Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Mapokea katika familia zetu ziwe za kiafrika au mataifa mengine ziku za nyuma ambazo wengi wetu wamekulia hasa vijijini watu walikuwa na mazoea kutovaa nguo au kujifunika kama siku hizi, walibaki na vifua wazi hasa kwa akina dada ambao kwa siku hizi inaonekana kama makwazo katika jamii kwa mwanamke kuacha maziwa wazi mwanaume anahamasika kumtamani. Hata baadhi ya viungo nyeti kwa wanaume na wanawake vilikuwa vinaonekana wazi bila kificho lakini maadili yalilinda mazingira walikuwa swafiii hadi wanapooana.
Kuna makabila ambayo wasichana wakisha kua na kuvunja ungo walikuwa wanajengewa kibanda chao pekee akilala huko karibu na nyumba ya wazazi. Hali kadhalika vijana walikuwa na nyumba yao. Lakini kashfa zilikuwa chache mno kama inavyotokea siku hizi. Vijana wa kiume walikuwa wanawatembelea wasichana na kuongea nao au kuwachumbia. Ila wasichana hawakuwa na mazoea ya kutembela makazi ya vijana.
Enzi hizo wasichana walikuwa wanabaki mabikira na bila kubakwa kama itokeavyo siku hizi ingawa walibaki kama walivyoumbwa bila kujifunika, jambo ambao siku hizi linaonekana kuwa gumu maana wanaume wanashinda kuvumilia kuona maumbile ya mwanamke na hivyo kutumia kila hila kumvizia inapoonekana njia za kushawishi zimeshindikana.
Binafsi naona kama kitu kinachoharibu watu mazingira ya leo ni kukosa maadili, kukosa uwepo wa pamoja na wazazi wao kwa kupata malezi ya kutosha, na kukosekana kwa malezi ya msingi katika shule na vyuo ambako vijana wengi wapo wapo tu. Ingawa siku hizi wanavaa kwa kuficha viungo vinavyohamasisha hamu ya ngono, lakini bado tatizo linakua zaidi.