Vijana wengi wanafuata mkumbo na kuchukulia kuwa Mpinzani ni fasheni na kwenda na wakati

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,070
3,705
Hapo vipi!

Binafsi mwaka 2019 nilikuwa mwanachama wa chama fulani cha upinzani, ila nilikaa nikatafakari na nikachunguza hicho chama mbadala nikagundua ni kitakuja kuwa ni chama cha ovyo kitakachokuwa kama kampuni ya watu fulani wanaotoka katika kabila fulani. Pima nimepima sera zake nikagundua ni za kilaghai na za hovyo kupitiliza.

Mfano mdogo tu wa sera zake, eti watabinafsisha na kuchukulia rasilimali ya nchi kama madini n.k mkopo wa fedha kutoka kwa mabeberu au bank ya Dunia.

Tafiti zinaonyesha nchi 14 zilizochukua mkopo kwa kutumia rasilimali ya nchi zao na nchi 10 kati ya nchi kumi nne zilizotumia sera hii zilishindwa kurudisha fedha atimaye rasilimali za nchi hizo zikakaliwa na mataifa mengine.

Wanazo Sera nyingi ambazo ukiweka kwenye minzani unagundua kabisa hapa huu ni usanii kama usanii mwingine.

Mfano mwingine, anasema atatoa bima ya afya kwa kila Mtanzania just imagine Marekani taifa kubwa limeshindwa kufanya hivyo na ina uchumi mkubwa Duniani. Alafu leo mtu anasimama jukwaani anatuaaminisha yakwamba nchi kama Tanzania yenya uchumi mdogo hivi itaweza kufanya hivi na watu wanaamini nakushangilia.

Hawa wanasiasa hawaogopi kudangaanya mchana peupe kwasababau wanajua Watanzania wengi wanafikiri under evarage, hivyo wanatumia hii hali kama daraja.

Nimejaribu kuhojiana na vijana wengi wanaojiita wanamabadiliko ila nimegundua kitu kimoja, wengi wao wapo upinzani kwa kufuata mkumbo na wakiamini yakwamba nikwenda na wakati. Ukimuuliza sera gani imemsababisha achague upinzani anaanza kukuambia habari za uhuru, ukimuuliza umenyang'anywa uhuru gani.

Hana sababu za msingi zaidi ya kusem mara vyombo vya habari vimenyimwa uhuru. Unamkuta ni dereva bado anafanya kazi zake kwa uhuru pasipo tatizo lolote na anapata habari zote zinazoendea nchini.

Moja kwa moja unaona huyu mtu anafuata mkumbo pasipo kupima sera za chama husika.
 
Back
Top Bottom