Vijana wanaokula na kulala bure hawawezi kujua kwanini watu wanalalamika maisha ni magumu

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Najua wapo watakaoniponda mimi lakini utafiti nilioufanya nimegundua vijana wanaokula na kulala bure hawawezi kujua uchungu maisha kwa sababu hawajui kwanini watu wanalalamika maisha ni magumu.

Watu ambao wameshazoea akiwa hana hela akimuomba shemeji yake anampa, akimbuomba baba anampa, akimuomba sijui anko wake anampa kula anakula bure, kulala analala bure, kitu wanachojua wengi ni kusifia watu na kupiga majungu watu.

Hivyo watu kama hawa hata mtu akilalamika life gumu yeye anakuona kama umebweteka.
 
Sio kweli.
Wengine tunashinda Lumumba kwenye viyoyozi
huku magari yamejaa full tank
 
Najua wapo watakaoniponda mimi lakini utafiti nilioufanya nimegundua vijana wanaokula na kulala bure hawawezi kujua uchungu maisha kwa sababu hawajui kwanini watu wanalalamika maisha ni magumu.

Watu ambao wameshazoea akiwa hana hela akimuomba shemeji yake anampa, akimbuomba baba anampa, akimuomba sijui anko wake anampa kula anakula bure, kulala analala bure, kitu wanachojua wengi ni kusifia watu na kupiga majungu watu.

Hivyo watu kama hawa hata mtu akilalamika life gumu yeye anakuona kama umebweteka.
Kwa mfano wakijua kweli maisha ni magumu itakupunguzia huo ugumu wa maisha?! Ifikie kipindi tukubali maisha sio magumu kwa kila mtu
 
Ugumu wa maisha haujalishi kama mtu anakula kulala bure kwasababu huo ugumu unamgusa pia anaemlisha na kumlaza bure.

Tukubaliane tu kuwa ugumu ukimgusa anemhudumia ambae anakula na kulala bure basi naye lazima aathirike.

Tatizo mleta mada unachukulia kila kitu serious sana. Usiamini kila kinachoandikwa humu labda anaeandika uwe unamfahamu personally. Watu wana fake maisha unaweza kukuta mtu anashabikia tu ujinga lakini kihalisia ni mchovu mbayaa. Ni utumwa tu wa fikra ndio shida ya watu kama hao.
 
Hata mimi nilikuwa hivyo ila tangu nianze kukaa ghetto na life la chuo yan kuna siku nalala njaa mpaka nakumbuka nyumbani ila ndo sina jinsi.Na nimegundua watanzania wengi wana maisha magumu yani watu wanatafuta pesa ya kula na bado inawapiga chenga
 
kwan huyo shemeji anatoa wap hio hela ya kumpa? baba na anko pia wao wanatoa wap ela?
 
Back
Top Bottom