VIJANA WENZANGU (25 - 30 YRS) (ME & KE) TULIOAMUA KUINGIA KATIKA COMMITMENT (UCHUMBA/NDOA)

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
451
500
Nyakati zinabadirika sana; misimamo, tamaduni na mitindo ya maisha sio kama vile ilivyokuwa miaka 50 iliyopita.

Kama nitakuwa sijakosea, naamini zaidi ya 85% ya wajomba na shangazi zetu, baba na mama zetu wengi waliingia katika ndoa wakiwa chini ya umri wa miaka 30. Na pia naamini zaidi ya 75% waliweza kuoa au kuolewa wakiwa na umri wa miaka 25 au chini zaidi.

Currently, natumaini mtakubaliana na mimi kuwa hizi statistics zimebadilika sana na kwa kasi. Umri wa vijana kuingia katika mahusiano ya ndoa umeongozeka, na kwa maono yangu naona kuwa wastani wa umri wa vijana kufanya committed relationship ni kuanzia miaka 29-35.

Kuna sababu tofauti nilizozisikia kupelekea mabadiliko haya:

1. muda mrefu wa elimu, muda mrefu hadi kupata kazi.

2. kujipanga kiuchumi na umiliki wa mali.

3. kupoteza tumaini juu ya mapenzi ya dhati, kutokana na kudolola kwa maadili na ongezeko la utapeli wa mapenzi.

4. uhitaji wa ku-enjoy nyakati za maisha, coz ya fikra kuwa ndoa au uchumba unafinya uhuru wa kuenjoy starehe, umauzi binafsi..etc

na nyingine zaidi....

Ila tofauti na changamoto hizo zote na mabadiliko katika generation yetu, bado kuna tumaini. Usiogope kuoa au kuolewa ukiwa una umri chini ya miaka 30.

Muda mwingine hauhitaji kusubiri mtu special katika maisha yako, au kusubiri muda special.. unachotakiwa ni kumpata the right person kwa ajili yako, na kiukweli hizi special moments haziji tu.. unatakiwa kutengeneza hizo special moments.

Kama katika huu umri; fursa ipo, umejipanga kisaikolijia, umepata mtu unaona yuko sawa na yeye yuko tayari na una uwezo wa kumudu maisha ya ndoa, na amekukubali kwa hali yako then usiangalie umri wako, usijione chalii, usiangalie wengine wameamuaje, unatakiwa uamue yako.

DO NOT HESITATE, GO FOR IT.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom