Vijimambo vya shemeji!

Rah_sputin

Member
Nov 3, 2009
83
10
Ninaye shemeji ambaye anatutia aibu sana sisi kwenye ukoo wetu.

Yeye hujifanya mtu wa heshima nyingi,ana cheo kikubwa, mali na kila kitu.ana mke na watoto na kila ambacho mtu angetamani akipate. Tatizo lake ni moja - kutaka kila sketi aionayo.tukianza na nyumbani kwake...

Hakuna mfanyakazi wa kike anaacha kumtaka kimapenzi. Kazini kwake kamaliza wanawake wote. Kibaya sasa anaanza kunyemelea ndugu zake wa damu!

Amekuwa akimlea binti mmoja yatima ambaye ni mwana wa shangazie - yaani binamu take. Amemsomesha hadi akamaliza. Sasa anamdai ujira wa mapenzi. Je huyu binti afanyeje? Amemkatalia lakini jamaa kakomaa tu. Binti kahama hadi nyumbani. Binti ni mcha mungu sana na hataki katakata kujiingiza kwenye uchafu huu wa binamu ambaye kwanza kamlea kama baba maana analingana na watoto wa huyu shemeji.

Mshaurini huyu yatima.
 
Tatizo munamuogopa sababu ana vijisenti,pia mmekuwa wanafiki kwa kuwa mnashindwa kumweka kiti moto live,haingii akilini ukoo wote mnanyea wakati ndugu yenu anaendeleza uchafu.Mwambieni ukweli badala ya kulalamika pembeni.
 
tatizo munamuogopa sababu ana vijisenti,pia mmekuwa wanafiki kwa kuwa mnashindwa kumweka kiti moto live,haingii akilini ukoo wote mnanyea wakati ndugu yenu anaendeleza uchafu.mwambieni ukweli badala ya kulalamika pembeni.
hasante kwaushauri.
Tatizo siyo kuwa tunamuogopa.tatizo ni kuwa ni mjanja sana kwa kuruka vihunzi akiulizwa na hakawii kusema wanamsingizia.wasichana wa kazi ambao wanamkataa basi atazusha tafrani hapo nyumbani hadi wafukuzwe kazi.dada yetu alikuwa anamuamini sana shemeji na aliamini kila analomuambia.
Hili la binamu sasa limemuumbua na hadi sasa limefikiswa kwa baba mzazi wa shemeji.bado tunasubiri itakuwaje.dada naye kaamua kuachana na mumewe huyu mkware. Tatizo, atawaambia nini watoto wake ambao sasa ni wakubwa?
 
Short and clear, awaambie tuu ukweli (nimeachana na babayenu kwa kuwa ni malaya) kama watoto ni wakubwa haya mambo wanayaelewa vizuri na watamchukia pia sana baba yao kwa tabia yake hiyo mbofu.
 
Huyo binti aendelee kumcha bwana na asikubali kumvulia huyo mzee kijana kikubwa hapo ni msimamo tu.
 
Short and clear, awaambie tuu ukweli (nimeachana na babayenu kwa kuwa ni malaya) kama watoto ni wakubwa haya mambo wanayaelewa vizuri na watamchukia pia sana baba yao kwa tabia yake hiyo mbofu.
Hichi ndicho nachohofia zaidi
 
Mkalisheni kikao cha ukoo msuluishe mambo, kama mnamuogopa atawatembelea ukoo wote awamalize!
 
Mlengesheni mtego tu..abambwe live siku moja na apewe dispilini, then atakoma ubishi.

Hela zake zisiwalevye nyie watu!

Umasikini nao bana ni shida sana!
 
Fanyeni maombi, kwa Mungu hakuna linaloshindiakana, namshauri mke wake afunge na kuomba bila kuchoka ataacha tu huu ufirauni.
 
sijui nimlaumu mama kwa uzembe?

wameishi kipindi chote mpaka watoto wanakuwa hajajua tabia ya mmewe? kwanini mwanaume ndo azushe tafrani kwa housegirl? hata mwanamke hakushtuka mahousegirl wanaondoka kwa same reason?

kazini siwezi sema maana hayo tunakutana nayo huku maofisini lkn home mama ndo anamjua housefirl kuliko baba.
 
Fanyeni maombi, kwa Mungu hakuna linaloshindiakana, namshauri mke wake afunge na kuomba bila kuchoka ataacha tu huu ufirauni.
hata katika vitabu vya dini kwa wale wakiristu (Bible) mwanamke aliye na hekima huijenga nyumba yake naye aliye mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe. amechelewa nalkn ana nafasi bado kama atasugua goti.
 
Ana mapepo huyo!!!! Mleteeni wachungaji aombewe!

Mi kuna mmoja namfuhamu anaishi kanda ya kati..... nadhani yeye ni zadi ya huyu, tabia chafu sana hii.
 
hasante kwaushauri.
Tatizo siyo kuwa tunamuogopa.tatizo ni kuwa ni mjanja sana kwa kuruka vihunzi akiulizwa na hakawii kusema wanamsingizia.wasichana wa kazi ambao wanamkataa basi atazusha tafrani hapo nyumbani hadi wafukuzwe kazi.dada yetu alikuwa anamuamini sana shemeji na aliamini kila analomuambia.
Hili la binamu sasa limemuumbua na hadi sasa limefikiswa kwa baba mzazi wa shemeji.bado tunasubiri itakuwaje.dada naye kaamua kuachana na mumewe huyu mkware. Tatizo, atawaambia nini watoto wake ambao sasa ni wakubwa?

Huu si uamuzi wa busara, ifike wakati tuwe na tahadhari kwamba kutokana na vyakula mbalimbali watu wanavyokula siku hizi yaweza kuwa ameathirika ki afya (ana nguvu za kiume kuliko anavyohitaji).Mtu huyu anastahili msaada, kwanza aonane na medical doctor halafu kama tatizo halitojulikana waende tiba asilia.

Kama huyo bi mkubwa huyo ni mume wa ujana wake nina hakika kama ingekuwa tabia yake kutoka mwanzao angekuwa ameishaifahamu kwa kuwa ni tabia mpya msi mzire huyo mpiganaji kuna familia zingine zina matatizo strikers kama hao wana hitajika sana, hiyo ni lulu isipotezwe.
 
kama ni wewe pole sana na pia kama ni mwingine unamsemea mpe pia pole
 
Huu si uamuzi wa busara, ifike wakati tuwe na tahadhari kwamba kutokana na vyakula mbalimbali watu wanavyokula siku hizi yaweza kuwa ameathirika ki afya (ana nguvu za kiume kuliko anavyohitaji).Mtu huyu anastahili msaada, kwanza aonane na medical doctor halafu kama tatizo halitojulikana waende tiba asilia.

Kama huyo bi mkubwa huyo ni mume wa ujana wake nina hakika kama ingekuwa tabia yake kutoka mwanzao angekuwa ameishaifahamu kwa kuwa ni tabia mpya msi mzire huyo mpiganaji kuna familia zingine zina matatizo strikers kama hao wana hitajika sana, hiyo ni lulu isipotezwe.

Asante,,,, ila unamaanisha nini?
 
Short and clear, awaambie tuu ukweli (nimeachana na babayenu kwa kuwa ni malaya) kama watoto ni wakubwa haya mambo wanayaelewa vizuri na watamchukia pia sana baba yao kwa tabia yake hiyo mbofu.

Usidanganyike kunguru daima hafugiki na maji hayasahau kale yake.Watoto wa nyoka nao ni nyoka tu.Wakikua watafanya hayo hayo ya baba yao.Kuna udhaifu umejificha katika hili,ukiachia tabia za mtu binafsi kuna mapungufu katika ndoa yawezayo kusababisha hali hii.Twaweza kumlaumu saana huyu baba kumbe taabu ni ya mama hajasimama katika nafasi yake kama mke wa ndoa.

Lipo jambo linalokosekana ndani ya ndoa na wala si ukware wa huyo shemejiyo.Hata hivyo nawe huko kwa shemejio unakutakia nini ??Ili hali unajua nawe yatakukuta kwa upande wako pia.
 
Ninaye shemeji ambaye anatutia aibu sana sisi kwenye ukoo wetu.

Yeye hujifanya mtu wa heshima nyingi,ana cheo kikubwa, mali na kila kitu.ana mke na watoto na kila ambacho mtu angetamani akipate. Tatizo lake ni moja - kutaka kila sketi aionayo.tukianza na nyumbani kwake...

Hakuna mfanyakazi wa kike anaacha kumtaka kimapenzi. Kazini kwake kamaliza wanawake wote. Kibaya sasa anaanza kunyemelea ndugu zake wa damu!

Amekuwa akimlea binti mmoja yatima ambaye ni mwana wa shangazie - yaani binamu take. Amemsomesha hadi akamaliza. Sasa anamdai ujira wa mapenzi. Je huyu binti afanyeje? Amemkatalia lakini jamaa kakomaa tu. Binti kahama hadi nyumbani. Binti ni mcha mungu sana na hataki katakata kujiingiza kwenye uchafu huu wa binamu ambaye kwanza kamlea kama baba maana analingana na watoto wa huyu shemeji.

Mshaurini huyu yatima.
.....Inaonekana huyu,kuna stages fulani katika maisha aliziruka!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom