Vijana wanawezeshwa vipi kujiajiri

mkuzi

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
1,618
2,000
je kwanza ni fursa zipi zipo za kufanya ili zikulipe ili ukiacha kazi usijute?hebu nipeni mifano wa shughuli zipi binafsi za kufanya ili zitulipe?na mtaji kwa makadirio ni shs ngapi?
 
Mwl.RCT

JF-Expert Member
Jul 23, 2013
10,065
2,000
je kwanza ni fursa zipi zipo za kufanya ili zikulipe ili ukiacha kazi usijute?
Unaangalia mazingira uliyopo na fursa zilizopo, Unazifanyia kazi kwanza ili upate mwelekeo wa nini cha kufanya baada ya kuacha kazi.
hebu nipeni mifano wa shughuli zipi binafsi za kufanya ili zitulipe?
Rejea hoja ya msingi hapo juu, Kila mahala kuna fursa, Ni jukumu lako kutafuta fursa zilizopo mahala ulipo, Umiza kichwa na utapata.
na mtaji kwa makadirio ni shs ngapi?
Mtaji huwa ni jambo la mwisho baada ya kuipata fursa sahihi ya ndoto yako. Ili kujitegemea kiuchumi hakuna kiwango kilicho fixed kwamba ukiwa nacho ndio utakuwa na mafanikio.

Wapo wajasiliamali walionza na mitaji ya 300,000 na wakapata mafanikio, na wengine walianza na mitaji 10,000,000 au zaidi, na wakashindwa kupata mafanikio. hii inategemea ni fursa ipi unataka kuifanyia kazi na skills ulizonazo katika fursa husika.

Na tafiti zinaonyesha wenye mafanikio makubwa ni wale walio anzia chini na kukabiiana na changamoto nyingi katika kufursa walizo zichagua kuzifanyia kazi.

Kila lakheri mkuu.
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
1,500
Mtaani kugumu...... Haya ndio Majibu ya walio wengi kwenye ushauri wa kuacha kazi, Kama unataka kuacha acha usiombe ushauri, Nakuomba ufanye kautafiti. Tafuta watu kama kumi ambao wako mtaani na unawaamini, waombe ushauri.

Kama wakitokea wawili wakakubaliana na wazo lako njoo nidai vocha ya 500(joke)

Kimsingi haya maamuzi yanategemea tu utashi wako, Unapokua na Biashara huku bado uko kwenye ajira watumishi huwa wanakupiga sana, mwisho wa siku biashara inakufa na ndoto yako ya kuacha kazi inakufa

Mimi nakushauri anagalia mfuko wako na uwe na uhakika wa biashara ambayo unataka kufanya, Kumbuka challenges hazipo maofisini peke yake hata kwenye biashara pia kuna challenges.

Biashara ambayo unaweza kuanza nayo kama bado hujabuni biashara jaribu kuangalia Mazao, Mazao hayana hasara jaribu ku avoid perishable things kama viazi na mboga mboga.

Mazao kama mahindi yakiharibika utauzia wanaotengeneza byakula vya kuku.

suala kubwa ni mfuko wako na utayari wako wa kuishi kigumu.
Mkuu umewai kufanya biashara? au kuacha kazi na kuwa mtaani?

Ukweli ni kwamba kuacha kazi na kwenda mtaani 90% ni jinsi utakavyo control hisia zako na zawatu around (emotional). 10% ndio failure or success.

Mimi niliacha kazi yenye kipato cha juu sana. Niliamua tuu kwamba ikifika september naacha, nikaandika resignation letter nikawapa one week, sikutaka discussion. Nikaacha, nyumba ilukuwa bado kuisha na familia nzima wakasema huyu anaitaji mganga amtibu. Nilichokuwa nacho ni courage, ukiwa na courage (utashi) hata dunia nzima iende mashariki wewe peke yako uende magharib hautajutia.

La muhimu ni ujipange, andika chini kwamba unataka kufanya nini na mauzo ya kiasi gani kwa mwezi yatakufanya upate utulivu, yaweke yale mauzo kwa siku kisha anza mapambano.

You can do it.
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
1,500
Great, nilishaacha kazi ya Ualimu mara mbili, nikarudi kwa kazi nyingine ila pia roho yangu inaniambia kuwa ni Lazima niache kazi ili niwe na kitu ambacho ni lasting.... kazi zina muda, kazi za watu zinazeesha, zinaleta magonjwa ya stress na kukuminya sana kufikiria nje ya box. Nashukuru kwamba nakarinia kuvuka daraja hili, sitarudi nyuma this time MUNGU anisaidie. Kuna kitabu nakisoma kipo kwenye Playstore kinaitwa THINK AND GROW RICH aaaghhhh kinanitia nguvu sana, I encourage you guys mkisome pia.

Hivi vitabu vipo vingi na vya bure
Lazima tubadilike, lazima tubadilishe our Life style, inawezakana lakini ni lazima tujikane kwanza, lazima tujishushe, lazima tuwe commited.

Thank you
Una burning desire ya kutoka mwana. Kikubwa sana ni uvivu wa kusoma ambao watu wengi wanao. Vitabu vina siri kubwa sana.
 
Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,335
2,000
Mkuu umewai kufanya biashara? au kuacha kazi na kuwa mtaani?

Ukweli ni kwamba kuacha kazi na kwenda mtaani 90% ni jinsi utakavyo control hisia zako na zawatu around (emotional). 10% ndio failure or success.

Mimi niliacha kazi yenye kipato cha juu sana. Niliamua tuu kwamba ikifika september naacha, nikaandika resignation letter nikawapa one week, sikutaka discussion. Nikaacha, nyumba ilukuwa bado kuisha na familia nzima wakasema huyu anaitaji mganga amtibu. Nilichokuwa nacho ni courage, ukiwa na courage (utashi) hata dunia nzima iende mashariki wewe peke yako uende magharib hautajutia.

La muhimu ni ujipange, andika chini kwamba unataka kufanya nini na mauzo ya kiasi gani kwa mwezi yatakufanya upate utulivu, yaweke yale mauzo kwa siku kisha anza mapambano.

You can do it.

Big point
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Jul 18, 2007
1,601
1,500
Kuna mambo makubwa kama mawili au matatu lazima uyafanye.
1. Jiandae kifikra kabla hujaachaa (mental preparation), hichi kitu muhimu sana na kinaweza chukua muda sana. Sababu kwenye kitu chochote psychology inachukua nafasi kubwa sana. Muhimu hapa ni kwamba hakikisha unafikiria positive side na unakaa mbali na negative thinking, sisemi uwe naive maana kuna tofauti kubwa ya kufikiria positive na kuwa naive. Andaa kichwa chako kupambana na "naysayers" wazee wa kukwambia utashindwa, huwezi kufanikiwa, utajuta, utasaga na ndala. Hawa lazima ujue jinsi ya kufanya fikra zao zisiingilie fikra zako, lakini kujiandaa kifikra ni pamoja na kuandaa kuishinda sauti ya ndani (inner voice) ambayo inakuongelesha kwa ndani kukwambia unajua mkuu ukichemka hapa familia yote choka, au at least wewe unapata 700,000 kwa mwezi, wenzio wanapata 0. Hii ikatae kabisa, kwa kujiandaa kifikra. Sikiliza sana motivational speakers kwenye youtube kama kina Les Brown, Napoleon kwa Tanzania kina Erik Shigongo, Mr Mauki na wengine.

2. Andaa Plan nzima ya mchezo kwenye karatasi. Najua watu wengi wanasema nisha plan, kila kitu na plan yenyewe kwa bahati mbaya ipo kichwani. Hawa wanajindanganya tuu. Plan lazima iwe kwenye karatasi, iweke uione na ujinasabishe nayo. Isome mara kwa mara rekebisha sehemu zinazo stahiki. Ibandike kwenye kuta za chumba chako, isome na ujirecord kisha isikilize over and over ukiifanyia maboresho. Mfano, unataka kufungua supermarket ndogo plan lazima iseme wapi, ukubwa wa duka, mtaji, njia yako ya kufanya marketing na kupata masoko. Plan ndio ushindi, mechi haishindwi uwanjani mechi yoyote inashindwa kwenye plan. Kama Plan zako ni weak, jiandae kuondolewa kwenye reli.

3. Test plan yako hapo juu kwa kufanya uchunguzi.Hii ni pilot process, unaweza kutembelea wenye hiyo biashara ukaangalia na kujifunza, unaweza kuanza kidogo. Hapa nafasi ni kubwa inategemea wewe unataka kutest vipi plan yako.

4. Never have Plan B. Usisubutu kuwa na Plan B, sababu plan B inaairibia Plan A tuu hakuna jingine. Ukipigana na mlango wazi ni tofauti sana kupigana mlango ukiwa umefungwa.

5. Never regret ukijaribu. Mimi nilipakiza watoto na familia kwenye ndege kurudi Tanzania baada ya miaka 15 ughaibuni na nilikuwa na maisha standard kabisa. Kikubwa nilichoshinda ni kwamba niliapa kuto kujilaumu kwa maamuzi niliyofanya. Life is too short kutojaribu roho nini inataka.

I support yoyote anaetaka kuacha kazi sababu hao ndio wajenga ajira za wengine wengi ambao mungu ajawapa utashi wa kujiamini na kufanya maamuzi magumu.
 
dagii

JF-Expert Member
Dec 23, 2013
3,984
2,000
Ukikaribia kuacha nielekeze nije niombe nafasi yako mkuu tena kwakukutaja kabisa
 
Jorochere

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
995
2,000
Mtaani kugumu...... Haya ndio Majibu ya walio wengi kwenye ushauri wa kuacha kazi, Kama unataka kuacha acha usiombe ushauri, Nakuomba ufanye kautafiti. Tafuta watu kama kumi ambao wako mtaani na unawaamini, waombe ushauri.

Kama wakitokea wawili wakakubaliana na wazo lako njoo nidai vocha ya 500(joke)

Kimsingi haya maamuzi yanategemea tu utashi wako, Unapokua na Biashara huku bado uko kwenye ajira watumishi huwa wanakupiga sana, mwisho wa siku biashara inakufa na ndoto yako ya kuacha kazi inakufa

Mimi nakushauri anagalia mfuko wako na uwe na uhakika wa biashara ambayo unataka kufanya, Kumbuka challenges hazipo maofisini peke yake hata kwenye biashara pia kuna challenges.

Biashara ambayo unaweza kuanza nayo kama bado hujabuni biashara jaribu kuangalia Mazao, Mazao hayana hasara jaribu ku avoid perishable things kama viazi na mboga mboga.

Mazao kama mahindi yakiharibika utauzia wanaotengeneza byakula vya kuku.

suala kubwa ni mfuko wako na utayari wako wa kuishi kigumu.
Kama hayo ndio mawazo yenu lazima kitaa kiwashike .....! Huwez kufanikiwa katika maisha kwa kukusanya data kutoka kwa watu walioshindwa.Kwa nn usitumie ..... "your own experience in lfe....?"ukikalia kusikiliza wanaosema hawawez na ww hutaweza.....!
 
Internal

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
3,541
2,000
Kaujiriwa ni utumwa tukubali au tukatae ukweli haubadiliki unabakia pale pale, binafsi bado nipo nimeajiriwa na kabla ya hapa nilikuwa mtaani hivyo najua wapi sahihi na wapi si sahihi.

Soon nipo njiani kuachia ngazi wakave ndugu, jamaa, na marafiki wenye njozi za kuajiriwa nao wajionee ninayowaambia kila siku.

Uhuru hakuna mpaka ndugu wananiuliza unafanya kazi nje ya Sayari Dunia nn,? Maana kuna vitu vinaniitaji niwepo nyumbani kwa muda flani lakin kazini huwezi kuomba ruhusa kila mwezi na ukaruhusiwa.

Ukiicha kazi hutakufa njaa maana wasioajiriwa wanalalamika tu kuwa maisha magumu lakini hawajawahi kuniomba debe la unga hata siku moja.
Ajira inalemaza akili mana unajua lazima pesa ije mwisho wa mwezi hivyo akili haipanuki kuona fursa hata kama watu wanakufa kwa kunywa maji yenye madini ww unadhani serikali ndio mtatuzi tu kumbe ungefikiri vizur unaweza kutumia mwanya huo kupiga pesa huku ukiokoa maisha ya wengi.

Ukijiajiri nashauri tusitegemee mradi mmoja bali tufungue miradi mingi hata kama ni midogo midogo hapo tutafurahia kuacha kazi.

Umuhimu mkubwa wa kujiajiri ni kwamba hutamuwaza mtu bali utawaza watu na kazi yako, kutokuwaza mtu mmoja na kuwaza watu wengi hio ni moja ya fursa kwako maana mmoja akiteleza unanafasi ya kuwaza wengine kama wateja lakini mmoja akikatisha kazi yako ndo basi tena.

Tusisubiri tuwe na mamilioni ndo tuniajiri hicho hicho kidogo ndo kinaleta kikubwa, ili uweze kuendesha mradi wako ni vyema ukaanza na kidogo kidogo ili uendelee kujifunza naman ya kuendesha mkubwa, mtoto wa darasa la kwanza haanzi na magazijuto bali huanza na toa, Toa, jumlisha, zidisha, gawanya kisha mafumbo mpaka hapo ndo anakuwa ameiva na kupewa magazijuto sasa.

Tutoke kwenye utumwa tuwe huru tuongeze siku za maisha kwa kuondoa stress za maboss, wao wakigombana na wake zao hasira wanamalizia kwetu, kwann tukubali kubeba stress za watu wengine wakati na sisi tuna zetu?
 
BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
781
1,000
Unaangalia mazingira uliyopo na fursa zilizopo, Unazifanyia kazi kwanza ili upate mwelekeo wa nini cha kufanya baada ya kuacha kazi.

Rejea hoja ya msingi hapo juu, Kila mahala kuna fursa, Ni jukumu lako kutafuta fursa zilizopo mahala ulipo, Umiza kichwa na utapata.

Mtaji huwa ni jambo la mwisho baada ya kuipata fursa sahihi ya ndoto yako. Ili kujitegemea kiuchumi hakuna kiwango kilicho fixed kwamba ukiwa nacho ndio utakuwa na mafanikio.

Wapo wajasiliamali walionza na mitaji ya 300,000 na wakapata mafanikio, na wengine walianza na mitaji 10,000,000 au zaidi, na wakashindwa kupata mafanikio. hii inategemea ni fursa ipi unataka kuifanyia kazi na skills ulizonazo katika fursa husika.

Na tafiti zinaonyesha wenye mafanikio makubwa ni wale walio anzia chini na kukabiiana na changamoto nyingi katika kufursa walizo zichagua kuzifanyia kazi.

Kila lakheri mkuu.
Angalia mahali ulipo/kwenye jamii yako HAKUNA NINI, KUNA TATIZO GANI, kisha kilete hicho kitu kwenye hiyo jamii. Au tatua hilo tatizo kwenye jamii yako.

Kuna tatizo la maji kubwa kwenye jamii yako, chimba kisima uuze maji. Je watu wa jamii uliyopo wanaenda mbali sana kukoboa na kusaga nafaka. Weka mashine ya kukoboa na kusaga.

HIYO NI APPROACH YA KWANZA

Aproach ya pili angalia hata kama huduma au bidhaa flani ipo kwenye mazingira yako, lakini jiulize JE WASAMBAZAJI WA HUDUMA HUSIKA WANATOSHA, WANALISTAHIMILI SOKO?

Kwa MFANO, kweli hapo ulipo kuna huduma ya M-PESA au TIGO PESA au YOYOTE PESA. Je wateja sio wengi kuliko uwezo wa mtoa huduma? Kama wateja wameelemea watoa huduma, anzisha na wewe.

Mbinu nyingine ni KUUZA BIADHAA ZA KAWAIDA TU kama wanazouza washindani wako, lakini unatumia mbinu ya KUFANYA JAMBO UNIQUE KWENYE BIASHARA YA KAWAIDA. Mfano, washindani wako wote wanafungua biashara saa mbili Asubuhi na kufunga saa 2 usiku, wewe fungua saa 12 Asubuhi na kufunga saa 4 usiku. Mfano mwingine, labda umegundua washindani wako hawana back up plan pale umeme unapokatika na huduma unayoitoa inahitaji umeme, weka solar au generator in case umeme umekatika. Cha muhimu ni KUFANYA UTAFITI KABLA na KIPINDI UNAENDELEA na biashara yako.
 
BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
781
1,000
Kuna mambo makubwa kama mawili au matatu lazima uyafanye.
1. Jiandae kifikra kabla hujaachaa (mental preparation), hichi kitu muhimu sana na kinaweza chukua muda sana. Sababu kwenye kitu chochote psychology inachukua nafasi kubwa sana. Muhimu hapa ni kwamba hakikisha unafikiria positive side na unakaa mbali na negative thinking, sisemi uwe naive maana kuna tofauti kubwa ya kufikiria positive na kuwa naive. Andaa kichwa chako kupambana na "naysayers" wazee wa kukwambia utashindwa, huwezi kufanikiwa, utajuta, utasaga na ndala. Hawa lazima ujue jinsi ya kufanya fikra zao zisiingilie fikra zako, lakini kujiandaa kifikra ni pamoja na kuandaa kuishinda sauti ya ndani (inner voice) ambayo inakuongelesha kwa ndani kukwambia unajua mkuu ukichemka hapa familia yote choka, au at least wewe unapata 700,000 kwa mwezi, wenzio wanapata 0. Hii ikatae kabisa, kwa kujiandaa kifikra. Sikiliza sana motivational speakers kwenye youtube kama kina Les Brown, Napoleon kwa Tanzania kina Erik Shigongo, Mr Mauki na wengine.

2. Andaa Plan nzima ya mchezo kwenye karatasi. Najua watu wengi wanasema nisha plan, kila kitu na plan yenyewe kwa bahati mbaya ipo kichwani. Hawa wanajindanganya tuu. Plan lazima iwe kwenye karatasi, iweke uione na ujinasabishe nayo. Isome mara kwa mara rekebisha sehemu zinazo stahiki. Ibandike kwenye kuta za chumba chako, isome na ujirecord kisha isikilize over and over ukiifanyia maboresho. Mfano, unataka kufungua supermarket ndogo plan lazima iseme wapi, ukubwa wa duka, mtaji, njia yako ya kufanya marketing na kupata masoko. Plan ndio ushindi, mechi haishindwi uwanjani mechi yoyote inashindwa kwenye plan. Kama Plan zako ni weak, jiandae kuondolewa kwenye reli.

3. Test plan yako hapo juu kwa kufanya uchunguzi.Hii ni pilot process, unaweza kutembelea wenye hiyo biashara ukaangalia na kujifunza, unaweza kuanza kidogo. Hapa nafasi ni kubwa inategemea wewe unataka kutest vipi plan yako.

4. Never have Plan B. Usisubutu kuwa na Plan B, sababu plan B inaairibia Plan A tuu hakuna jingine. Ukipigana na mlango wazi ni tofauti sana kupigana mlango ukiwa umefungwa.

5. Never regret ukijaribu. Mimi nilipakiza watoto na familia kwenye ndege kurudi Tanzania baada ya miaka 15 ughaibuni na nilikuwa na maisha standard kabisa. Kikubwa nilichoshinda ni kwamba niliapa kuto kujilaumu kwa maamuzi niliyofanya. Life is too short kutojaribu roho nini inataka.

I support yoyote anaetaka kuacha kazi sababu hao ndio wajenga ajira za wengine wengi ambao mungu ajawapa utashi wa kujiamini na kufanya maamuzi magumu.
Hahaha Naysayers, umenikumbusha Kiyosaki anawaita Cynics (ikiwepo na sauti ndani yako). Cynics will always tell u, the sky is falling.... It's just NOISES
 
DA HUSTLA

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
2,381
2,000
dedication kwenu;
retire young, retire rich by R.Kiyosaki...
ni miongoni mwa maamuzi magumu ambayo ni sahihi.
ni kosa kuacha kazi ujiajiri akilini mwako ukiwa na wazo mambo yakigoma nitarudi kuajiliwa.
unaweza kuja kuaibika. Hiyo mission ni kama movie ya The Hardway The only way, makomando wanatua na ndege iliyowaleta inalipuliwa kuwadhihirishia hawana option zaidi ya kushinda pambano msituni maana hakuna usafiri wa kuwarudisha.

ukifanya maamuzi hayo mapema, utapata faida ya Muda mrefu ila lazima upitie bonde la uvuli wa mauti ili kukuandaa kukabiliana na kupata na kukosa maishani. bonde hilo huwarudisha wengi kwenye ajira wakiogopa gharama ya kujiajiri.
Salute
 
Mlachake

JF-Expert Member
Oct 13, 2009
4,335
2,000
Kama hayo ndio mawazo yenu lazima kitaa kiwashike .....! Huwez kufanikiwa katika maisha kwa kukusanya data kutoka kwa watu walioshindwa.Kwa nn usitumie ..... "your own experience in lfe....?"ukikalia kusikiliza wanaosema hawawez na ww hutaweza.....!

Point Mkuu.
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
25,545
2,000
Mtaani kugumu...... Haya ndio Majibu ya walio wengi kwenye ushauri wa kuacha kazi, Kama unataka kuacha acha usiombe ushauri, Nakuomba ufanye kautafiti. Tafuta watu kama kumi ambao wako mtaani na unawaamini, waombe ushauri.

Kama wakitokea wawili wakakubaliana na wazo lako njoo nidai vocha ya 500(joke)

Kimsingi haya maamuzi yanategemea tu utashi wako, Unapokua na Biashara huku bado uko kwenye ajira watumishi huwa wanakupiga sana, mwisho wa siku biashara inakufa na ndoto yako ya kuacha kazi inakufa

Mimi nakushauri anagalia mfuko wako na uwe na uhakika wa biashara ambayo unataka kufanya, Kumbuka challenges hazipo maofisini peke yake hata kwenye biashara pia kuna challenges.

Biashara ambayo unaweza kuanza nayo kama bado hujabuni biashara jaribu kuangalia Mazao, Mazao hayana hasara jaribu ku avoid perishable things kama viazi na mboga mboga.

Mazao kama mahindi yakiharibika utauzia wanaotengeneza byakula vya kuku.

suala kubwa ni mfuko wako na utayari wako wa kuishi kigumu.
Daah safi sana mkuu
 
Wimsha

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
518
500
Mkuu umewai kufanya biashara? au kuacha kazi na kuwa mtaani?

Ukweli ni kwamba kuacha kazi na kwenda mtaani 90% ni jinsi utakavyo control hisia zako na zawatu around (emotional). 10% ndio failure or success.

Mimi niliacha kazi yenye kipato cha juu sana. Niliamua tuu kwamba ikifika september naacha, nikaandika resignation letter nikawapa one week, sikutaka discussion. Nikaacha, nyumba ilukuwa bado kuisha na familia nzima wakasema huyu anaitaji mganga amtibu. Nilichokuwa nacho ni courage, ukiwa na courage (utashi) hata dunia nzima iende mashariki wewe peke yako uende magharib hautajutia.

La muhimu ni ujipange, andika chini kwamba unataka kufanya nini na mauzo ya kiasi gani kwa mwezi yatakufanya upate utulivu, yaweke yale mauzo kwa siku kisha anza mapambano.

You can do it.

At least JF imeanza kurudi kwenye heshima yake. People discuss ideas. Huu uzi kwa sasa ni wa mwaka kwangu. Yale mambo ohhh mara kibamia mara nimeachwa naomba ushauri blablaaaaa yalikuwa hayana positive impact both physically and mentally as well.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom