Vijimambo vya kisiasa: Si kutumbua majipu,ni kupanga safu

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Rais Magufuli nampongeza kwa jambo moja. Jambo la kuunda msamiati wa kisiasa. Msamiati wa kutumbua majipu. Rais Magufuli ametumia msamiati huu kupanga safu yake ya uongozi. Ameweka wa kwake. Amesuka safu kwa kuteua,kutengua,kuondoa na kuweka.

Wananchi wamemuelewa vibaya Rais. Wamedhani kutumbua majipu ni kupambana na wizi na ufisadi. Wananchi wamepigwa chenga na msamiati wa Rais alioanza nao Bungeni,Dodoma. Nasema hapa kuwa kutumbua majipu si kupambana na ufisadi. Ni kupanga safu ya uongozi tu. Kupata ngozi mpya.

Kupambana na ufisadi ni kupambana na mizizi yake. Mikataba mibovu,sheria mbovu na ukosefu wa nia dhabiti ya kisiasa ndiyo mizizi ya ufisadi Tanzania. Wapi mambo haya yameshughulikiwa?

Siasa ina misamiati. Siasa ina vijimambo. Kutumbua majipu ni moja ya misamiati na vijimambo hivyo!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Ngoja Jipu lowassa litumbuliwe ndio utajua kama anawapangia safu UKAWA au anatumbua majipu?
 
Mzee Vuta Nkuvute mwambie arudi Kutumbua lile alilopeleka pale Bungeni,maana ile zawadi ya Christmas haifai hata kwa Chumvi
 
na alisema hata wale wenye arufu ya rushwa awafai kwenye serikali yake lakin cha ajabu kawaweka muhongo.mwakyembe.na kama aitoshi chenge wamempa uenyekiti.yaani ni full usanii tu
 
Back
Top Bottom