Vijana Watafuta Kadi za Uanachama wa CCM Kama Dhahabu

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,147
9,607
Ndugu zangu watanzania,

Vijana Mitaani wanazitafuta kadi za CCM Kama madini ya Dhahabu,wanapita na kuwatafuta makatibu Tawi wa CCM kwa bidii kubwa Sana ili waweze kupewa kadi na kujiunga na CCM na kuweza kushirikiana na Wana CCM wenzao katika ujenzi wa Taifa letu.

Hii Ni baada ya serikali ya CCM kuleta matumaini kwa vijana,kuleta Tabasamu Katika maisha ya vijana,kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao za kielimu na kimaisha,Hii Ni Baada ya serikali ya CCM kuwekeza mabillioni ya Fedha katika miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo imetoa fursa za ajira kwa vijana,hii Ni baada ya kuona juhudi za serikali katika kuwatatulia kero zao ambazo zilikuwa kizingiti katika ukuaji wao wa kiuchumi na kujitegemea na kuondokana na Hali ya utegemezi.

Hii Ni Baada ya kuona Sera na ajenda za ilani ya CCM na mikakati ya serikali ya CCM ikitoa kipaombele kwa vijana ambao ndio kundi kubwa hapa nchini,Hii Ni baada ya kuona serikali ya CCM ikiwatengenezea njia za kiuchumi kusonga mbele,Hii Ni Baada ya kuona serikali ya CCM ikiwa karibu yao ,kuwajibu maswali Yao, kuwatumikia,kuwasikiliza na kuwapa nafasi ya kueleza changamoto zao na kuwapa matumaini,Hii Ni Baada ya kuona kesho yao ni njema, Hii Ni Baada ya kuwa na uhakika wa kutimiza malengo Yao,Hii ni baada ya kuona jicho la serikali ya CCM lipo juu Yao,Hii Ni Baada ya serikali ya CCM kupitia halmashauri kuwapatia mikopo ili kuwawezesha kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao na kukuza mitaji yao.

sasa wameamua kujiunga CCM kuunga juhudi za serikali ya CCM chini ya Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania,wameamua wawe ndani ya CCM ili kutoa mawazo yao chanya ,wameamua wawe CCM kwa kuwa ndio chama pekee kilichoonyesha kwa vitendo kuwa na uchungu na maisha yao na kuumia pale kinaapoona vijana wakihangaika au kuhangaishwa na mtu yeyote yule,

wameamua kufanya hivyo ili washirikiane na Rais Samia aliyeonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa wa kiuongozi,wanataka wawe sehemu ya wazalendo wa Taifa letu,Sasa vijana wanaonaa fahari kuwa sehemu ya CCM na wanajitambulisha bila hofu Wala wasiwasi wawapo katiKati ya watu kuwa Ni wanaccm,Sasa vijana wanaitetea CCM na serikali Yake kwa hoja kutokana na kazi kubwa za kimaendeleo zilizofanyika na kutekelezwa kwa umakini.

kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
 
Hao wanatafuta posho tu za 10000-30000..kadi inawezaje kukupa ajira acha ujinga mtoa mada
Serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia imeweka mazingira mazuri kwa vijana kuweza kujiajiri kwa kutoa na kuwapa mitaji kupitia halmashauri zao Inayowasaidia kuinuka kiuchumi na kuondokana na utegemezi.

Pia serikali ya CCM imeboresha secta binafsi na kuifanya kutengeneza fursa nyingi Sana za ajira kwa vijana,lakini pia serikali imetoa ajira nyingi Sana za ajira kupitia miradi mbalimbali inayojengwa kila Kona ya nchi yetu pamoja na kutoa ajira za moja kwa moja serikalini
 
Hahahah Mimi ninayo ,nilijiandikisha mwaka 2018 nikaja pewa mwaka Jana dodoma walipokuwa na mkutano wao ule mkuu,niliamua kujiunga huko ili nipate cheo kazini,manake cheo nachokihitaji kwenye fani yangu kinategemea Sana uwe mwanaCCM ingawa hawasemi dairekti.Sema bado sijakipata manake nimekuja fanya kazi kwa kina ngosha wakaniwekea kauzibe kisa ni mwanamke,hii nchi bana🤔ila Mungu yupo ataniona tu one day🙏
 
Mtajuana wenyewe huko ccm me ilimradi nishapata ajira yangu serikalini basi fresh nakula hizo mamilioni zenu ila naonea huruma sana wakazi huko site napoenda wengi ni ccm ila choka mbaya
 
Hahahah Mimi ninayo ,nilijiandikisha mwaka 2018 nikaja pewa mwaka Jana dodoma walipokuwa na mkutano wao ule mkuu,niliamua kujiunga huko ili nipate cheo kazini,manake cheo nachokihitaji kwenye fani yangu kinategemea Sana uwe mwanaCCM ingawa hawasemi dairekti.Sema bado sijakipata manake nimekuja fanya kazi kwa kina ngosha wakaniwekea kauzibe kisa ni mwanamke,hii nchi bana🤔ila Mungu yupo ataniona tu one day🙏
Usijiulize Tanzania au CCM au serikali itakufanyia Nini Bali jiulize utaifanyia Nini Tanzania yetu, Fanya kazi kwa bidii ,onyesha matokeo chanya katika nafasi uliyonayo kwa Sasa,jibidishe kuwatumikia na kuwahudumia watanzania wanaofika kwako kuhitaji huduma kulingana na nafasi uliyopo kwa upendo unyenyekevu busara hekima na ukarimu,usiwe mjivuni na mwenye kiburi ,jishushe na kuwa muungwana.

Ukifanya hayo naamini utaonekana na kwa uweza wa MWENYEZI MUNGU utapanda cheo kazini kwako, Usimtegemee mtu au mwanadamu kupanda cheo maana amelaaniwa yule amtegemeaye mwanadamu,

Jiulize ikiwa ukamtegemea mtu kupanda cheo,vipi siku mtu huyo akifariki? Au mkakosana? Au akahitaji vitu vinavyoshusha utu wako au kukuvunjia heshima au kutetelesha ndoa yako au kukufanya ukasaliti ndoa yako na kuishia kuambukizwa Hadi maradhi na kuyapeleka katika ndoa yako au kwa mpenzi wako?

Uongozi unatoka kwa Mungu ,hivyo usiwe na haraka ya kutaka madaraka na vyeo, acha vyeo vije kutokana na uwezo wako wa kiuongozi na kiutendaji, Endelea kumtanguliza na kumtegemea Mwenyezi MUNGU katika kazi zako zote,mwombe Mungu akupe maarifa na njia za kazi ufanyazo ili zikawe zenye kufanikiwa na kukubalika machoni pa watu.

Zingatia ushauri wangu utakuja kunishukuru siku moja.
 
Wacha?! Na hazipatokani? That's more than serious. Wamegundua nini kwenye hizo kadi?
Wamegundua kuwa CCM ndio chama chenye uwezo wa kuliongoza Taifa letu na kulinda Rasilimali zetu , wametambua kuwa Ni CCM pekee yenye kuweza kuwasaidia kutimiza Ndoto zao,wameelewa kuwa ni CCM pekee yenye uchungu na maisha yao,wametambua ya kuwa Ni CCM pekee yenye muelekeo unaoeleweka na yenye mipango mikakati ya kuwainua kiuchumi
 
Usijiulize Tanzania au CCM au serikali itakufanyia Nini Bali jiulize utaifanyia Nini Tanzania yetu, Fanya kazi kwa bidii ,onyesha matokeo chanya katika nafasi uliyonayo kwa Sasa,jibidishe kuwatumikia na kuwahudumia watanzania wanaofika kwako kuhitaji huduma kulingana na nafasi uliyopo kwa upendo unyenyekevu busara hekima na ukarimu,usiwe mjivuni na mwenye kiburi ,jishushe na kuwa muungwana.

Ukifanya hayo naamini utaonekana na kwa uweza wa MWENYEZI MUNGU utapanda cheo kazini kwako, Usimtegemee mtu au mwanadamu kupanda cheo maana amelaaniwa yule amtegemeaye mwanadamu,

Jiulize ikiwa ukamtegemea mtu kupanda cheo,vipi siku mtu huyo akifariki? Au mkakosana? Au akahitaji vitu vinavyoshusha utu wako au kukuvunjia heshima au kutetelesha ndoa yako au kukufanya ukasaliti ndoa yako na kuishia kuambukizwa Hadi maradhi na kuyapeleka katika ndoa yako au kwa mpenzi wako?

Uongozi unatoka kwa Mungu ,hivyo usiwe na haraka ya kutaka madaraka na vyeo, acha vyeo vije kutokana na uwezo wako wa kiuongozi na kiutendaji, Endelea kumtanguliza na kumtegemea Mwenyezi MUNGU katika kazi zako zote,mwombe Mungu akupe maarifa na njia za kazi ufanyazo ili zikawe zenye kufanikiwa na kukubalika machoni pa watu.

Zingatia ushauri wangu utakuja kunishukuru siku moja.

Ukiona kijana anachukua kadi ya chama cha majizi ya kura, ujue sio kwa sababu za kiitikadi, bali kuna fursa anaitaka. Maana sasa hivi ili upate upendeleo inabidi uigize kuwa ni mwanachama wa chama cha majizi ya kura.
 
Ndugu zangu watanzania,

Vijana Mitaani wanazitafuta kadi za CCM Kama madini ya Dhahabu,wanapita na kuwatafuta makatibu Tawi wa CCM kwa bidii kubwa Sana ili waweze kupewa kadi na kujiunga na CCM na kuweza kushirikiana na Wana CCM wenzao katika ujenzi wa Taifa letu.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Naunga mkono hoja, na sio vijana tuu hata Wazee pia wapo!. Kwanini sipati kadi ya uanachama wa CCM?
P
 
Ukiona kijana anachukua kadi ya chama cha majizi ya kura, ujue sio kwa sababu za kiitikadi, bali kuna fursa anaitaka. Maana sasa hivi ili upate upendeleo inabidi uigize kuwa ni mwanachama wa chama cha majizi ya kura.
Sera Bora ,ajenda zenye kugusa maisha ya vijana,ilani nzuri ya CCM na safu Bora na yenye kuleta matumaini kwa vijana imekuwa Chachi ya vijana wengi kutafuta kadi za CCM Kama Dhahabu ili kuunga juhudi za serikali ya CCM, vijana wameridhishwa na kuvutiwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia.

Tofauti na vyama Kama chadema walikojaa wababaishaji na watu waliokosa muelekeo ,wasioweza hata kujiongoza na waliokosa matumaini
 
CHAMA CHA MAPINDUZI kimefanya mabadiliko chanya na makubwa mno kwa kila nyanja,kwa upande wetu wakulima hatuna neno, Go ahead mama SAMIA. Majanga ya mvua za upepo na mawe ni nje ya uwezo wa kibinadamu,tukosapo msimu huu wa kilimo tunaamini msimu ujao tutapata kwa kuwa masoko ya mazao yetu yamekaa sawa.
 
Sera Bora ,ajenda zenye kugusa maisha ya vijana,ilani nzuri ya CCM na safu Bora na yenye kuleta matumaini kwa vijana imekuwa Chachi ya vijana wengi kutafuta kadi za CCM Kama Dhahabu ili kuunga juhudi za serikali ya CCM, vijana wameridhishwa na kuvutiwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM chini ya uongozi shupavu na madhubuti wa Rais Samia.

Tofauti na vyama Kama chadema walikojaa wababaishaji na watu waliokosa muelekeo ,wasioweza hata kujiongoza na waliokosa matumaini

Sera za kusema mtajenga madarasa, hayo hata wanaoingia madarakani kwa kupindua nchi wanafanya. Chama cha majizi ya kura mnakwama wapi?
 
2016 nilichukua kadi ya CCM baada ya kuhitimu mahali fulani na tukatuma PDF ya majina ya waliochukua kadi vyuo mbalimbali ajabu nikuwa wote tuliochukua huo upuuzi mpaka leo hakuna aliyepata ajira.

Ukiona vijana wanachukua kadi za CCM basi jua Kuna fursa na sio wanaitaka CCM.
 
Ndugu zangu watanzania,

Vijana Mitaani wanazitafuta kadi za CCM Kama madini ya Dhahabu,wanapita na kuwatafuta makatibu Tawi wa CCM kwa bidii kubwa Sana ili waweze kupewa kadi na kujiunga na CCM na kuweza kushirikiana na Wana CCM wenzao katika ujenzi wa Taifa letu.

Hii Ni baada ya serikali ya CCM kuleta matumaini kwa vijana,kuleta Tabasamu Katika maisha ya vijana,kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao za kielimu na kimaisha,Hii Ni Baada ya serikali ya CCM kuwekeza mabillioni ya Fedha katika miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo imetoa fursa za ajira kwa vijana,hii Ni baada ya kuona juhudi za serikali katika kuwatatulia kero zao ambazo zilikuwa kizingiti katika ukuaji wao wa kiuchumi na kujitegemea na kuondokana na Hali ya utegemezi.

Hii Ni Baada ya kuona Sera na ajenda za ilani ya CCM na mikakati ya serikali ya CCM ikitoa kipaombele kwa vijana ambao ndio kundi kubwa hapa nchini,Hii Ni baada ya kuona serikali ya CCM ikiwatengenezea njia za kiuchumi kusonga mbele,Hii Ni Baada ya kuona serikali ya CCM ikiwa karibu yao ,kuwajibu maswali Yao, kuwatumikia,kuwasikiliza na kuwapa nafasi ya kueleza changamoto zao na kuwapa matumaini,Hii Ni Baada ya kuona kesho yao ni njema, Hii Ni Baada ya kuwa na uhakika wa kutimiza malengo Yao,Hii ni baada ya kuona jicho la serikali ya CCM lipo juu Yao,Hii Ni Baada ya serikali ya CCM kupitia halmashauri kuwapatia mikopo ili kuwawezesha kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao na kukuza mitaji yao.

sasa wameamua kujiunga CCM kuunga juhudi za serikali ya CCM chini ya Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani kipenzi Cha watanzania,wameamua wawe ndani ya CCM ili kutoa mawazo yao chanya ,wameamua wawe CCM kwa kuwa ndio chama pekee kilichoonyesha kwa vitendo kuwa na uchungu na maisha yao na kuumia pale kinaapoona vijana wakihangaika au kuhangaishwa na mtu yeyote yule,

wameamua kufanya hivyo ili washirikiane na Rais Samia aliyeonyesha ushupavu na umadhubuti mkubwa wa kiuongozi,wanataka wawe sehemu ya wazalendo wa Taifa letu,Sasa vijana wanaonaa fahari kuwa sehemu ya CCM na wanajitambulisha bila hofu Wala wasiwasi wawapo katiKati ya watu kuwa Ni wanaccm,Sasa vijana wanaitetea CCM na serikali Yake kwa hoja kutokana na kazi kubwa za kimaendeleo zilizofanyika na kutekelezwa kwa umakini.

kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627
Hao vijana watakuwa hawana akili bila shaka.

Kabisaa wapoteze muda wao kutafuta kadi za ccm kama dhahabu, badala ya kupambana na haya maisha magumu mtaani, yaliyosababishwa na hiyo serikali ya ccm!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom