Vijana wengi wa CCM hawajauishi mfumo wa chama kimoja wanausikia tu ndio maana wanautamani hata sasa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Zama hizi siasa ni ajira wala siyo mapenzi au itikadi kama ilivyokuwa enzi za mwalimu Nyerere. Ndio utaona hata Lowassa wakati anasaka ajira ya urais ilimlazimu kwenda Chadema bila kujali itikadi wala mapenzi.

Ambacho nakiona wapinzani kwa wingi wao wakiisha hamia wote CCM ndipo athari za zoezi hilo zitakapoonekana na hapo vijana hawa hawa wa CCM wataanza kuutamani mfumo wa vyama vingi.

Mfumo wa chama kimoja ulikuwa ni mzuri kwa wakati wake lakini kwa sasa umepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo duniani kote. Vijana wa CCM kazeni buti vinginevyo mtaujenga upinzani wa ndani ya chama na huo ndio unatisha afadhali hata ya huu wa akina Mbowe. Upinzani ni fikra siyo taasisi na mtu mwenye fikra za kipinzani huziondoi kwa dakika moja.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
 
Asee Mkuu huyu siyo wewe, 😂
Umeongea ukweli..
 
vijana wengi wa ccm akili hawana.Hata vyuoni tumewaona.wanapenda cheap cheap politics.Hakuna hoja.Fikiria mfano mtu kama Bashite eti ndo vijana.

Hata itikadi za vyama vyao hawazijui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zama hizi siasa ni ajira wala siyo mapenzi au itikadi kama ilivyokuwa enzi za mwalimu Nyerere. Ndio utaona hata Lowassa wakati anasaka ajira ya urais ilimlazimu kwenda Chadema bila kujali itikadi wala mapenzi.

Ambacho nakiona wapinzani kwa wingi wao wakiisha hamia wote CCM ndipo athari za zoezi hilo zitakapoonekana na hapo vijana hawa hawa wa CCM wataanza kuutamani mfumo wa vyama vingi.

Mfumo wa chama kimoja ulikuwa ni mzuri kwa wakati wake lakini kwa sasa umepitwa na wakati kutokana na mabadiliko ya kimaendeleo duniani kote. Vijana wa CCM kazeni buti vinginevyo mtaujenga upinzani wa ndani ya chama na huo ndio unatisha afadhali hata ya huu wa akina Mbowe. Upinzani ni fikra siyo taasisi na mtu mwenye fikra za kipinzani huziondoi kwa dakika moja.

Niendelee kuwatakia Kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!
Leo mwezi umekaa vzr mkuu
 
Back
Top Bottom