Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mheshimiwa Rais anashawishika kuwapa nafasi za juu vijana wengi wengi wenye elimu na uwezo wa kazi. Nadhani amefikia maamuzi hayo baada ya kutazama utendaji kazi wa baadhi ya vijana waliopo serikalini kwa sasa.
Rais ameiona ile nguvu ya ujana, kujituma kwao na ubunifu kazini. Amevutiwa na sifa hizo. Lakini nadhani cha muhimu sio ujana pekee, nadhani uadilifu ni muhimu sana. Sio vijana wote wenye kutambua maana pana ya kuwa waadilifu na kuridhika na kinachopatikana kihalali. Wapo vijana wenye tamaa ambao kuhongeka kwao ni jambo jepesi tu kama vile kupiga chafya.
Viongozi wengi wakubwa duniani huwa na washauri ambao ni wafanyakazi wastaafu. Barack Obama anao washauri wastaafu. Wakurugenzi wengi wa mashirika makubwa ambao wameweza kufanikiwa, wanapoandika vitabu vya kumbukumbu za maisha yao huelezea ni kwa namna gani wameweza kufaidika kupitia uwepo wa washauri ambao ni watu wenye umri mkubwa kuliko wao.
Vijana wanao umuhimu wao kwa maana ya kuwa na nguvu nyingi za kufuatilia mipango na maazimio yanayofikiwa mikutanoni lakini wazee ni muhim sana kikazi kwani wanao ule utulivu kabla ya kutoa maoni yao, wanayo hazina ya matukio mengi waliyoyahifadhi vichwani mwao.
Nadhani mheshimiwa Rais aweke balance kati ya wazee na vijana, pande zote hizo mbili siku zote huwa na mchango wa maana katika ufanikishaji wa malengo yanayokusudiwa.