Vijue vyakula bora na faida zake mwilini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijue vyakula bora na faida zake mwilini

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,379
  Likes Received: 4,224
  Trophy Points: 280


  [​IMG]TUNAAMBIWA kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipasavyo na kuvitumia vyakula bora pamoja na kufanya mazoezi.

  Katika makala yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa bora (super foods) ambavyo faida zake mwilini vimeanishwa. Kwa mlaji, linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza tumboni. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora, Bw.Hakeem Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri kuendelea kuwa na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya…

  [​IMG][​IMG]TUNAAMBIWA kuwa kuishi vizuri ni pamoja na kula chakula bora na sahihi. Pia, mtu anayeishi vizuri ni yule ambaye hasumbuliwi na maradhi hatari na njia pekee ya kuulinda mwili dhidi ya maradhi hatari ni kujua ipasavyo na kuvitumia vyakula bora pamoja na kufanya mazoezi.

  Katika makala yafuatayo, nitakuorodhoshea baadhi ya vyakula vinavyotajwa kuwa bora (super foods) ambavyo faida zake mwilini vimeanishwa. Kwa mlaji, linakuwa jambo la busara kujua faida ya kila chakula unachoingiza tumboni. Kwa mujibu wa mwandishi wa makala kuhusu vyakula hivi bora, Bw.Hakeem Rahman, hivi ni vyakula vinavyowafanya “wenye afya nzuri kuendelea kuwa na afya nzuri zaidi na wenye afya mbovu, kuwa na afya nzuri.”


  SAMAKI
  Wana virutubisho aina ya Omega 3 ambavyo huulinda moyo dhidi ya maradhi. Samaki pia wana virutubisho vinavyomuongezea mlaji uwezo wa kukumbuka (memory), kuna virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kansa mwilini, kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini (Bad cholesterol). (unashauriwa kula samaki kwa wingi kadiri uwezavyo).
  Baadhi ya virutubisho muhimu vinavyopatikana kwenye samaki ni pamoja na vitamini D, vitamin 12, vitamini B3, vitamini B6, Omega 3 Fatty acids, protini na madini mengine mengi.


  KARANGA
  Unaweza ukazidharau karanga, lakini zina faida kubwa mwilini. Miongoni mwa faida zake ni pamoja na kuimarisha afya ya moyo, hupunguza kolestro mbaya mwilini na kuongeza kolestro nzuri. Mafuta mazuri yaliyomo kwenye karanga hupunguza shinikizo la juu la damu na huponya magonjwa ya moyo na hupunguza uzito. Faida zote hizi unaweza kuzipata kutoka kwenye karanga au siagi iliyotengenezwa kutokana na karanga (peanut butter). (unashauriwa kula kiasi kadhaa kila siku, hasa za kuchemsha ndiyo nzuri).


  KAROTI
  Miongoni mwa faida nyingi za karoti ni pamoja na kushusha kolestro mbaya mwilini, kupunguza unene, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha shinikizo la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini. (kula kadiri unavyoweza, mbichi au zilizochemshwa).


  MAHARAGE YA SOYA
  Haya ni maharage bora kabisa ambayo yana faida nyingi mwilini, ikiwemo kushusha shinikizo la damu, kuimarisha sukari mwilini, kupambana na ugonjwa wa kisukari, figo, moyo, kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa kansa ya kibofu na magonjwa mengine ya wanawake.


  PAPAI, TIKITI MAJI
  Miongoni mwa matunda muhimu mwilini ambayo hata mgonjwa wa kisukari anashauriwa kuyala ni pamoja na papai na tikitimaji ambayo yanaelezwa kuwa na kiwango kikubwa cha ufumwele (fibre) na hivyo kutoa mchango mkubwa sana katika kuimarisha kiwango cha sukari mwilini. (kula kiasi cha moja katika ya matunda hayo mawili, kila siku).


  KITUNGUU SAUMU
  Hiki ni kiungo cha mboga, licha ya kuonekana kama ni kiungo cha kuongezea ladha tu ya chakula, lakini ni miongoni mwa vyakula vyenye faida kubwa katika afya zetu. Kitunguu saumu husaidia kuyeyusha damu mwilini hivyo kumuepusha mlaji kushikwa na ugonjwa wa moyo pamoja na presha. Kitunguu hicho pia hutoa kinga kwenye ini na huondoa maumivu ya viungo. Kula angalau kitunguu kimoja mara moja kwa wiki.


   
 2. Mhindih

  Mhindih JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Ahsante
   
 3. m

  mipango k Senior Member

  #3
  Dec 29, 2012
  Joined: Oct 31, 2012
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante,uongezewe zaidi.
   
 4. N

  Noboka JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,115
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Shukrani kwa taarifa nzuri. Tatizo letu ni kutokuwa watu wa maarifa, hivyo vyakula vyote pamoja na umhimu wake, gharama yake ni chini ya sh. 5000, lakini shangaa wa Tz hasa hapa bongo yuko tayari kununua Kitimoto Tsh. 10,000 na Tusker baridi ambavyo vyote mwilini faida zake ni ndogo sana.
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,792
  Likes Received: 1,594
  Trophy Points: 280
  heading yako nilijua umeagwanya vyakula kwa makundi hivyo nikapata raha kweli kuona kwamba leo hii tunapata somo la lishe bora/ mlo kamili.
   
 6. REMSA

  REMSA JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,569
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Thank u
   
 7. M

  MASOUD NYUMBANYINGI Member

  #7
  Dec 29, 2012
  Joined: Nov 11, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  thanx mkuu kwa elimu
   
 8. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,106
  Likes Received: 1,567
  Trophy Points: 280
  Na wewe pia umemsaidia MziziMkavu kutoa elimu kuhusu mbinu ya kuweza kununua matunda maana mtu anaweza akawa anakunywa kila siku kilaji lakini akashindwa kununua matunda
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,106
  Likes Received: 1,567
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu kwa elimu maana watz huwa tunakula kutokana na utamu wa mboga au tunda na si kwa umuhimu wa kitu
   
 10. Isumbwile

  Isumbwile JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2012
  Joined: Dec 12, 2012
  Messages: 805
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kama kawa kama dawa,always ur threads are educative...thanx kwa sana!!
   
Loading...