Vikao vya Bunge vyaanza leo. Miraj Mtaturu aapishwa rasmi kuwa Mbunge wa Singida Mashariki

Doncy monco

Member
Jul 26, 2019
38
101
Ratiba iliyotolewa na Bunge la Tanzania mbali na kuelezea shughuli zitakazofanywa na mkutano huo wa 16 ni pamoja na kiapo cha uaminifu kwa Mtaturu ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Katika ratiba ya Bunge, inaonesha miswada hiyo ni wa Sheria ya Serikali Mtandao wa Mwaka 2019, Marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 na namba 5.

Ratiba hiyo ndogo ambayo inaonyesha kuwa pia kesho kutakuwa na azimio la kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuendesha mkutano wa 9 wa jumuiya hiyo.


***UPDATE***
Miraji Mtaturu (CCM) ameapishwa kuwa Mbunge wa Singida Mashariki. Wakati wa uapishwaji wake, wabunge wa upinzani hawakuingia ndani ya ukumbi wa Bunge(Wamesusia).

Kiti cha Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, kilikaliwa na Mbunge wa Ulanga Mashariki, Goodluck Mlinga (CCM).

Pia, baadhi ya wabunge wa CCM walihamia kwenye jukwaa la upinzani ili akidi itimie.
 
Fanya mabadiliko hapa kweye hiki kisehemu.
Wakati Spika Ndugai alitoa taarifa hiyo, Lissu alikuwa nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 mchana wa Septemba 7, 2019 akitoka bungeni.
 
Bunge limerejea rasmi leo 3/09/2019 na mda mfupi uliopita Ndugu Jumanne Mtaturu ameshaapa na Yeye ndiye sasa ni Mbunge halali wa Jimbo la Singida Mashariki.

Hongera kwake na kila lililo la kheri katika kuwatumikia Wananchi wa Jimbo lile.
 
Bunge limerejea rasmi leo 3/09/2019 na mda mfupi uliopita Ndugu Jumanne Mtaturu ameshaapa na Yeye ndiye sasa ni Mbunge halali wa Jimbo la Singida Mashariki.

Hongera kwake na kila lililo la kheri katika kuwatumikia Wananchi wa Jimbo lile.
Hongera sana kwa kumwapisha tutarajie nafasi ya kwenda kasi jimboni maana Tundu Lissu alishindwa
 
Back
Top Bottom