SoC01 Vijana wenzangu tukalime kilimo kinalipa sana

Stories of Change - 2021 Competition

DustBin

JF-Expert Member
Jun 3, 2021
544
558
“Vijana wenzangu tukalime, kilimo kinalipa sana” haya yalikua maneno ya rafiki yangu mmoja ambae aliacha kazi yake ya kupiga picha (Camera Man) na kuhamia shambani kulima.

Bwana Jenkeni ni rafiki yangu wa karibu sana, nilifahamiana nae mwaka 2014 alialikwa nyumbani Kimara kwenye sherehe ya kumbukizi ya kuzaliwa mdogo wangu wa mwisho. Alipata tenda ya kuandaa mkanda wa video. Ni mahiri sana kwenye kazi ya upigaji picha kwa sababu amesomea, na kubwa zaidi alikua na vifaa vya kutosha vya kisasa; hiyo ndio kazi iliyokua ikimuweka mjini. Lakini miaka minne mbele mwaka 2018 aliamua kufunga ofisi yake ya video production iliyopo pale Magomeni kanisani na vifaa vyake akavirejesha nyumbani kwake na kufanya safari kwenda Namtumbo kuanza shuguli za kilimo lakini familia yake ilibaki mjini. Maamuzi yake yalikuja baada ya kufanya uchunguzi mdogo na kujiridhisha kuwa huko Namtumbo kuna ardhi safi sana kwa kilimo cha maharage, mahindi, viazi na alizeti.

Alichokifanya mwaka ule alikodi shamba la hekari kumi, kwa sababu kila hekari moja alikodi kwa shilingi elfu hamsini kwa hiyo alilipa laki tano kwa ajili ya msimu wa 2018/2019. Akatumia vibarua kusafisha shamba lote kwa gharama ya laki moja na elfu hamsini. Akalipa pango ya nyumba aliyokua amefikia pale Namtumbo kiasi cha shilingi elfu sitini kwa miezi sita. Kiasi cha fedha kama laki nne hivi akanunua mbegu, dawa, mbolea pamoja na sumu za kuua wadudu waharibifu. Akawapata vijana kama watano hivi wa kulinda shambani ambao walikubaliana anawahudumia chakula, huduma ya afya wanapoumwa na huduma ndogo ndogo ili wao wahudumie shamba na malipo yao ni hapo baadae watakapovuna. Hivyo alikua anakaa Namtumbo muda kidogo anarejea mjini kuona failia yake.

Mwaka huo alilima mahindi na maharage, ambapo kipindi cha mavuno kilipofika Jenkeni alifanikiwa kupata tani tatu za mahindi na tani mbili za maharage. Mavuno hayakua mazuri kwa sababu kwanza alichelewa kuliandaa shamba mapema, lakini pia ugeni katika sekta ulichangia kwa kiasi kikubwa. Na hata hivyo mvua hazikua za maana hivyo ustawi haukua wa kuridhisha. Hivyo mazao aliyapeleka sokoni ambapo alipata fedha kidogo tu zilizokua zimerudisha gharama zake zote. Faida alipata kidogo pia ambayo aliitumia kununua sehemu ya shamba alilokua amelikodi.

Mwaka uliofuata alijitahidi kuandaa shamba mapema na alitumia muda mwingi huko shamba ili kuhakikisha usimamizi. Akaongeza idadi ya vijana wa kufanya kazi shambani, mavuno yakaongezeka kidogo haikua sawa na mwaka uliopita. Akapata mara mbili ya mazao aliyopata mwaka jana.

Maajabu yamekuja kutokea mavuno ya mwaka huu ambao Jenkeni ameuaga umasikini. Pamoja na mavuno yake ya shambani lakini pia mwaka huu alikua na fedha za kununua mazao hayo hivyo alifanikiwa kuwa na mzigo wa maana. Shamba lake lilizalisha tani ishirini za mahindi, tani kumi na tano za maharage, viazi tani nane na linunua tani saba za mazao mchanganyiko. Na sokoni mwaka huu bei imechangamka basi amevuna fedha ya maana sana. Anachokifanya Jenkeni huwa akishamaliza kukusanya mzigo wake anausafirisha mwenyewe hadi Dar-es-Salaam sokoni.

Muda mrefu umepita nilikua sijaonana na Jenkeni, wiki iliyopita alinitembelea ofisini kwangu ndio akanipa hadithi yake hii yenye mafanikio makubwa. Akaniambia mwaka huu ana mpango wa kununua mashine ya kukoboa na kusaga ili akazifunge huko huko Namtumbo mwakani akivuna aanze kufungasha unga yeye mwenyewe awe anausambaza kwa wafanyabiashara. Nilivutiwa na kisa hiki cha rafiki yangu mpiga picha aliyehamia katika ukulima nikaona nami niwakumbushe vijana wenzangu ya kwamba “tukalime, kilimo kinalipa sana.”

DustBin
 
Tea

Labda humo shambani wakati analima aliokoto jiwe la madini ghali. Laa sivyo kilimo ni hasara tupu. Usidanganyike.
 
Vijana pasua kichwa sana kuwaingiza kwenye kilimo maana tunaona wastaafu wengi wakizeeka ndio wanaamia mashambani.. vizuri uwekeze kwa wakulima ambao wanafeli katika kilimo kila siku ukawape funzo zuri na kilimo cha kisasa wakafanikiwe.. mkuu
 
Kauli za kuvunjana moyo zishindwe
Nayajua hadi mashamba yake kule S/Wanga. Sasa jifananishe wewe na Sumry, mwenzio kaingia na mtaji wa billions wewe nenda na ka million 5 kako ujionee maajabu.
 
Kuwa masikini inategemea unalima nini na una soko gani.
Still ardhi ukiitumia vizuri haikutupi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom