Vijana zaidi ya 500 wamekutwa wamehifadhiwa sehemu mbalimbali Mkoa wa Kilimanjaro wakifanya mafunzo yasiyojulikana

Vijana 500 wamekamatwa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wakiwa wanapatiwa mafunzo yasiyo rasmi mafichoni.

Mkuu wa wilaya ya Moshi mh Mtanda amesema vijana hao wametoka katika mikoa mbalimbali na viongozi wao 6 wanahojiwa na polisi.

Source: ITV habaHongera
Hii habari siyo nzuri na inasikitisha sana.

Vijana zaidi ya 500 waliokuwa wakipewa mafunzo juu ya ile biashara pendwa ya kujionyesha umefanikiwa kifedha na mali kutokana na mauzo ya virutubisho vy Global Alliance wametiwa mbaloni.

Kinachosikitisha ni pale ambapo viongozi wa serikali kusema vijana hao waliotoka mikoa mbalimbali, hawajui walikuwa wanapewa mafunzo gani wakati inafahamika mafunzo na biashara hiyo imekuwepo miaka kadhaa huko nyuma.
Hongera hii habari nilivyoina nilidhani huko mafichoni wanafundishwa ugaidi

Ila na bado wapo kibao wazee wa pyramid schemes wakina sudii slaaa wa inclusive
 
Mbona matangazo ya kuwavuta hao vijana yalibandikwa kila kona na huyo mkuu wa mkoa anayaona

Sio huko Kilimanjaro tu hata huko Simiyu nk watu wanapigwa hela sana kwa kudanganywa watoe pesa za kuchukulia fomu za ajira
 
Hawa vijana wana umri,

kati ya miaka 18 na miaka 20.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza,amewaamuru warudi mikoa walikotoka.

Swali langu ni kwamba,kwa nini.

Radia One wakubali kutangaza habari za namna hii,kwa nini wakubali kutangaza habari kwa staili hii. Mafunzo yasiyojikana ndio mafunzo gani?
----

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai, ametoa siku saba kwa vijana zaidi ya 500, wanaodaiwa kutapeliwa ajira na kampuni ya Alliance Motion in Global, mjini Moshi, kurudi makwao.

Kagaigai ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza na vijana hao ambapo amesema watakaokiuka agizo hilo na kuendelea kuwepo mkoani Kilimanjaro baada ya siku saba, watahesabika ni wahalifu na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo pia alimuagiza Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, kufuatilia mtandao wote uliohusika na utapeli huo kwa kuwahoji viongozi halali wa kampuni hiyo na watuhumiwa wafikishwe mahakamani haraka.

Vijana hao kutoka mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Mbeya,Shinyanga, Kigoma na Tanga, wanadaiwa kutapeliwa ajira walizoahidiwa katika kampuni ya Alliance Motion in Global na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Joseph.

Vijana hao wanadai kutozwa Sh200,000 hadi Sh900,000, na kuahidiwa kupewa ajira, kwa sasa wamepangishiwa vyumba katika kata ya Majengo na Njoro mjini Moshi na chumba kimoja wanakaa watu wanne huku wakidai kuishi mazingira magumu na hawana chakula.

Kigaigai amesema tukio hilo ni hatari kwa usalama na kumuagiza kamanda wa polisi kuwasiliana na makamanda wa polisi mikoa mingine ili kufuatilia mtandao huo unaojihusisha na utapeli huo hapa nchini.

"Ninyi mlikuwa mnashughulika na wezi na mmetapeliwa, poleni sana vijana, hakuna utaratibu wa mtu kuomba kazi na kuambiwa atume fedha kwanza na mimi ninachoelekeza rudini makwenu mlipotokea" amesema Kagaigai.

"Wote mlioitwa na kampuni hii walioko Kilimanjaro, ndani ya siku saba, muwe mmeondoka Kilimanjaro mrudi makwenu, mnaweza kuharibikiwa maisha na nisingependa hilo litokee, rudini nyumbani mkafanye kazi halali"

"Kwa kijana ambaye hataondoka, tutamchukulia ni mzururaji na sheria ya uzururaji itafanya kazi yake, lakini niombe wakuu wa mikoa wenzangu hili wimbi ni baya, yawezekana pia lipo mikoa mingine, tushirikiane kulidhibiti hili" amesema

Amewataka Wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Serikali za mitaa kurejea utaratibu wa zamani wa kuwahoji wageni wanaoonekana katika maeneo yao, ili kudhibiti matatizo kabla ya madhara.

"Wenyeviti wa mitaa na watendaji, naaomba tuanze ule utaratibu wa zamani, ambapo alikuwa akionejana mtu hafahamiki, alikuwa akihojiwa na taarifa kutolewa kwa uongozi wa juu, sasa Kilimanjaro ni lazima turudi huko, tukiona wageni tuwahoji na tukipata shaka tuende zaidi hadi polisi"

Akizungumza mmoja wa vijana hao, anatokea Mkoa wa Mara, Stephano Chacha, amesema wanaishi mazingira magumu na kwa sasa hawana chakula.

"Wakati tunakuja niliambiwa nije na Sh250,000 na baadae nilipofika walimpigia baba yangu simu kumwambia kuwa nimefaulu vizuri, atume Sh600,000 kwa ajili ya kutumiwa vifaa mbalimbali na kompyuta na hela ile ikatumwa," amesema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema wanaendelea kuwashikilia watu sita na msako unaendelea kumtafuta mmiliki wa kampuni hiyo.

"Yapo madai kuwa watu hawa baada ya kubanwa Kilimanjaro, wamekimbilia mikoa mingine, na kwa mujibu wa taarifa wamekimbilia Singida, Mbeya na mikoa mingine, niombe makamanda wenzangu, tusaidiane na kupeana taarifa za kundi hili linalotapeli watu kwa mgongo wa kuwapa ajira" amesema.

Chanzo: Mwananchi
Impact of severe unemployment
 
Walikuwa wanajifunza mbinu za ugaidi.
Ivi huwa mnajua hata tafsiri ya gaidi kweli? Ulishaambiwa wametapeliwa wewe unawaita magaidi?? Embu msome kidogo hiyo sheria ya ugaidi mjue ina nn ndani???
Liserikali lenu limeshindwa kutoa ajira kwa vijana kupitia vile viwanda 4000 vya UONGO mnashinda mitandaoni kusingizia watu ugaidi!!!!
Yaani mtu alilie 200000 ili akawe gaidi????
 
Hawa vijana wana umri,

kati ya miaka 18 na miaka 20.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza,amewaamuru warudi mikoa walikotoka.

Swali langu ni kwamba,kwa nini.

Radia One wakubali kutangaza habari za namna hii,kwa nini wakubali kutangaza habari kwa staili hii. Mafunzo yasiyojikana ndio mafunzo gani?
----

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Steven Kagaigai, ametoa siku saba kwa vijana zaidi ya 500, wanaodaiwa kutapeliwa ajira na kampuni ya Alliance Motion in Global, mjini Moshi, kurudi makwao.

Kagaigai ametoa agizo hilo leo Jumatano, Septemba 15, 2021 wakati akizungumza na vijana hao ambapo amesema watakaokiuka agizo hilo na kuendelea kuwepo mkoani Kilimanjaro baada ya siku saba, watahesabika ni wahalifu na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu huyo pia alimuagiza Kamanda wa Polisi Kilimanjaro, kufuatilia mtandao wote uliohusika na utapeli huo kwa kuwahoji viongozi halali wa kampuni hiyo na watuhumiwa wafikishwe mahakamani haraka.

Vijana hao kutoka mikoa ya Mara, Tabora, Singida, Mbeya,Shinyanga, Kigoma na Tanga, wanadaiwa kutapeliwa ajira walizoahidiwa katika kampuni ya Alliance Motion in Global na mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Joseph.

Vijana hao wanadai kutozwa Sh200,000 hadi Sh900,000, na kuahidiwa kupewa ajira, kwa sasa wamepangishiwa vyumba katika kata ya Majengo na Njoro mjini Moshi na chumba kimoja wanakaa watu wanne huku wakidai kuishi mazingira magumu na hawana chakula.

Kigaigai amesema tukio hilo ni hatari kwa usalama na kumuagiza kamanda wa polisi kuwasiliana na makamanda wa polisi mikoa mingine ili kufuatilia mtandao huo unaojihusisha na utapeli huo hapa nchini.

"Ninyi mlikuwa mnashughulika na wezi na mmetapeliwa, poleni sana vijana, hakuna utaratibu wa mtu kuomba kazi na kuambiwa atume fedha kwanza na mimi ninachoelekeza rudini makwenu mlipotokea" amesema Kagaigai.

"Wote mlioitwa na kampuni hii walioko Kilimanjaro, ndani ya siku saba, muwe mmeondoka Kilimanjaro mrudi makwenu, mnaweza kuharibikiwa maisha na nisingependa hilo litokee, rudini nyumbani mkafanye kazi halali"

"Kwa kijana ambaye hataondoka, tutamchukulia ni mzururaji na sheria ya uzururaji itafanya kazi yake, lakini niombe wakuu wa mikoa wenzangu hili wimbi ni baya, yawezekana pia lipo mikoa mingine, tushirikiane kulidhibiti hili" amesema

Amewataka Wenyeviti wa mitaa na watendaji wa Serikali za mitaa kurejea utaratibu wa zamani wa kuwahoji wageni wanaoonekana katika maeneo yao, ili kudhibiti matatizo kabla ya madhara.

"Wenyeviti wa mitaa na watendaji, naaomba tuanze ule utaratibu wa zamani, ambapo alikuwa akionejana mtu hafahamiki, alikuwa akihojiwa na taarifa kutolewa kwa uongozi wa juu, sasa Kilimanjaro ni lazima turudi huko, tukiona wageni tuwahoji na tukipata shaka tuende zaidi hadi polisi"

Akizungumza mmoja wa vijana hao, anatokea Mkoa wa Mara, Stephano Chacha, amesema wanaishi mazingira magumu na kwa sasa hawana chakula.

"Wakati tunakuja niliambiwa nije na Sh250,000 na baadae nilipofika walimpigia baba yangu simu kumwambia kuwa nimefaulu vizuri, atume Sh600,000 kwa ajili ya kutumiwa vifaa mbalimbali na kompyuta na hela ile ikatumwa," amesema

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amesema wanaendelea kuwashikilia watu sita na msako unaendelea kumtafuta mmiliki wa kampuni hiyo.

"Yapo madai kuwa watu hawa baada ya kubanwa Kilimanjaro, wamekimbilia mikoa mingine, na kwa mujibu wa taarifa wamekimbilia Singida, Mbeya na mikoa mingine, niombe makamanda wenzangu, tusaidiane na kupeana taarifa za kundi hili linalotapeli watu kwa mgongo wa kuwapa ajira" amesema.

Chanzo: Mwananchi
Kumbe siku hizi uhuru wa kutembea na kuishi popote Tanzania bila kuvunja sheria haupo tena au mpaka tuombe ruhusa Polisi? Bila ruhusa tunaitwa wazurulaji? Mhhh hivi tunaviongozi gani Tanzania?
 
Hii habari siyo nzuri na inasikitisha sana.

Vijana zaidi ya 500 waliokuwa wakipewa mafunzo juu ya ile biashara pendwa ya kujionyesha umefanikiwa kifedha na mali kutokana na mauzo ya virutubisho vy Global Alliance wametiwa mbaloni.

Kinachosikitisha ni pale ambapo viongozi wa serikali kusema vijana hao waliotoka mikoa mbalimbali, hawajui walikuwa wanapewa mafunzo gani wakati inafahamika mafunzo na biashara hiyo imekuwepo miaka kadhaa huko nyuma.

UKIACHA UWEPO WA BIASHARA HIYO PIA IMESAJILIWA KISHERIA.
Hii nchi inaitwa Danganyika so kinachoendelea ni matapeli waliobarikiwa na baadhi ya viongozi kuwachinjia wahanga wa utapeli baharini.
Kirahisirahisi aliyetapeliwa anatishwa aondoke pasipo kujua haki yake ataipataje???
 
Nimesikia clouds muda si mrefu. Ni kuwa kuna vijana 500 wameenda kilimanjaro ili kupata kazi kwa kampuni fulani. Kufika kumbe kampuni ya kitapeli, wameachwa kwenye mataa.

Wale matapeli wamekamatwa. Sasa mkuu wa mkoa anataka vijana hao waondoke sababu hawana kazi hivyo wanaweza kuwa wahalifu. Vijana wanalalamika kwanini waambiwe waondoke wakati wengine wameanza kupata vibarua hapa na pale.
Sasa hilo suala ni sawa? Ni nani mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro?
 
Mkuu kwanini hukuangalia kwanza undani wa habari hii hapa JF na badala yake ukakurupuka kuanzisha uzi wa kijinga kama huu!
Mods futa hii thread tafadhari!
 
Nimeileta habari kama ilivyotangazwa na Clouds fm. Na mkuu wa mkoa amehojiwa na vijana wanaoambiwa waondoke wamehojiwa.
 
Mkuu wewe ni muungwana sana! Kumradhi, nilitakiwa nikuelezee kuwa hii habari ipo hapa tangu juzi....vijana hao ni wahanga wa utapeli unaoendelea kwa kasi sasa hivi!
 
Hao ni wale wa Q net and the likes, sijui huwa wanawapa madawa gani, maana wanakuwa kama wamepagawa walifukuzwa eneo moja wakaenda eneo jingine
 
Back
Top Bottom