Vijana wanaofaulu mitihani ya kidato cha 4 vizuri tuwaandalie kanzi data(Database) na tuwafuatilie

Kikiwo

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
1,967
1,046
Wana JF, nimejaribu kuwaza kwamba juzi kwenye matokeo ya mtiani wa kidato cha nne 2019 hawa vijana 10 au "the best 10 students" kama yule kijana Yohana kutoka mkoa wa Simiyu na wengine waliotoka shule mbalimbali nchi nzima followup yao inakuwaje badae ili tuone kama nchi yaweza kunusuru na kufaidika na akili walizonazo.

Hawa ni ma "genious" students. Hongera CRDB kwa kumutembelea Yohana na kumufungulia Bank Account ya Tsh 1.5M nakujulia hali familia yake yenye kupanga chumba kimoja kwa Book saba (Tsh7,000) kwa mwezi.

Nimependelea labda wizara ya Elimu ingeunda au kuanzisha Database yao ili ijue wazazi wao au walezi wao pamoja na kuwa na contact zao za simu hao ndugu wa karibu na hawa vijana wetu kama wanayo mawasiliano.

Wako vijana wengi utasikia Form 1V kapasua lakini sijui wanaishiaga wapi katika maisha. Kila mwaka Wizara ikiweka huu mkakati itasaidia sana kuwapa moyo katika masomo yao mpaka wamalize University na kupewa vipaumbele katika ajira kuliko kuishia kuvuta madawa ya kulevya na bangi wakati walikuwa vichwa katika masomo.

Wizara tusaidieni kubuni na kuendeleza jambo hili tafadhali.
 
Ni wazo zuri sana ila sijui kama unajua tofauti ya A ya darasani na A ya mtaani? Tuna vijana wengi sana mtaani huku wana zaidi ya hizo A za darasani ila maisha yanawapiga kwenzi sawa tu na wale ambao hawakubahatika wala kupata F ya darasani!
 
Uangaliza unahitajika sana hasa kwa yule kijana wa Iringa, yule ni genius kweli sio hawa wa FEZA nk..

Uangalizi unahitajika sana tusije kupoteza kile kipaji ambacho kinaweza kulisaidia Taifa baadaye, mfumo wa kuwasimamia na kuwalea vijana kama ndio msaada kwa baadaye kuwa na watu wenye akili kwenye mifumo ambao wanaweza kulifikisha Taifa mbali...
 
Tusiwasahau wabunifu kama yule wa Kigoma aliyeunda pikipiki, radio station, gari; Kuna jamaa Arusha ameunda tractor inatumia injini ya pikipiki, Kuna vijana wanaunda vitu vingi ila sioni amsha amsha.
 
Mku hapo ndipo tunapofeli sisi wa Tz.. Watoto wanaopass vizuri sana darasani (Wenye "A") wengi sio wazuri wa kuanzisha biashara zao bali wanatakiwa waajiliwe wapige mzigo ofisini. Hawa Mungu kawapa akili za darasani sio kwenye Biashara. Wazungu hapo ndo wanatupigia bao wanajua kuwalea vijana kama hao. Mungu hagawi mara 2 kwa mtu moja otherwise ukimukuta mtu wa aina hiyo ni "very rare" yani mara chache sana.
Wengi wenye ufaulu wa wasitani na wanaofeli ndo wazuri kwenye biashara.
 
Uangaliza unahitajika sana hasa kwa yule kijana wa Iringa, yule ni genius kweli sio hawa wa FEZA nk..

Uangalizi unahitajika sana tusije kupoteza kile kipaji ambacho kinaweza kulisaidia Taifa baadaye, mfumo wa kuwasimamia na kuwalea vijana kama ndio msaada kwa baadaye kuwa na watu wenye akili kwenye mifumo ambao wanaweza kulifikisha Taifa mbali...
Very nice comment. Alafu yule wa Iringa ni yupi na alifanya nini simukumbuki?
 
Tusiwasahau wabunifu kama yule wa Kigoma aliyeunda pikipiki, radio station, gari; Kuna jamaa Arusha ameunda tractor inatumia injini ya pikipiki, Kuna vijana wanaunda vitu vingi ila sioni amsha amsha.
Nafikiri kama hao wabunifu COSTECH iko hapa Sayansi na Technologia Kijitonyama ndo kuna makao makuu yao wana program yakusaidia kama huyo kijana. nenda pale mku usaidie kijana.
 
Ni wazo zuri sana ila sijui kama unajua tofauti ya A ya darasani na A ya mtaani? Tuna vijana wengi sana mtaani huku wana zaidi ya hizo A za darasani ila maisha yanawapiga kwenzi sawa tu na wale ambao hawakubahatika wala kupata F ya darasani!
Sisi wenye akili za darasani tunapaswa tufanye kazi za technical zaidi. Tafiti za madawa, uvumbuzi na pia kuhadhiri na kuandaa generation zijazo na wanataaluma.

Wenye akili za maisha wanapaswa wapige biashara na ujasiriamali.

Kila mtu atengenezewe fursa kulingana na uwezo aliojaliwa na Mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom