Vijana wasio na ajira vs wakuu wa mikoa

meku7

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
375
266
Mh Rais ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa akiwaapisha leo ikulu..kuhakikisha wanawalazimisha vijana kufanya kazi,, ni marufuku kucheza pool table wakati wa kazi.. hoja ni kwamba vijana wajitokeze wenye utayari wa kufanya kazi na wasio na ajira tukawapokee wakuu wa mikoa kwa maandamano watuonyeshe wapi pa kufanya kazi...
 
Ila vijana nao wamezidi kushinda kwenye ma-pool kucheza kamali...

Japo wapo ambao ajira ni tatizo ila baadhi yao ni kujiendekeza tu....

Na siku hizi ku-bet ndio habari ya mjini...wanashinda kwenye vibanda umiza kufatilia mikeka sijui
 
Ajira ni shida kweli ila vijana wengi siku hizi wamekuwa nyoronyoro sana wanachagua kazi mno mtu hana kazi ila anataka kazi aanze na mshahara wa Milion 1...Kuna dogo mmoja jirani nilimtafutia kazi ya takehome 700... Kisa tu ile kazi sometimes anatoka saa 3 usiku na weeknd wakati mwingine anaitwa kazini hiyo ndiyo ikawa sababu ya dogo kuacha kazi baada ya kupokea mshahara wa mwezi mmoja tu...Hopeless kabisa..
 
Tukalime kwenye mashamba ys babaako??? Musiwe mnaropoka mashamba wameyaodhi wao afu wanatuletea tararira hapa kumanina zake na vijibwa vyake mnakera sana.
Lazima muwe wabunifu si lazima kulima hata kuuza maji kweli inashindikana? Hata kufanya kazi za ulinzi napo mtoto Wa kiume huwezi ili upate kimtaji cha kuanza?
Serikali ninavyojua haiwezi kuwaajiri watu wote, eeeh kwa hiyo mtaamkia kwenye pool hadi maisha yenu yote hapa duniani?
 
Ajira ni shida kweli ila vijana wengi siku hizi wamekuwa nyoronyoro sana wanachagua kazi mno mtu hana kazi ila anataka kazi aanze na mshahara wa Milion 1...Kuna dogo mmoja jirani nilimtafutia kazi ya takehome 700... Kisa tu ile kazi sometimes anatoka saa 3 usiku na weeknd wakati mwingine anaitwa kazini hiyo ndiyo ikawa sababu ya dogo kuacha kazi baada ya kupokea mshahara wa mwezi mmoja tu...Hopeless kabisa..
mkuu km hyo nafasi bdo ipo nifanyie mpango mm basi ht km ntaenda mpk j2 na kutoka 6 za ucku,,dah!!
 
mkuu km hyo nafasi bdo ipo nifanyie mpango mm basi ht km ntaenda mpk j2 na kutoka 6 za ucku,,dah!!
Ndiyo shida watu wenye shida na kazi hawapata na hawa wengine wanakatisha hata tamaa ya kujua yupi yupo serious yupi na yeye anatafuta ela ya mwezi mmoja apate smart fone tu arudi kitaa...Hiyo chansi nilimpa sister mmoja amempeleka dogo wake..
 
Hapo ndio tunapokosea kuhusu kuhalalisha ipi ni kazi bora na ipi sio bora. Kuhusu Pool table ni bonge la biashara kuanzia wauzaji wa hizo pool table, mfanyabiashara anayeenda kuliweka sehemu mtaani na vijana wanaocheza hiyo michezo pia, ila kwasababu tunaamua kubana akili zetu tunaona kama vijana na wafanya biashara waliowekeza kwenye hiyo biashara ni kama mchezo wa luxury kwa hiyo vijana hawaruhusiwi kucheza. Pool table imenisaidia sana hasa nilipokuwa chuo afu boom limekata hapo ndio umuhimu wake ulipokuwa unakuja nabakiwa na elfu 5 lakini nikikomaa kuanzia mida ya saa 10 nimetoka kwenye pindi mpaka saa 5 usiku nakuwa nimepiga kama Elfu 60 sababu naamini kwenye pool table niko vizuri so mambo ya kumsumbua mzazi na kuwasubilia bodo mpaka walete hiyo pesa wanayoichelewesha kimagumashi mpaka tutake kogoma ndio walete. Kwa hiyo mi naona kutolea mfano pool table ni mawazo mgando kwa kiasi flani, sisemi kila mtu achezepool table au kila kijana achote maji hapana ni mgawanyo wa kazi hii ni inchi inaongozwa na Capitalist system ilimradi biahara ni halali na inalipiwa kodi, mpaka bao alilocheza Mwalimu Nyerere linapigiwa kamali siku hizi sio sehemu ya kupigia story tena.
 
Tatizo vijana wanatumia mchezo wa pool table kutafutia pesa za viroba, bangi na mambo mengine ya kijinga hawawazi kujikwamua kiuchumi. Jaribu kuchunguza vijana wengi wanaocheza pool table mida ya asubuhi wengi wao hawana malengo yoyote ya kimaisha na ndo huwapa wanawake mimba na kushindwa kulea watoto. Nchi yetu ina fursa nyingi sana na tuko blessed kuna shughuli unaweza anzisha hata kwa capital ya sh. 2000 na ukaendesha maisha yako na kufanikiwa. Tatizo hatupendi kujituma na kuacha maisha ya anasa, wengi tunapenda kuishi maisha yaliyo nje ya kipato chetu.
 
Lazima muwe wabunifu si lazima kulima hata kuuza maji kweli inashindikana? Hata kufanya kazi za ulinzi napo mtoto Wa kiume huwezi ili upate kimtaji cha kuanza?
Serikali ninavyojua haiwezi kuwaajiri watu wote, eeeh kwa hiyo mtaamkia kwenye pool hadi maisha yenu yote hapa duniani?
Huo ni mfano mmoja ila sector zote wamekaba wanataka tukawe watwana kwenye mashamba yao!
 
Lazima muwe wabunifu si lazima kulima hata kuuza maji kweli inashindikana? Hata kufanya kazi za ulinzi napo mtoto Wa kiume huwezi ili upate kimtaji cha kuanza?
Serikali ninavyojua haiwezi kuwaajiri watu wote, eeeh kwa hiyo mtaamkia kwenye pool hadi maisha yenu yote hapa duniani?
Kuna dogo zamani alikuwa mcheza pool table sana maeneo ya Soweto, saizi ana baiskeli 8 anakodisha na anadai mtaji aliupatia hapo ila sasa hivi ameacha. Je, mipango yenu haikinzani na imani kwamba riziki ni mafungu saba?
 
Mh Rais ametoa agizo kwa wakuu wa mikoa akiwaapisha leo ikulu..kuhakikisha wanawalazimisha vijana kufanya kazi,, ni marufuku kucheza pool table wakati wa kazi.. hoja ni kwamba vijana wajitokeze wenye utayari wa kufanya kazi na wasio na ajira tukawapokee wakuu wa mikoa kwa maandamano watuonyeshe wapi pa kufanya kazi...
Kazi ipo. Viwanda tayar ndio maana kawaagiza. Wasipofanya kazi viwanda vitakufa. Kiwanda cha samaki ukanda wa piano tayar
 
Ila vijana nao wamezidi kushinda kwenye ma-pool kucheza kamali...

Japo wapo ambao ajira ni tatizo ila baadhi yao ni kujiendekeza tu....

Na siku hizi ku-bet ndio habari ya mjini...wanashinda kwenye vibanda umiza kufatilia mikeka sijui
Hicho ni kizazi cha vijana waliokata tamaa. Hawaoni mlango, hakuna wa kuwakomboa ndio maana wamekwama hapo...
 
Back
Top Bottom