Vijana wamsimamisha Kikwete Mwanjelwa; wazomea "fisadi fisadi"

Gottee,

Ni kweli JK kafika Mbeya jana na leo ndio kaelekea Rungwe. JK hana ziara ya wilaya ya Mbeya mpaka Jumatatu. Sasa hii ya kuzomewa inatoka wapi?

Msafara wa rais unapopita barabarani watu wanajipanga na kila mtu kuongea la kwake. Sasa kama huko ndio kuzomea, basi kazi ipo. Vipi na wanaoshangilia mbona hukuelezea?

Ulivyoandika ilikuwa inaleta impression kwamba rais alikuwa anazomewa kama walivyofanyiwa wale mawaziri mwaka jana kitu ambacho sio kweli. Vijana walikuwa wanatoa dukuduku zao kama ambavyo wanatoa sehemu mbalimbali ambako JK anapita
.
NI MANENO YANGU AU YAKO MTANZANIA?

NINAWASIHI WATANZANIA KUWA WENYE NIDHAMU NA KUHESHIMIANA KWA MDOGO NA MKUBWA.

FDR.Jr

Hao ni kina Spin doctors on duty!!!
 
Teh teh teh,watu bwana.Vituko tu kila sehemu.Sijui Ufisadi ulikua hauhusuiani na jk? Na kwa nini wananchi waonyeshe frustration zao za kuchukia mafisadi marra tu walipomuona Jk?

Ok,Tuchukulie JK ni Sheikh au Askofu au Kiongozi mwadilifu na msafi sana,Hivi ingeingia akilini kweli kama wananchi wangemuona tu na kuanza kuonyesha kilichoitwa frustrations za kuchukia ufisadi? Ingekua irrelevant kweli?

Sometimes kabla watu hatujapost ni bora tufikirie mara mbili maanke tutakua vituko forever.Kwi kwi kwi

Unajua nyie hamjamuelewa mtanzania,ambacho hataki yeye ni suala la kikwete kuzomewa basi,ila neno lingine unaweza kutumia hata kama litakuwa na maana sawa na kuzomewa,kama hilo la fruatration za kuchukia ufisadi hana tatizo nalo.lakini usiongelee suala la muungwana kuzomewa
 
Gottee unajua viungo,ufanya chakula kuwa kitamu sana tena chenye ladha ya kupendeza,ila vikizidi kipimo nakuhakikishia uwezi kula.Tumekusikia mkuu na kila mtu amekuelewa kwani viungo vinakaribia kuzidi

Kivipi? Una uhakika kila Mtu kanielewa akiwemo MTANZANIA na ndugu yake Nungunungu?
 
Baada ya post zaidi ya 60, naona malumbano bado yanaendelea. Tujadilini yale ya msingi.
 
Kuzomewa kazomewa tena hiyo ni cha mtoto! Sana sana tumuombee arejee vyema wasije Mtikila akiwakata dry zake za sitembei na fuko la fedha!
 
Wale wenye habari zozote ziwekeni hapa; JF siyo kituo cha habari ambapo kuna wahariri n.k hapa ni self-censoring na kujiwabisha wewe mwenyewe. Hii ni forum ambapo mawazo na maoni mbalimbali yametolewa; Tusiingie kwenye mtego wa kujifanya sisi ni chombo cha habari, we are not.

Yawezekana tulikuwa na influence ya habari n.k lakini kamwe tusijekugeuka baraza la habari la Tanzania ambapo waandishi wanatuletea habari, tunazipima ukweli wake halafu tunaziapprove. Hapa ni kuleta mawazo, maoni, habari, kero n.k na kuziweka hadharani na kila mtu analazimika kuzipima, kuzikubali au kuzipinga. Ndio maana wakati mwingine inachekesha watu wanapodai "ushahidi" kana kwamba wamejijengea ka "mahakama" ka aina fulan hivi.

JF tusipoteze nafasi yetu ya kuwa sehemu ya fikra, hoja, maoni, mabishano, kugonganisha vichwa n.k tukipoteza hilo (na dalili zipo) tutakuwa irrelevant. We can not become irrelevant.
 
Gottee,

Ni kweli JK kafika Mbeya jana na leo ndio kaelekea Rungwe. JK hana ziara ya wilaya ya Mbeya mpaka Jumatatu. Sasa hii ya kuzomewa inatoka wapi?

Msafara wa rais unapopita barabarani watu wanajipanga na kila mtu kuongea la kwake. Sasa kama huko ndio kuzomea, basi kazi ipo. Vipi na wanaoshangilia mbona hukuelezea?

Ulivyoandika ilikuwa inaleta impression kwamba rais alikuwa anazomewa kama walivyofanyiwa wale mawaziri mwaka jana kitu ambacho sio kweli. Vijana walikuwa wanatoa dukuduku zao kama ambavyo wanatoa sehemu mbalimbali ambako JK anapita
.
NI MANENO YANGU AU YAKO MTANZANIA?

NINAWASIHI WATANZANIA KUWA WENYE NIDHAMU NA KUHESHIMIANA KWA MDOGO NA MKUBWA.

Mkuu FDR.jr,

Hayo ni maneno yangu, lakini kweli sijakuelewa, wapi nimesema JK hajapita Mwanjelwa? Kama kuna kitu hukuelewa basi uliza lakini maana uliyoichukua na maana niliyokuwa naandika ni tofauti kabisa.

Pili hii ya kuheshimiana mdogo kwa mkubwa inatoka wapi? Binafsi muda wote najitahidi kutomjadili mtu na ku concentrate kwenye hoja. Lakini hata kwenye maisha ya kawaida huwezi kukuta nikimdharau mtu yeyote.
 
Mtanzania,

Source yangu inasema mheshmiwa alikutana na watu waliokuwa wanapiga kelele za "mafisadi" "mafisadi"!.

Ndo kuzomewa au?
 
Mkuu Gottee,
Nimekuelewa habari nzuri saaaaana,asiyetaka kuamini shauri yake.
Najua wapo baadhi ya wanajf waliotaka uandike JK kapokelewa kwa vifijo Mbeya.
Wananchi wa Mbeya wanawakilisha maoni ya watanzania wote,huyu jamaa kashindwa kuwafikisha mahakamani mafisadi wananchi wa Mbeya wamempatia salamu nzuri sana.
 
Mtanzania,

Source yangu inasema mheshmiwa alikutana na watu waliokuwa wanapiga kelele za "mafisadi" "mafisadi"!.

Ndo kuzomewa au?

Jamani I am missing something hapa, si dhani kama kumshangilia kwa mafisadi, mafisadi, mafisadi ni dalili nzuri kwa kiongozi wa nchi ama Am I getting Paranoid?
 
Mtanzania,

Source yangu inasema mheshmiwa alikutana na watu waliokuwa wanapiga kelele za "mafisadi" "mafisadi"!.

Ndo kuzomewa au?

FairPlayer,

Sijui mkuu, hivi Dr. Slaa akipokewa na vijana wanaopiga kelele za Mafisadi ina maana wanamzomea yeye? Huenda wanamshangilia kwa kazi nzuri ya kupambana na mafisadi.

Kwa JK watu wako frustrated na vita vya mafisadi na wangetaka achukue hatua, je huko ni kumzomea yeye? Sijui mkuu.
 
Mkuu lets put this way, JK ashangiliwa na kelele kubwa mafisadi, mafisadi mafisadi, hakuzomewa hope this will make u happier .....wikiend njema!
 
Mkuu lets put this way, JK ashangiliwa na kelele kubwa mafisadi, mafisadi mafisadi, hakuzomewa hope this will make u happier .....wikiend njema!

Ushirombo,

Zoezi limegeuka kutoka subject kuwa JK kuzomewa na sasa Mtanzania kawa ndio subject?

Kama ni suala la mimi kufurahi au kutokufurahi usijali mkuu, I am strong enough to be able take care of myself. Jadili hoja iliyopo mbele yetu na mambo ya Mtanzania mwachie Mtanzania.
 
Nimekupata Mtanzania. Labda walikuwa wanashangilia kuwa amefanya vyema kuhusu mafisadi!
 
Jamaa inaonekana halikuwa hakujui, ukichanganya na machungu haya ya umasikini kwa kila mtanzania, nina wasiwasi unaweza kumeza mtu. Pamoja na kwamba inawezekana ukawa na hasira sana, maneno haya (hayo yalokiza)ni ya kweli hasa wala haujaongopa,watu wamechoka huo ndo ukweli

It is so true, inabidi wabadilishe slogan

Wale wenye habari zozote ziwekeni hapa; JF siyo kituo cha habari ambapo kuna wahariri n.k hapa ni self-censoring na kujiwabisha wewe mwenyewe. Hii ni forum ambapo mawazo na maoni mbalimbali yametolewa; Tusiingie kwenye mtego wa kujifanya sisi ni chombo cha habari, we are not.

Mzee umeteleza.

.
 
kama mawaziri wake walizomewa Mbeya, iweje yeye asizomewe? wasio mzomea kwa makelele wanamzomea kimya kimya!

Hivi kama Kikwete angepita mahali ambapo kundi la wana JF wamekaa, asingezomewa kwakweli?

Amezomewa kwasababu ya usanii wake. hakuna la maana alilofanya huyu toka aingie madarakani. Ahadi zake hewa hakuna hata aliyoitekeleza. hakuna ajira, na maisha yanazidi kuwa ngangari.

hivi Mbeya na marekani wapi mbali? au kati ya wananchi wa mbeya na wamarekani, nani walimpa kura Jakaya?
 
Jamani Kiswahili kigumuu....aaaghh!!,

.........zile kelele ni big embarassment kwa msafara wa JK.......hee....siku hizi wala ndizi wenzetu "wanashangilia" kinyume nyume.......dah!
 
Ohhh,
Niseme tu kuwa namfahamu Mtanzania kwa muda mrefu. ukisema kuwa yeye ni PRO-JK basi utakuwa unakosea. Naanza kuelewa ni nini hasa anakisema Mtanzania. Watu wenye matatizo huwa wakiona mwanga kwa mbali basi wanafikiri wameokolewa na kumbe unakuta ni macho ya Fisi au Simba gizani. Wakati wa uchaguzi mwaka 1995, nakumbuka kumshangilia sana Mrema. Na kila lililotokea nililishangilia sana. Utamu ulinoga pale Nyerere alianza kuisagia CCM kuwa imeoza. Nikajua basi yuko upande wa Mrema. nakumbuka wakati ule wakili mmoja aitwaye Wambali aliniambia neno moja kuwa "Kijana humfahamu Nyerere, wee subiri tu uone...." Na kweli nilikuja ona kuwa si Mrema ila Mkapa. Nafikiri haya ya kusikia FISADI na kufikiri JK kaisha, tunaweza kuwa tunajipa maneno matamu ambayo watu wengi wanataka kuyasikia. Ikijafika mwaka 2010, tukapigwa bao jingine na JK na 2015 akatuachia Membe. Don't under-estimate Muungwana. Kakulia na kasomea Siasa. Kakaa nje sana na kucheza SIASA anajua.
Mie nimeelewa hivyo, inawezekana siko sawa.
 
Tofauti ya Slaa na JK kuimbiwa "mafisadi, mafisadi" na kadamnasi ni kwamba kwa Slaa ni kwa sababu he has done something about them na kwa JK he has not. Simple as that.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom