Uchaguzi 2020 Vijana wanaosadikiwa kuwa ni wa CCM kurusha mawe kwenye msafara wa Lissu ni njama ya kuwafanya CHADEMA wajibu mashambulizi ili waonekane wanavurugu?

inabidi atulie sasa na yeye sindano iingie vizuri, yeye si ndo anaitaga watu MAJINGA, sasa atulie zamu yake sasa kupokea maumivu
 
Hao wa huko Njombe wameuawa na vijana wao ili waichafue @chademe.
Tuweke hapa orodha ya walio uliwa na CCM na hamna muuaji amekamatwa Wala polisi kuchunguza?
Bali huko Chato sio Chadema ili waichafue CCM. Kweli akili kubwa ni shida, kitu ni kimoja tu kuwashikisha adabu tarehe 28. Hapa kazi tu! Ding ..... Dong.
 
Screenshot_20201006-171411.png
Screenshot_20201014-110947.png
 
Mi kizungu sijui tafsiri wewe kama upo vizuriii ndg
Shirika la Kimataifa la Utafiti wa masuala ya Siasa kutoka China limepinga vikali ripoti ya Amnesty International kuhusu uchaguzi mkuu wa Tanzania na kudai ni ripoti iliyoegemea upande mmoja. Shirika hilo limehoji taratibu na vigezo vilivyotumiwa na Amnesty kuhoji makundi hayo ya watu na taasisi walizotaja kwenye utafiti wao. Shirika hilo limeenda mbali zaidi na kudai kuwa japo Amnesty wanajitanabaisha kama taaisisi inayotetea haki, hawaoni haki iliyotumika hapo kwenye utafutaji wa maoni.

Shirika hilo limeshangazwa na Amnesty kudai kuwa kumekuwa na matukio ya utekaji, ukamataji na unyanyasaji wa wapinzani kipindi cha kampeni ambapo imeonyesha kuegemea upande mmoja wakati wapo wanachama na wafuasi wa CCM waliouawa na kuumizwa na wapinzani.

Shirika hilo limesema utafiti wa Amnesty ni upotoshaji wa wazi kabisa wenye lengo la kuitumbukiza nchi ya Tanzania katika matatizo makubwa. Ni wazi kuwa taasisi ya Amnesty inafanya haya kwa maslahi fulani. Amnesty imelalamika kuhusiana na Vyombo vya Habari kufungiwa huku ikisahau Tanzania ni nchi huru na ina sheria na taratibu zake kwa watu au taasisi zinazokiuka sheria za nchi.

Kwa mwenye akili timamu lazima ashangae haya yanayoendelea kutoka kwa Taasisi inayojiita inatetea Haki na Demokrasia kwa wote bila ubaguzi ya Amnesty International.

Baada ya uchaguzi wa 2015 na John Pombe Magufuli kushinda Urais alianza kazi kwa kishindo na kufanya mengi makubwa ambayo hayakutegemewa katika Ulimwengu ya karne ya 21. Utendaji wa Magufuli uliibua makundi, kwa upande mmoja wakisifia kupatikana Kiongozi bora na imara asiyeyumbishwa anayeweza kuikomboa Afrika tena toka mikononi mwa wakoloni mamboleo na kwa upande wa wezi wa rasilimali za Watanzania ukiacha maumivu makali.

Makundi yenye maumivu yameamua kujitokeza hadharani kupambana na Magufuli yakitumia watu na vyombo mbambali vya habari, wanaharakati, taasisi zisizo za kiserikali, wanasheria na wanasiasa kumkwamisha na kumchafua Magufuli.

Mataifa hayo sasa yameamua kutumia uchaguzi huu kuhakikisha Magufuli harudi madarakani kwani amekwamisha mambo yao mengi na yanatumia watanzania wenzetu kuihujumu nchi yetu kwa maslahi binafsi.

Bila aibu Amnesty International imediriki kutoa makala ya kumshambulia Magufuli wakidai kuwa wapinzani wamekuwa wakionewa. Nasema ni aibu kwani kama Amnesty inasimamia haki kwa wote ilitakiwa kukemea pia mauaji ya vijana na wafuasi wa CCM yaliyofanywa na vijana wa CHADEMA tena ambao wamekiri kufanya matukio hayo.

Amnesty walitakiwa kukemea tukio la wafuasi wa CCM kukatwa mapanga ndani ya Msikiti na mwananchama wa ACT Wazalendo.

Amnesty walitakiwa kukemea suala la vijana wa CCM kushambuliwa maeneo mbalimbali ya mwili na wafuasi wa CHADEMA kama mikoa ya Arusha, Morogoro, Njombe, Mbeya na kadhalika.

Swali fikirishi, ina maana Amnesty wanatetea tu wanachama wa CHADEMA? Hii ni taasisi maalumu kwa ajili ya CHADEMA? Je wana maslahi gani kwa CHADEMA ikiingiia madarakani?

Wakati huu ndio tunaona mashirika ya kipumbavu kabisa kama hili la Amnesty linalojaribu kuleta machafuko nchini kwa kivuli cha kutetea haki. Ni haki gani wanayotetea angali watanzania wameuawa bila hatia au kwa kuwa si wafuasi wa CHADEMA?

Amnesty International wanapaswa kufahamu tu kwamba Watanzania sasa wameamka, John Pombe Magufuli ameamsha watanzania. Hawako tayari tena kuona rasilimali zao zikifaidisha watu wa mataifa mengine na ambao wametukandamiza kwa kipindi kirefu.

Amnesty wanatakiwa wajue kuwa mipango yao na nia ovu waliyonayo inajulikana na haitafanikiwa dhidi ya Tanzania. Mungu aliyetuponya na Covid19 ndiye huyo huyo atakayetuepusha na wabaya wetu. Kamwe Tanzania haitaingia kwenye machafuko kama wanavyopanga na tutaendelea kuwa na amani chini ya John Pombe Magufuli.

*Niwaombe watanzania wenzangu, tuwe makini sana na hizi taasisi, wanasiasa na watanzania wenzetu ambao wamejitoa kutumika kwa maslahi ya mabeberu. Tuwakatae kwa nguvu watatuangamiza.*

*Shime Watanzania, tarehe 28/10/2020 twende tukapige kura kumchagua mzalendo wa kweli JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI kiboko ya mabeberu*
 
Back
Top Bottom