Vijana wengi wanakosa kazi kutokana na kutokuwa au kutunza contacts zao

Tulimumu

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
13,832
2,000
Maelfu ya vijana na wahitimu mbalimbali wapo mitaani hawana ajira. Wengi wamesambaza barua za maombi ya kazi sehemu mbali mbali na sasa wanasubiri majibu.

Hivi karibuni tuliita waombaji 10 tulioona wako vizuri kwaajili ya kuwafanyia usaili. Cha ajabu kila muombaji aliyepigiwa alikuwa hapatikani au unaambiwa namba hiyo haipo. Tulijaribu kwa siku 2 na tukatuma na ujumbe wa maandishi angalau tukitegemea ndani ya saa 24 ujumbe utapokelewa kwa maana kama mtu alizima simu ataupata. Ni mmoja tu ndiye alipatikana. Ajabu ni kuwa unakuta mtu ameandija namba 3 katika CV yake lakini ukipiga zote hazipatikani. Emails nazo hawafungui kwa wakati.

Ushauri wangu ni kuwa namba za simu unazoweka kwenye nyaraka muhimu kama CV, bank nk zinatakiwa ziwe hai muda wote. Nimefikiria tu kama kati ya 10 tulimpata mmoja je ni waombaji wangapi wanakosa kazi wanapoitwa katika taasisi na ofisi mbali mbali kwa kutopatikana kwa simu? Kama simu imepotea su kuibiwa rejesha namba. Wengine wanatumia namba za watu wengine kwenye CV ukipiga unaambiwa mhusika hayupo alitumia namba isiyo yake. Ndipo unajiuliza hivi mhitimu wa chuo kikuu amekosa hata simu ya kitochi hadi atumie namba ya mwingine?

Kuweni makini waombaji wa kazi mnapoteza nafasi kwa kwa kukosa umakini

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom