Vijana wengi CCM ni wanafiki, wenye tamaa na wasio na Uzalendo

mngony

JF-Expert Member
Jul 27, 2012
5,193
6,381
Ni vile tu ni kwa sababu ni vijana ni sehemu ya Chama, lakini naamini Mama hana jinsi lakini sote tunafahamu kuwa asilimia 90 ya vijana wa CCM ni wanafki, wamejawa na tamaa ya maisha huku wakiwa wameweka maslahi binafsi kuliko Uzalendo.

Tukichukulia mfano wa Wakuu wa Wilaya na Mikoa kwa miaka mitano iliyopota vijana ndio wamekuwa mfano mbaya wa viongozi waliokosa heshima na hekima. Wamekuwa ni watu wanaosemwa, kulalamikiwa na kushutumiwa kuanzia kuonea watu, kuvunja sheria na kujibambikia mali. Watu kama Hapi, Makonda, Kihongosi, Sabaya ni mfano mizuri kabisa. Hawa hawakuwa na ajenda ya kuleta maendeleo kwao kupambana na upinzani ndio walioma ndio majukumu yao. Walifikia hatua kuwadharau na kuwatukana Wazee

Mama yetu alivyoingia, humu mitandaoni alikuwa akitetewa na vijana wasio na vyama na hata baadhi ya wale walio katika upinzani. Kwao waliona Taifa mbele na wakatamani utulivu na ustawi wa amani kwanza kama Taifa kisha mengine tayakuja baadae.

Leo baada ya Mama kuahidi Mkeka uliosheheni vijana ndio unaona vijana wa CCM kama wakina Mwakibinga wanaanzisha nyuzi za kumsifia Mama.

Vijana wa CCM mmekiangusha sana Chama na Taifa kwa ujumla. Huwezi fananisha na vijana wa upinzani badilikeni
 
Chadema mnawashwa SI bure
Tena Ni kalio
Nilitamani nibishe anachosema ila kama vijana wa CCM ndio nyie? Haaaa yuko sahihi. Kwahiyo ndo umemjibu hivyo? Halafu kila anayetoa mawazo mbadala ni CHADEMA? Basi CHADEMA wana akili sana.
 
Endeleeni kujichanganya,
Mtakuta PDF ya DC,DAS,DED imejaa vijana toka CHAUMA,NCCR,UPD,CUF,CHADEMA,ACT,TLP,CCM kwa mbali.
NDUGAI ALIWAMBIA MAMA HATABIRIKI
 
Endeleeni kujichanganya,
Mtakuta PDF ya DC,DAS,DED imejaa vijana toka CHAUMA,NCCR,UPD,CUF,CHADEMA,ACT,TLP,CCM kwa mbali.
NDUGAI ALIWAMBIA MAMA HATABIRIKI
Kama wapo ambao Mama ataoka wanafaa awachukue tu sisi sote ni Watanzania
 
Back
Top Bottom