toplemon
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 4,581
- 4,631
Vijana wa kiume na wa kike sasa hivi wanajichubua kwasababu ya ubaguzi na upendeleo unaokuwepo ktk jamii
Mfano unakuta mtoto anakosea mzazi anamwambia kwamba amefanya hivyo na ndo maana tu mungu alimuumba mweusi
Mweusi kama chungu cha mchawi
Wewe ni mweusi hadi huko rohoni kwangu
Una uzuri gani wewe mweusi kama mkaa!
Tatizo wewe ni mweusi sana yaani mbayaa
Ila jamaa wewe ni mweusi aisee sijui huko kwenu ulitokea wapi
Wazazi wako sisi ni weupe hata sijui ilikuaje tukakuzaa ww ukawa mweusi kuliko watoto wote
Wazazi na jamii kuonyesha mapenzi kwa watoto au watu weupe huku wale weusi wakiachwa tu unakuta mzazi anampenda mtoto mweupe na kuonyesha mapenzi ya waziwazi dhidi ya yule mweusi.
Jamii ya kitanzania inaongoza kwa kuwabagua watu weusi nazungumzia mtu ambaye ni mweusi yaani cheusi mangala
Huko mashuleni ndo usiseme na utani wa hapa na pale, ukigombana tu na mtu cha kwanza anaanza kukushambulia na ngozi yako kwanza kwenda huko ndo maana wewe ni mweusi, peleka weusi wako huko, lione leusi.
Mwishoni kaka wa watu au dada wa watu anaanza kujichubua tu, ubaguzi unauma sana asikwambie mtu bora hata kuuawa kuliko kubaguliwa au maneno ya ubaguzi