Vijana wenzangu hakika nawaambia kupitia hili nimejifunza....

Na hiki ndicho kinachokera haswaaa
Lazma tulinganishe kwa sababu mzaz ndiyo katulea kwashida na raha, Mama yako ukimtumia 20000, anaonyesha kufurahi tulitegemea mzaz ndiyo alalamike akugombeze , lanik inakiwa kinyumechake madem ndiyo wana leta lawama.
 
Ni upuuzi wake tu,yaani hawezi kujua kuwa unapomsapoti ni kwa sababu ya moyo wa mapenzi na hisia za huruma,anaanza kudhani yeye ndo kika kitu na kila anachotaka lazima umpe in full package
Yeye si anawazaz na ndugu zake wao walimsaidia kwa kiwango kipi? Au yeye anaga marafiki
 
Kwani hujui kama mama ndio bora kuliko mpenzi wako. Mama hata ukimpa pesa mbili lazima ashukuru na kukuombea dua nyingi mno kwa Mungu ili uzidi kufanikiwa. Huyo ndio mama. Mpenzi wako ukimpa pesa nyingi ama kidogo huna unachoambulia zaidi ya maneno makali yakukuumiza. Hata umuhonge BOT nzima bado hazimtoshi. Hao ndio wanawaka sio wanawake.
Hahahaaa hata umhonge BoT nzima.....
 
Kwenye comment yako ya mwanzo umesema "Wanaume tuna fanya makosa kuwalinganisha wapenzi wetu na mama zetu hawawezi kuwa sawa na mama zetu katika ulimwengu wa vitendo".... Ukaenda mbele zaidi ukasema lazima tutambue "malezi ya mama zetu ni tofauti na ya wapenzi wetu"

Kwa tafsiri ya haraka tu ni kwamba ulikuwa una jaribu ku-rationalize tabia za kipuuzi za wanawake tulio nao leo hasa hii ya tamaa tamaa pamoja na kutokuwa na shukrani. Na tunatakiwa tuwachukulie easy tu kwa hizo tabia zao sababu zinatokana na malezi wanayopitia siku hizi.

Kutoka background tofauti sio sababu ya mtu kuniletea tabia mbovu mbovu za kishenzi na mimi nikachukulia easy sina muda wa kuanza kumpa behavioral trainings mtu mzima mwenye miaka 25+ nitamuacha atafute wa kufanana na yeye.
You are very right mate.

Hicho ndicho alichokuwa anakimaanisha huyo jamaa.
 
Na ndio inavyotakiwa..
Msipende kutoa hela hovyo....sio kazi yenu hiyo.
Kama mnatupenda,,zitunzeni kwa ajili ya mahari yetu.
Asante sana mama.

Ndio maana nampigia debe @SHIMBAYABUYENZE hili akupate uje kwenye koo zetu huku maana wanawake adimu kama wewe tunawahitaji sana.

Come to us Anne
 
Asante sana mama.

Ndio maana nampigia debe @SHIMBAYABUYENZE hili akupate uje kwenye koo zetu huku maana wanawake adimu kama wewe tunawahitaji sana.

Come to us Anne
Mimi sitaki mangumi..
Hicho tu ndicho nakiogopa kwenu
 
Jana nimeamka asubuhi nikatafakari kwa kina sana juu ya maisha haya. Kubwa zaidi ni namna aliyewahi kuwa mpnz wangu aliponishambulia sana kuwa nimempa pesa kidogo,(aliniomba 150,000/= lakini mimi nilimpatia 100,000/=) kwa sababu nilikuwa najua kabisa kuwa ana pesa yake nyingine nyingi tu,kwa hiyo nikafanya jaribio la makusudi kuona reaction yake ingekuwaje baada ya kumpa kiasi pungufu na alichokiomba!

Lahaulaaa,lawama nilizopokea sasa....,"haujali shida zangu, najua unanikomoa, sawa,ila kumbuka mimi ni mke wako mtarajiwa,kama leo hii unashindwa kunisaidia 150k,sijui huko baadaye itakuwaje"

Nilipomaliza kusoma meseji nilivuta pumzi nikazifuta zote,nikajisemea moyoni,kuwa huyu hanifai kabisa....(na ndiyo ukawa mwisho wa mimi na yeye,japo mpaka sasa sijamwambia chochote)

Kilichofanya nije hapa ni baada ya kuamua kumtumia mama yangu mzazi kiasi cha sh.ELFU HAMSINI TU YA MATUMIZI,maombi niliyopokea hakika niliumia sana moyoni,sanaaa,kwamba mpenzi wangu nilimtumia sh.LAKI MOJA akaishia kunilaumu na kunisema sana,lakini mama yangu nimemtumia sh.50k shukrani alizotoa ni nzito sana! Hii imeniongezea hasira juu ya wanawake wasioridhika na kingi tunachowapatia,ilhali wazazi wetu wanapata kidogo na bado wanashukuru kweli kweli!

Haya ni maombi ya mama baada ya kutumiwa kiasi kidoogo sana cha pesa
Vijana wenzagu,tuwakumbukeni wazazi wetu wana baraka nyingi sana kwetu
View attachment 1206408
Mkuu hakika umenigusa, tena sana tu
 
Back
Top Bottom