Vijana zaidi ya 300 zanzibar wanufaika na fursa za ajira

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019








Vijana zaidi ya 300 visiwani Zanzibar wamenufaika na fursa mbali mbali za ajira zilizotolewa na Taasisi zaidi 25 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.



Baadhi ya Taaisisi hizo ni NMB, Emerson Hotel, ZNCCIA,Elimu ya Amali na Mabaraza ya Vijana Zanzibar, Ambazo zote zilitoa fursa mbali mbali za ajira kwa vijana zaidi ya 300 walijitokeza katika Tamasha la Ajira kwa Vijana 2019.

Tamasha hilo liliandaliwa na Shirika la VSO na kufanyika katika viwanja vya chuo cha utalii Zanzibar Maruhubi Mjini Magharib Unguja.

Akifungua Tamasha hilo Waziri wa Kazi, Uwezeshaji,Wazee, Wanawake na watoto Zanzibar Moudline Castiko alisema tamasha hilo limekuja kuunga mkono jitihada za serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuwapatia vijana ajira.

Alisema tatizo la ajira kwa vijana ni kubwa ambapo vijana wengi Zanzibar bado hawana ajira zilizokuwa rasmi zinazoweza kuwaingizia kipato na kujikwamua na maisha.

"Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa 2014 ambao hadi sasa tunatumia unaonesha kuwa vijana takribani asilimia 21 tu ndio wenye ajira zilizokuwa rasmi zinazowaingizia kipato"alieleza Waziri Castiko.

Aidha alieleza kuwa tafiti hiyo inaonesha kuwa vijana wengi bado hawana ajira na kuwa tegemezi.

Hata hivyo waziri Castiko alitoa wito kwa vijana walijitokeza katika tamasha hilo kuchangamkia fursa hizo za ajira ambapo watapata kuajiriwa na kupewa mafunzo ya kujiajiri wenyewe.

"Nataka niwambie vijana wangu tumie ipasavyo fursa hiii ya tamasha la ajira kwa kujifunza mabo mbali mbali ikiwemo njia ya kupata mikopo na kuwawezesha kukopa na kuanza biashara zenu wenyewe sambamba na kujifunza na namna ya kuwa na sifa za kuweza kuwajiriwa"waziri aliwaeleza vijana hao.

Aidha aliongeza kuwambia vijana hao Serikali haina uwezo wa kuwaajiri vijana wote nchini badala yake wachangamkie fursa kama hizo ili kujitengenezea nafasi ya kupata ajira na kujiajiri wenyewe.

Hata hivyo aliwataka vijana hao kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na rushwa wakati wa mchakato wa kutafuta ajira.

"Najua katika kipindi hichi cha kutafuta ajira kuna matukio mengi yanaweza kujitokeza iiwemo udhalilishaji rushwa ya ngono hivyo vijana munatakiwa kupiga vita vitendo hivyo kwa kuripoti sehemu husika pindi vinapotokea" alifafanua Waziri.

Kwa upande mwingine aliwapongeza waandaji wa tamasha hilo kwa kuja na mbinu ya kuwakutansha vijana ambao wanatafuta ajira na taaasisi mbali mbali ili kuwapatia fursa walizokuwa nazo.
 
Back
Top Bottom