Vijana wapenda mabadiliko tuwe watulivu

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Dec 14, 2013
611
724
Nimeona niliseme kidogo hili.

Kuna watu ambao ni wapiganaji wenzetu katika kulete mabadiliko ya kweli hapa nchini wamekuwa na mzuka sana juu ya mambo kadhaa yanayotokea hivi sasa hasa hili la ukandamizaji wa haki unaowakumba wapinzani.

Nimesoma maandiko kadhaa yanayowalaumu viongozi wa juu wa chama kwamba wamekuwa wapole sana , hawana maamuzi magumu katika kupigania haki za makamanda wanaoteseka. Kamanda fulani nimemsoma akilalamika na kumlaumu mzee Lowasa eti hajaenda kumjulia hali kamanda Lema huko gerezani . Huyu kamanda ameenda mbali na kutoa lugha kali kwa huyu mzee kwamba hafai tena kukaa kwenye upinzani.

Ndugu zangu mimi nadhani tunapaswa kuwa watilivu na werevu sana katika kipindi hiki cha kupigania demokrasia ya kweli hapa nchini.

Mimi siko karibu na viongozi wa CHADEMA , lakini naamini ukimya wao kwenye swala hili la Lema umekaa kimkakati zaidi. Kitendo cha viongozi wa CHADEMA kuanza kujazana kule gerezani kitawafanya watesi wa Lema kijiona ni Miungu watu. Isitoshe Lema si wa kwanza kukubwa na haya yanayomfika leo. Wapigania haki wote duniani walifungwa na wengine kuuawa kabisa. Mandela alikaa gerezani zaidi ya miaka 20, badae ukombozi ulipatikana kule kusini wa Afrika.

Nawaomba tena ndugu zangu tuwe watulivu, werevu , wenye fikra pevu katika kuyatafakali mambo. Haki huwa haipotei na ukweli ukiupuuza na tabia ya kujitetea wenyewe. Mimi naamini haki ya Lema iko karibu sana, na mda si mrefu ataipata.
 
Back
Top Bottom