Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 29,357
- 40,245
Wanatakiwa waelewe, kampuni binafsi inahitaji mtu smati na aliyeiva kweli kweli, ili kuendelea kubaki kwenye nafasi yako; kwa sababu lengo la makampuni ni kutengeneza faida na si hasara. Sasa utakuta vijana:-
- Wengi hawajimudu kwa kile walichokisomea au wanachokielezea wanaweza kukifanya.
- Wakiingia 'field' wanashindwa ku-perform kazi inavyotakiwa na kuleta hasara kwenye makampuni
- Wengi wanauelewa mdogo kuhusu hupatikanaji wa fedha za uendeshaji katika makampuni
- Kuongeza mauzo au faida maeneo wanapoajiriwa kwa matazamio (probation)
- Kusaidia kampuni katika majanga ya kisheria yanayoweza kusababisha upotevu wa fedha
- Kubuni namna kampuni inavyoweza kupata malighafi kwa gharama nafuu
- Uwezo wa kusimamia kampuni kwa uadilifu na uaminifu mkubwa bila kupata hasara