lakini vikaahirishwa kwamba sasa vingefanyika viki ya pili ya Bunge kabla ya kuahirishwa kuwa vingefanyika wiki ya tatu ya Bunge iliyoanza jana.
Kuna taarifa kuwa vikao hivyo vimeahirishwa tena hivyo Kikao cha Bunge, kinamalizika rasmi Ijumaa hii, kama kawaida kwa buzuki la nguvu, bila uhakika vikao hivyo vitafanyika lini haswa.
Hata hivyo wajumbe wa NEC, wameshapewa taarifa rasmi kuwa wao wasisambaratike baada ya kuahirishwa kwa Bunge, kwa maelezo kuwa waendelee kuwepo mjini Dodoma kwa semina maalum ya NEC.
Hii hali ya sintofahamu, kwa upande wa vikao hivi, inaelezewa kama "kimya kingi" hivyo sasa unasubiriwa huo "mshindo mkuu", haswa kwa kuzingatiwa ni vikao hivi, ndivyo vitapokea taarifa ya Kamati ya Mzee Ruksa kuhusiana na mustakabali wa mafisadi walioko ndani ya CCM kama chama kitaamua kusuka kwa kuwakumbatia, ama kunyoa na kujisafisha kwa kunawa matanga!.
Mwana CC na NEC mmoja almaarufu kwa jina la 'king maker' ametika Dodoma asubuhi ya leo kuelekea Kwa Mzee Mandela, akiahidi kurejea wiki ijayo, hali inayoelezewa vikao kuendelea kusogezwa mbele, kutoa nafasi kwa wajumbe muhimu kumaliza issues zao! Ama kweli kumbe king maker sio tuu ni mtawala wa nchi kisiri siri, bali hata kudetermine vikao vya chama!.