Vijana wasio na ajira wajiajiri katika sekta binafsi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wasio na ajira wajiajiri katika sekta binafsi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwakajilae, Dec 15, 2011.

 1. m

  mwakajilae Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwanza hakuna suala linalo udhi kama suala la kuiga vitu pasipo kushirikisha akili,hasa hili linapotokea kwa watu wenye akili timamu.

  Hoja ya kisera kwa kuwataka vijana wanaozidi kumiminika mtaani kwa kuhitimu masomo yao kutoka vyuoni kwamba serikali haina uwezo wa kuwaajiri hivyo kuwataka wajihusishe na ajira binafsi au kwa tafsiri pana kwamba wajiajiri kwenye mifumo isiyo rasimi ya kiajira ni janga la kifikra linalo kua kwa kasi.

  Kwani wenzetu wamagharibi wanavyosema kwamba vijana wao wajiajiri ni kutokana na sababu za wazi na kweli kwamba kutoka Wizarani au Ikulu mpaka ngazi ya Serikali ya mtaa,walio shikilia nafasi hizo ni watu wenye sifa za kuajiriwa kwa maana ya Elimu,uwezo na Ujuzi wa kufanya kazi hizo,kwa wenzetu hutaskia nafasi tano zina kaimiwa na mtu mmoja!!!hivyo wanaongeza uwajibikaji kwa kutoa huduma zilizobora kwa Taifa lao,lakini pia uchumi unakua kwa kasi kwasababu ya ongezeko la uzalishaji unaotokana na umakini na uwajibikaji.

  Ukirudi Tanzania unaambiwa vijana wajiajiri,wakati kutoka Ikulu,wizarani mpaka ngazi ya mtaa hakuna raslimali watu[wafanya kazi] hata kama wapo ujue wengi wao hawanasifa za kushika nafasi walizo nazo kwa maana ya kwamba wapo kiuzoefu,ni mashuhuda wa Muungano wa Tanu na Asp,au tamko la Azimio la Arusha,hata kama anasifa ujue anashikilia nafasi tano ofisini kwako.

  Kwa wanaobisha wafanye utafiti wa kukagua ofisi zetu zote kuanzia ikulu mpaka serikali ya mtaa,wawabaini wafanyakazi idadi yao,majukumu yao na sifa zao kwa kila idara ikiwa ni pamoja na umri wao.

  Pia wenzetu Magharibi kwa huyu kijana anaye toka chuoni halafu ajira ni tatizo,wana mifumo ya kuwawezesha kwa sera zinazofanya kazi kama mikopo ili wajiajiri,mikataba ya ajira pamoja na posho maalum za kujikimu ambazo kwa Tanzania wanazitafuna wabunge,kwa wenzetu zinaelekezwa katika kupunguza ugumu wa maisha kwa vijana wasio na ajira pamoja na wazee.

  Tanzania unasema wakajiajiri wakati hakuna uhalali wa kisiasa na kisera kwa kuongeza vijana wa kujiajiri kukiwa hakuna sababu ya msingi ya kufanya hivyo kwa Taifa changa lenye kila aina ya fursa za kuboresha huduma kwa jamii katika kila idara,ambapo wasomi waliopo bado hawatoshelezi kwani hata Teknolojia inayosemekana kwamba haihitaji watu mia mbili ofisini bado hatujaifikia.

  Cha kuumiza zaidi hata wabunge wanashindwa ubunifu kwa kutumia zile fedha za majimbo ambazo zipo chini ya uthibiti wao kwa kuweza kuibulia miradi na kuwaajiri vijana,sioni sababu yoyote ile inayowafanya washindwe kuwaajiri vijana majimboni kwao kwa kubuni miradi itakayo hitaji raslimali watu.

  Kila suala la ajabu hutendeka Tanzania tuu siyo mahara pengine duniani kwa kupenda majibu mepesi kwa hoja nzito,baadala ya kuumiza kichwa mara nyingi tunapenda majibu waliyowahi kuyato watu,hatupendi kufikiri zidi,tunachukia mawazo mapya yaliyo tofauti na ya jana.Tunataka kila mmoja aenzi ya jana siyo aje na mapya yaliyobora.

  Mungu ibariki Tanzania.
   
Loading...