Vikao vya Bunge vinakaribia kuanza, Serikali ina mpango gani?

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Naamini uchumi umeimarika kwa sababu tunaweza kufadhili miradi yetu wenyewe kwa sasa.. Tazama SGR, Stiegler's gorge na kadhalika.

Nilielewa dhamira ya serikali wakati ule kufungia Bunge Live kwa sababu za kiuchumi. Kuna uwezekano kweli mzee alikuta kapu limechacha, lakini kwa sasa baada ya jitihada zake tumeona uchumi umekua kwa kasi, nadhani sisi (Tanzania) ni nchi ya 2 kwa uchumi unaokuwa kwa kasi hapa Afrika.

Kwa sababu hizo, naomba turejeshewe hewani huduma ya kufuatilia vipindi vya Bunge kama zamani. Izingatiwe kuwa Watu 9 kati ya 10 wanaona umuhimu wa kurushwa live kwa vipindi vya Bunge.

Au mambo bado?!

2.JPG
 
PS: Na kudhihirisha hilo, siku hizi matukio mengi ya serikali yanarushwa Live hata kwa masaa 10..
 
Back
Top Bottom