Vijana wengi wanakosa ajira kwa sababu ni 'incompetent'

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,174
39,933
Wanatakiwa waelewe, kampuni binafsi inahitaji mtu smati na aliyeiva kweli kweli, ili kuendelea kubaki kwenye nafasi yako; kwa sababu lengo la makampuni ni kutengeneza faida na si hasara. Sasa utakuta vijana:-
  • Wengi hawajimudu kwa kile walichokisomea au wanachokielezea wanaweza kukifanya.
  • Wakiingia 'field' wanashindwa ku-perform kazi inavyotakiwa na kuleta hasara kwenye makampuni
  • Wengi wanauelewa mdogo kuhusu hupatikanaji wa fedha za uendeshaji katika makampuni
Vijana wanatakiwa kujua na kujitahidi katika:-
  • Kuongeza mauzo au faida maeneo wanapoajiriwa kwa matazamio (probation)
  • Kusaidia kampuni katika majanga ya kisheria yanayoweza kusababisha upotevu wa fedha
  • Kubuni namna kampuni inavyoweza kupata malighafi kwa gharama nafuu
  • Uwezo wa kusimamia kampuni kwa uadilifu na uaminifu mkubwa bila kupata hasara
Haya, pambaneni vijana.
 
Back
Top Bottom