Vijana wanaposhawishika kwa viungo vya maumbile tofauti na vijana wa enzi za kuwa uchi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,891
6,902
10171638_626535134090473_2180518108614397670_n.jpg article-2094362-11893135000005DC-490_634x493.jpg download.jpg girls-dancing.jpg images.jpg penissheathII.jpg zulucover.jpg peru-nan-xx-12-medium_article_column.jpg Yanomami-leader-and-shaman.jpg zulucover.jpg yanomami-shabono2.jpg

Mapokea katika familia zetu ziwe za kiafrika au mataifa mengine ziku za nyuma ambazo wengi wetu wamekulia hasa vijijini watu walikuwa na mazoea kutovaa nguo au kujifunika kama siku hizi, walibaki na vifua wazi hasa kwa akina dada ambao kwa siku hizi inaonekana kama makwazo katika jamii kwa mwanamke kuacha maziwa wazi mwanaume anahamasika kumtamani. Hata baadhi ya viungo nyeti kwa wanaume na wanawake vilikuwa vinaonekana wazi bila kificho lakini maadili yalilinda mazingira walikuwa swafiii hadi wanapooana.

Kuna makabila ambayo wasichana wakisha kua na kuvunja ungo walikuwa wanajengewa kibanda chao pekee akilala huko karibu na nyumba ya wazazi. Hali kadhalika vijana walikuwa na nyumba yao. Lakini kashfa zilikuwa chache mno kama inavyotokea siku hizi. Vijana wa kiume walikuwa wanawatembelea wasichana na kuongea nao au kuwachumbia. Ila wasichana hawakuwa na mazoea ya kutembela makazi ya vijana.

Enzi hizo wasichana walikuwa wanabaki mabikira na bila kubakwa kama itokeavyo siku hizi ingawa walibaki kama walivyoumbwa bila kujifunika, jambo ambao siku hizi linaonekana kuwa gumu maana wanaume wanashinda kuvumilia kuona maumbile ya mwanamke na hivyo kutumia kila hila kumvizia inapoonekana njia za kushawishi zimeshindikana.

Binafsi naona kama kitu kinachoharibu watu mazingira ya leo ni kukosa maadili, kukosa uwepo wa pamoja na wazazi wao kwa kupata malezi ya kutosha, na kukosekana kwa malezi ya msingi katika shule na vyuo ambako vijana wengi wapo wapo tu. Ingawa siku hizi wanavaa kwa kuficha viungo vinavyohamasisha hamu ya ngono, lakini bado tatizo linakua zaidi.
 
ni kweli mkuu kuporomoka kwa maadili na kushindwa kujizuia ndilo tatizo hasa kwa vijana wetu wa sasa,na ikitokea leo hii wakasema tunaurudia utamaduni wetu wallahi vile tutalia na moyo.
 
ni kweli mkuu kuporomoka kwa maadili na kushindwa kujizuia ndilo tatizo hasa kwa vijana wetu wa sasa,na ikitokea leo hii wakasema tunaurudia utamaduni wetu wallahi vile tutalia na moyo.

Kikubwa kianchokosekana ni self control. Kiazi cha leo ambacho kinakosa malezi ya msingi kifamilia tofauti na kizazi kilichotutangulia ambacho vijana walikuwa karibu na familia zao kwa muda mrefu na hivyo kupata malezi ya msingi kwa maisha yao.
 
kwa kweli kikubwa ni self control vijana wa leo hawana hiyo hata kidogo utafikiri wao ndo wamewahi kuwa wanaume peke yao na wenye kutamani na wenye mihemko peke yao,yaani nakwambia mkuu ikitokea wakisema turudishe utamaduni wa zamani leo hii ni lazima tutaomba poo tu.
Kikubwa kianchokosekana ni self control. Kiazi cha leo ambacho kinakosa malezi ya msingi kifamilia tofauti na kizazi kilichotutangulia ambacho vijana walikuwa karibu na familia zao kwa muda mrefu na hivyo kupata malezi ya msingi kwa maisha yao.
 
is because we are living in an artificial world the world of human creation but at past we had a natural life very nice ,disciplined and with goodmorals now we are controlled previous the nature controlled us
 
Labda ni vyakula vya siku hizi....

Vyakula vya siku hizi si kisingizio maana vina vimelea zaidi vinavyoadhiri afya na kuwa wavivu tofauti na vyakula vya zamani ambavyo vilikuwa ni organic really pure food, ambavyo katika nchi zilizoendelea vinauzwa ghali sana kwa vile vinakuwa imported kutoka huku. Tatizo ni moja tu kukosa malezi ya msingi. Mtoto akishaanza shule basi ameachana na wazazi wake anabaki na walimu ambao nao wamekulia mazingira yaho hayo, nini kinaendelea huko shuleni au vyuoni?
 
hizo picha zenyewe hapo zilipo balaa, kifua kimesimama kama nini vile kwani wewe ukiona hivyo hushtuki hata kidogo?
 
kwani kipindi hiko hakukuwepo na polisi?Nina uhakika kesi za kubaka zilikua nyingi sana
 
Mi pono ndo inawasababishia.

Licha ya kiashiria ulichosema, lakini kuna mambo mengine ya msingi ambayo wizara ya elimu ilitakiwa kurudisha mashuleni michezo na elimu ya kujitegemea husaidia vijana ukakamavu. Vijana wengi ni tepeteme wasiojiweza, ni laini mno. Kila mara wavivu hunyemelewa na ugonjwa wa ngono, maana mwili unadai haki zake usipochoshwa kwa shughuli nyingine.

Siku za nyuma elimu iliendana sambamba na elimu ya kujitegemea kivitendo, hali kadhalika michezo mashuleni. Leo ni full uvuvu hakuna cha elimu yakujitegemea kivitendo, hakuna michezo mashuleni na vyuoni, hakuna mchakamchaka wa kuwachangamsha na kuwajengea ukakamavu vijana kabla hawajaingia madarasani, hakuna gwaride na Brass band mchana kabla ya kuingia madarasa ya alasiri. Wapo katika harakati za mipasho kwenye mitandao kama facebook. Vijana ambao damu moto na homoni ndo zinakomaa tutegemee nini sasa?

Enzi za nyuma licha ya elimu ya kujitemegea mashuleni na michezo, wanafunzi walikuwa wanatembea kwa miguu mwendo mrefu alfajiri na kurudi nyumbani alasiri tofauti na siku hizi. Tulikuwa tunapata uji mchana au makande kutokana na mavuno ya shuleni tuliyovuna tokana na elimu ya kujitegemea mashuleni. Tulikuwa na bustani, mibuni kwa ajili kahawa kibiashara, nk.
 
Back
Top Bottom