Vijana wanaoshambulia madereva kwenye foleni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vijana wanaoshambulia madereva kwenye foleni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Darling, Feb 20, 2009.

 1. D

  Darling Member

  #1
  Feb 20, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kama hamna habari habari ndio hiii; kuweni makini.

  Good afternoon

  Lets share this with you

  Napenda kuwatahadharisha kuwa muwe makini zaidi mkiwa barabarani hasa kwenye foleni. Kuna kundi la vijana zaidi ya 30 wanavamia magari wakiwa na mapanga, nondo na visu kwa lengo la kupora chochote ulichonacho na halikadhalika wanauwa ama kujeruhi.

  Maeneo hatari ni maeneo ya Jangwani- Morogoro Road,Ocean Road Seaview,Salender Bridge, Bonde la Kigogo ukitokea Ilala kuja Magomeni, Daraja la Ubungo karibu na njia panda ya kwenda UDSM na barabara ya Mandela Road ukitokea Tazara kuja Ubungo.
   
 2. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kuna kanuni inasema kuwa yeyote mwenye mali ni mwangalizi wa mali za jamii. Jamii ikiamua inaweza kuzichukua mali zake. Ni kama kitendo kinachoonekana hapa kwa hiki kikundi kinachojiita "Kiboko Msheli". Haya ni matokeo ya ubinafsi na sera mbovu za kujua kuwa unapokula wewe na kusaza wakati mwenzako analala na njaa basi hata wewe pia hautakuwa na furaha ya shibe hiyo.

  The late Prof Chachage alikuwa anapigia kelele sana gap kati ya masikini na tajiri na kusema kuwa Tanzania hatuna amani, ila tuna utulivu tu. Kwani amani itapatikana mpaka pale watu watakapo kuwa na milango ya vioo badala ya magrili, watu watakapoona kuwa hakuna haja ya kuvunja kwa mtu kuchukua kitu ambacho hata mimi kama nikitaka ntakipata kihalali.

  Haya ni matokeo ya kutowaandaa vijana kukabili maisha yao na kuendelea na utamaduni wa "on your own" kunakofanywa na watunga sera. Kwa kuwa wao wana walinzi kuanzia wanapotembea barabarani na mpaka majumbani mwao basi hawaoni haja ya kutatua tatizo hili la vijana kutokuwa na mwelekeo wa maisha na kuamua kuanzisha himaya zao barabarani kama nchi haina serikali vile ya kuvamia na kupora au hata kuua ikibidi ili mradi nao wapate kile ambacho si halali yao ila kwa kunyimwa nafasi halali ya kukipata.

  Serikali na Jeshi la Polisi hawana budi kuimarisha ulinzi kwa walipa kodi wote including wenye magari ambao wamekuwa kwenye matatizo ya kukosa ulinzi japo wanalipa kile kinachostahili. Tusipolitafutia suluhu hili basi tusishangae siku moja hawa vijana watakapokuwa tayari kufa na kuvamia pale magogoni na twin towers kwa malengo ya kuchukua chao ambacho kinaliwa na wachache kwa njia ya maandamano au hata vurugu.

   
 3. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2014
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Ninamkumbuka Mzee Ali Haji Hassan Mwinyi alisema, "pengo la wenye nacho na wasio nacho linapoongezeka, linasababisha pale yule aliyenacho anapotumia asiyenacho huona anaonewa".
   
 4. S

  Swat JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2014
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 4,182
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  kwa tunaotembea na manati ya mzungu,ukiona kundi limekuzunguka na mapanga na nondo,na ukiona wanaanza kuvunja vioo,usingoje kusikia parapanda. Lenga na kuachia kwa watatu au wanne,magari yenyewe ya mikopo haya,yanavyouma!
   
Loading...