Vijana wenzangu hakika nawaambia kupitia hili nimejifunza....

ThaGreatman

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
708
1,465
Jana nimeamka asubuhi nikatafakari kwa kina sana juu ya maisha haya. Kubwa zaidi ni namna aliyewahi kuwa mpnz wangu aliponishambulia sana kuwa nimempa pesa kidogo,(aliniomba 150,000/= lakini mimi nilimpatia 100,000/=) kwa sababu nilikuwa najua kabisa kuwa ana pesa yake nyingine nyingi tu,kwa hiyo nikafanya jaribio la makusudi kuona reaction yake ingekuwaje baada ya kumpa kiasi pungufu na alichokiomba!

Lahaulaaa,lawama nilizopokea sasa....,"haujali shida zangu, najua unanikomoa, sawa,ila kumbuka mimi ni mke wako mtarajiwa,kama leo hii unashindwa kunisaidia 150k,sijui huko baadaye itakuwaje"

Nilipomaliza kusoma meseji nilivuta pumzi nikazifuta zote,nikajisemea moyoni,kuwa huyu hanifai kabisa....(na ndiyo ukawa mwisho wa mimi na yeye,japo mpaka sasa sijamwambia chochote)

Kilichofanya nije hapa ni baada ya kuamua kumtumia mama yangu mzazi kiasi cha sh.ELFU HAMSINI TU YA MATUMIZI,maombi niliyopokea hakika niliumia sana moyoni,sanaaa,kwamba mpenzi wangu nilimtumia sh.LAKI MOJA akaishia kunilaumu na kunisema sana,lakini mama yangu nimemtumia sh.50k shukrani alizotoa ni nzito sana! Hii imeniongezea hasira juu ya wanawake wasioridhika na kingi tunachowapatia,ilhali wazazi wetu wanapata kidogo na bado wanashukuru kweli kweli!

Haya ni maombi ya mama baada ya kutumiwa kiasi kidoogo sana cha pesa
Vijana wenzagu,tuwakumbukeni wazazi wetu wana baraka nyingi sana kwetu
 
Ebwaaaaneeeh.......

Jomba watu wanaonga mimi tu kumpa ten manzi ambaye sijamuoa naumia kwelikweli..... Sijui kwa vile maisha yangu nina uhakika na pugi.
Asante Mungu kunibariki sikosi vihela vidogodogo , zaidi sana nagawana na mama.
Hongera sana kwa kugawana na mama zaidi!
Mimi huyu nilikuwa ready kumhudumia kwa sababu psychologically nilishaanza kumfanya mke wangu wa siku chache sana zijazo,ila kumbe naye mpuuzi tu
 
Wanawake ndio walivyo ,niliwai toa promise ya kumsaidia pesa ya viatu ,kabla sijampa nikawa nimekutana nae tukawa tunapiga story mbili tatu akasema kuna rafiki yake aliomba pesa so nimsaidie then ata refund,haikuwa shida nikafanya hivyo ..changamoto ikaja sasa kupima je anathamini na wengine nikwambia sahivi sina pesa kuna mtu fulani nimemsaidia (rafiki yangu wa kike) so viatu tutununua next time “mtoto aliwaka kama moto wa kuchomoa betri”,hakumbuki yote ya nyuma uliyowai jitoa juu yake

Na ndio nikafunga report nae ..
 
Jana nimeamka asubuhi nikatafakari kwa kina sana juu ya maisha haya. Kubwa zaidi ni namna aliyewahi kuwa mpnz wangu aliponishambulia sana kuwa nimempa pesa kidogo,(aliniomba 150,000/= lakini mimi nilimpatia 100,000/=) kwa sababu nilikuwa najua kabisa kuwa ana pesa yake nyingine nyingi tu,kwa hiyo nikafanya jaribio la makusudi kuona reaction yake ingekuwaje baada ya kumpa kiasi pungufu na alichokiomba!

Lahaulaaa,lawama nilizopokea sasa....,"haujali shida zangu, najua unanikomoa, sawa,ila kumbuka mimi ni mke wako mtarajiwa,kama leo hii unashindwa kunisaidia 150k,sijui huko baadaye itakuwaje"

Nilipomaliza kusoma meseji nilivuta pumzi nikazifuta zote,nikajisemea moyoni,kuwa huyu hanifai kabisa....(na ndiyo ukawa mwisho wa mimi na yeye,japo mpaka sasa sijamwambia chochote)

Kilichofanya nije hapa ni baada ya kuamua kumtumia mama yangu mzazi kiasi cha sh.ELFU HAMSINI TU YA MATUMIZI,maombi niliyopokea hakika niliumia sana moyoni,sanaaa,kwamba mpenzi wangu nilimtumia sh.LAKI MOJA akaishia kunilaumu na kunisema sana,lakini mama yangu nimemtumia sh.50k shukrani alizotoa ni nzito sana! Hii imeniongezea hasira juu ya wanawake wasioridhika na kingi tunachowapatia,ilhali wazazi wetu wanapata kidogo na bado wanashukuru kweli kweli!

Haya ni maombi ya mama baada ya kutumiwa kiasi kidoogo sana cha pesa
Vijana wenzagu,tuwakumbukeni wazazi wetu wana baraka nyingi sana kwetu
View attachment 1206408
Nilishasema humu. Nikituma kwa mwanamke 50 basi na mama nitume 50. Kama siwezi kufanya hivyo basi jaribio hilo linishinde.

Hawana shukrani mbuzi hao. Mama zetu wanasali usiku kwa ajili yetu ila sio hao raia. Shenzi.
 
69 Reactions
Reply
Back
Top Bottom