Elections 2010 Vijana wapatiwe nafasi ya kugombea Ubunge 2010!

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kumekuwa na usemi hapa Tanzania kwa muda sasa kuwa VIJANA NI TAIFA LA KESHO.Sensa ya 2002 imedhihirisha pia kuwa Vijana ni wengi zaidi kuliko wazee,vilevile wazee wamekwisha tuongoza kwa nafasi mbalimbali hivyo ni muafaka kwao kupumzika na kuwaachia nafasi watoto wao ili nao wawaongoze na wao kubakia washauri tu.Nakaribisha maoni kuhusu hili kama changamoto ya uongozi katika Tanzania.
 
wazo zuri lakini jambo la msingi kwanza vijana wenyewe lazima wajipike kielimu kuongoza si mchezo, hata kuongoza kundi la n'gombe na mbuzi kunataka maarifa fulani na si kukurupuka tu, vijana wajipike kielimu, wajifunze ukomavu wa kukabiliana na matatizo,ustahamilivu na kukubali kukosolewa na kujirekebisha.
 
Kumekuwa na usemi hapa Tanzania kwa muda sasa kuwa VIJANA NI TAIFA LA KESHO.Sensa ya 2002 imedhihirisha pia kuwa Vijana ni wengi zaidi kuliko wazee,vilevile wazee wamekwisha tuongoza kwa nafasi mbalimbali hivyo ni muafaka kwao kupumzika na kuwaachia nafasi watoto wao ili nao wawaongoze na wao kubakia washauri tu.Nakaribisha maoni kuhusu hili kama changamoto ya uongozi katika Tanzania.

Mkuu,
Una maana vijana sasa hivi hawaruhusiwi kugombea Ubunge au una maana na wao wapewe viti maalum au upendeleo fulani kwa sababu ni vijana.?? Point yako hapa wala sioni.
 
..Hussein Mwinyi, Laurian Masha,Vita Kawawa,Zitto Kabwe,Ngeleja,Adam Malima,Tony Apson Mwangonda, Deusdedit Kamala, David Mathayo, Hawa Ghasia,....

..badala ya kusubiri kushikwa mkono, ni vizuri vijana wakajitosa kugombea nafasi za uongozi.

..vyama vya siasa viko vingi vya kutosha, siyo lazima kwenda CCM.
 
..Hussein Mwinyi, Laurian Masha,Vita Kawawa,Zitto Kabwe,Ngeleja,Adam Malima,Tony Apson Mwangonda, Deusdedit Kamala, David Mathayo, Hawa Ghasia,....

..badala ya kusubiri kushikwa mkono, ni vizuri vijana wakajitosa kugombea nafasi za uongozi.

..vyama vya siasa viko vingi vya kutosha, siyo lazima kwenda CCM.

Hivi ujana ni umri au fikra? manake kwenye hiyo list hapo juu, ni wachache wenye mawazo na uwezo tunaotegemea vijana wengi wawe nao. Ukimuona kijana anatetea ujinga wa mfumo tulionao, sidhani kama anapaswa kuitwa kijana, eti kwa sababu ya umri wake tu.
 
Katika nchi ambayo average ya watu kuishi ni miaka 45, mnamuita mtu mwenye miaka 40 ni kijana? Ajabu kubwa hii!

Sasa mwenye miaka 20 atakuwa nani? Mtoto?

Uwezo ndio kiwe kigezo cha kupewa uongozi wowote ule.
 
Suala sio vijana kupewa nafasi, ni vijana wenye nia na uwezo kujitokeza. Issue ingekuwa kwa wazee ambao wanajua uwezo wao umefikia ukomo, wakae pembeni kupisha nguvu mpya ili mradi hiyo nguvu kweli ipo na inaonyesha proven leadership ability na capabilities.

Tatizo moja kubwa la wengi wa viongozi wetu, ubunge ni ulaji na status quo na sio uwezo wa uongozi. Yaani kuna watu wanaingia bungeni ili kusaka ulaji na status sio kuongoza. Hata wabunge ka Edward Lowasa, Ritha Mlaki na wengineo, baada ya kukosa ulaji, huko bungeni wako wako tuu kutunza status quo zao maana hawaulizi swali lolote wala hawachangii mada yoyote.

Hata wabunge wenye uwezo mkubwa kifedha kama Mkono, Rostam Aziz, Sumri na matajiri wengine, hawana haja ya kurudi bungeni, badala yake wapishe nguvu mpya na wao kuendeleza maendeleo kwa jeuri ya pesa yao.

Lakini pia hata vijana walioko bungeni ambao hawana lolote, nao pia wapumzike maana kuna vijana lukuki na hamna wafachanyacho zaidi ya kutembeza 'bakora' na kwa wanawake 'kuachia' badala ya kuonyesha uwezo wa uongozi.

Issue muhimu ni jee, hao vijana wenye nia na uwezo wa kujaza hiyo vacuum ya wazee/wasiweza wapo?.
 
Vijana lazima wajue wajibu wao, na lazima wajue ushindani na lazima wao wenyewe wajue wakati ndio huu.
Wananguvu wanafikira na wanaweza, sasa wajitokeze hakuna mbereko hapa.

Futa useme wa vijana ni taifa la kesho vijana ni taifa la leo, sasa na wakati huu.
Wazee wamezeeka sio umri tu hata fikra zao ni nzee.
 
Vijana "wapatiwe, wapewe" - watapatiwa na nani? Kama wewe ni kijana na unafikiri unafaa, enter the race period.Usitegemee kupewa maana ukipewa utapewa na masharti na matokeo yake utakuwa kama hao unaoona hawafai.
Ukiingia kwa nguvu na uwezo wako utakuwa na uhalali wa kuleta mabadiliko.
 
Mimi nami nilitaka kusema "kwa nini wapatiwe"? na "kwa nini wasichukue nafasi"?

Lakini ukitaka kuielewa pointi ya swala hili (a true tragedy actually) ni kwamba, mleta mada ameshaelewa kwamba kwa sasa ubunge Tanzania kuna monopoly fulani inaendelea, ambayo inakaliwa na wazee.

Na katika political culture ya Tanzania kwenda against hii monopoly ni risky sana, kwa sababu unaonekana "kijana hana heshima" na utaishia kuchekwa tu huku wazee wakipendekezana wao kwa wao.Sana sana hii hali iko CCM ambako kuna watu wamekuwa wabunge tangu serikali ya awamu ya kwanza.Na sote tunajua CCM ndicho chama chenye viti vingi vya ubunge, tumefika wakati mpaka wagombea urais wazee wananadiwa kwa turufu ya ujana! vijana wafanye nini kama sio kuomba msale?

Huu unaweza kuwa ni wito mzuri sio tu kwa vyama, bali pia hata kwa wananchi kuwapigia kura vijana wenye sifa watakaojitokeza.

Ila kama walivyosema wengi hapo juu, sina budi kumalizia kwa kusema vitu vizuri haviji kirahisi na inabidi vifanyiwe kazi, na kama vijana wanataka hizi nafasi, zaidi na kuombewa dua hizi, itabidi wajionyeshe kuwa wanafaa kwa kujitokeza kwa wingi wa namba na ujuzi.
 
Last edited:
Back
Top Bottom